Wadau mmesikia haya ya Zanzibar... CUF imepigwa chenga ama ?

Wadau mmesikia haya ya Zanzibar... CUF imepigwa chenga ama ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,906
Date::11/24/2009Shamhuna,Khatib watia doa shangwe ya Karume, Maalim Seif
broken-heart.jpg
Na Salma Said, Zanzibar
Â
WAKATI Zanzibar ikiendelea kushangilia maafikiano ya kihistoria baina ya Rais Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Serikali ya Mseto, mawaziri wawili wamejitokeza hadharani kutia doa shangwe hizo.

Wameeleza bayana kuwa Serikali ya Mseto si muhimu visiwani hapa.

Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Muungano), Mohammed Seif Khatib, wametofautiana na msimamo wa Karume ambaye alisema kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali ya Mseto ni wa Wazanzibari wenyewe.

Tamko hilo la Karume alilitoa siku chache baada ya kukutana kwa faragha na Maalim Seif, ambaye baadaye aliitisha mkutano wa hadhara na kueleza kuwa CUF imeamua kumtambua rais huyo kwa kuwa kufanya hivyo kutarahisisha mazungumzo ya kutafuta muafaka.

Lakini Shamhuna, ambaye pia ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali kinachotakiwa ni kujenga utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi ya kushinda na kushindwa.

Alisema hayo katika kipindi cha “Harakati za Kisiasa” kinachorushwa hewani kila siku ya Jumanne na kituo cha redio cha Zenji FM, ambacho kinamilikiwa na Waziri Seif.

Tamko hilo la Shamhuna lilirudiwa kwa siku tatu mfululizo; Jumapili, Jumatatu na jana asubuhi, kuonyesha kuwa hakuna haja ya ajenda hiyo ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwenye mazungumzo ya muafaka baina ya vyama hivyo viwili vikuu visiwani Zanzibar.
Â
“Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa wala serikali ya nini hapana, la msingi ni tujenge utamaduni wa kukubali kushindwa na kushinda... tukijenga utamaduni huo tutafanya kazi kwa pamoja na rais atakayeingia madarakani atachagua watu wenye uwezo wa kufanya kazi,” alisema Shamhuna.
Â
Shamhuna alisema watu wengi wanafikiri kwamba suluhisho la mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na serikali hiyo ndio itakayoweza kuondoa matatizo yaliyopo, lakini hilo sio sahihi kwa kuwa hata ikiundwa serikali ya umoja matatizo bado yataendelea kuwepo.

“Masuala yaliyopo yanatokana na baadhi yetu kuweka mbele umimi na si utaifa kwa hivyo kuundwa au kutokuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hakutusaidia,” alisema.

“Kadiri umimi utakavyokuwepo miongoni mwetu wana siasa, tatizo bado litaendelea. Solution (suluhisho) ni kuondoa umimi. Hakuhitajiki hotuba wala hakuhitajiki mikutano, kunataka management,” alisema Shamhuna kwa kujiamini.

Shamhuna alikwenda mbali zaidi na kusema watu wanasahau kwamba Zanzibar ni nchi ya kimapinduzi na wanadhani kwamba ni nchi ya watu kupiga kura na kutangazwa tu huku wengine wakifikiri kuwa Zanzibar ni nchi yenye watu walegevu legevu.
Â
Lakini hakufafanua anamaanisha nini, ingawa suala la mapinduzi limekuwa likizua mgogoro baina ya wafuasi wa vyama hivyo viwili, baadhi wakipinga mapinduzi hayo na wengine wakiunga mkono.

Akizungumzia urais, Shamhuna alisema Zanzibar haihitaji rais kijana wala mzee, lakini inahitaji rais meneja ambaye ataweza kuwakusanya watu wote pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Â
“Karume anamaliza muda wake; nikiulizwa tunataka rais wa aina gani nitajibu tunataka rais meneja (kiongozi) sijui nimefahamika,” alisema waziri huyo machachari.
“Kwa hapa tulipofikia, tunataka tuwe na kiongozi meneja na sio lazima awe kijana kama wengi mnavyodhani. Zanzibar hatutaki rais kijana wala mzee, tunataka meneja ili aweze kuondoa challenges (changamoto) zote...sasa nani ana quality (ubora) ya umeneja,” alihoji.
Â
Alisema rais wa aina hiyo atachagua watu wenye kuweza kufanya kazi hata bila ya kujali ametoka wapi.
Â
“Sio huyu anatoka wapi na huyu anatoka wapi watu ni inclusive government (serikali inayojumuisha) na sio idadi ya watu kutoka chama cha siasa... tufanye hivyo kwa matakwa yetu na sio kulazimishwa, hapo tutajenga umoja na tutafanya kazi.”
Â
Shamhuna alisema mbio za urais kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2010 tayari zimeshaunda makundi zaidi ya matatu na kwamba tayari wapo watu wameshaanza kupigia debe viongozi wao. Alisema watu hao wameanza kutoa lugha za vitisho kuwa mgombea wa kundi lao asipopitishwa na CCM, hawatakipigia kura chama hicho.
Â
“Tunawasikia wanasema hivyo wengine wanasema sasa ni zamu yetu; wengine wanasema sisi vijana tuchagueni ili tufanye mabadiliko ya nchi; wengine wameamua kunyamaza kimya; tegemeo lao hatulijui. Sasa tuna makundi matatu mpaka manne hivi yanayotafuta urais wa Zanzibar,” alisema Shamhuna. Â
Â
Akizungumzia suala linalopendekezwa na baadhi ya watu kuwa safari hii rais atoke Pemba ili kupunguza joto la kisiasa, Shamhuna aliwaita watu wenye mapendekezo hayo kuwa wamefilisika kisiasa.
Â
“Zanzibar hatuchagui rais kwa zamu na suala la kusema sasa zamu yetu Wapemba; zamu yetu  Waunguja limekwisha. Hiyo ni hoja batili na anayezungumza lugha hiyo sijui nimuite kwa lugha gani,” alisema Shamhuna.
Â
“Rais Amani anaondoka na Rais Kikwete anaendelea kipindi cha pili na hapa mitazamo tofauti kwa kuwa anayeondoka anataka arithiwe na ni nani huyo wa kurithi?

“Muungano unataka apatikane mtu kutoka Zanzibar ambaye ataweza kufanya naye kazi hivyo ndio mitizamo miwili ya msingi hii, mitizamo ya kuwa anatoka Pemba au Unguja ni mitizamo ya umimi na huko ni kufilisika kisiasa kwa jinsi navyoangalia suala hilo haraka haraka.”
 Â
Naye Waziri Seif, ambaye anatajwa kama mmoja wa watu wanaoweza kujitokeza kuwania urais wa Zanzibar, aliwaambia wananchi wa kisiwani Pemba wiki hii kwamba umoja wa Wazanzibari hauhitaji kushirikishwa chama kingine chochote kwa kuwa CCM pekee inaweza kuweka umoja na mshikamano kwa kuwa hiyo ndio sera ya chama hicho.

Aliwaambia wananchi wa kisiwa hicho kwamba MwanaCCM wa Pemba anakuwa ni CCM wa kweli kweli kwa kuwa wanakabiliana na mambo mbalimbali yanayofanywa na wapinzani, lakini wameweza kumudu na kuvumilia bila ya kutoka katika chama hicho.

“Nikwambieni ndugu zangu kuwa katika suala la umoja hakuna haja ya kushirikiana na chama kingine kwani CCM wenyewe tunaweza sana kuwaunganisha Wazanzibari wote. Na huku Pemba, CCM anakuwa wa kweli kweli maana vitimbi na vituko anavyofanyiwa na wafuasi wa CUF ni vingi, lakini bado anaweza kubakia kuwa CCM, hilo si jambo dogo,” alisema Khatib katika kipindi kilichorushwa na Zenj FM wakati wa ziara yake kisiwani Pemba.

Hii ni mara ya pili kwa Waziri Shamhuna kupingana na viongozi wakuu wa nchi katika kipindi cha miaka mitatu. Oktoba 5, 2006 Shamhuna alipingana na Rais Kikwete kuhusu suala la mwafaka wa Zanzibar.

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema utatuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar umefikia mahali pazuri, Shamhuna, aliibuka na kusema kamwe serikali ya umoja wa kitaifa au ya mseto haitaundwa visiwani.

Shamhuna alitoa msimamo alipokuwa akiwahutubia viongozi wa ngazi mbalimbali na wazee wa CCM wa Kikombweni Wilaya ya Kaskazini A, Unguja na hotuba hiyo kutangazwa na vyombo vya habari vya SMZ.
 "Hakuna Serikali ya Mseto itakayoundwa nchini kama inavyodaiwa na viongozi wa chama cha upinzani," alisema Shamhuna.
Tuma maoni kwa Mhariri
Facebook
 
Wewe yanakuhusu nini? yako ya Chadema yanawashinda.....
 
Uzuri wa Shamhuna huwa ni mkweli na haumi maneno! Karume anapodai kuwa suala la serikali ya mseto anawaachia Wazanzibari wenyewe ni kuuma maneno bila kuelezea ukweli wa mambo! Seif na Libumba mmeliwa mchana kweupeee!
 
Wewe yanakuhusu nini? yako ya Chadema yanawashinda.....
Kaka CUF ni chama cha kisiasa..kwa Tanzania nzima kinategemewa kuchukua nchi na kuongoza wananchi wote ..wanachama na wasio wanachama..hivyo kina mhusu kila mtu Mtanzania..so usituambia haimhusu

Mimi nilijua hili deal ni maumivu kwa CUF na ikifika 2010 kazi yenu ndio imekwisha..mgawanyiko kati ya wanachama na viongozi ..take my words.
 
Seif atawekwa na labda kufukuzwa chama maana amepata amani na kula kwa mgongo wa marehemu walio mwaga damu. Waha tuone na majibu ya CUF yatakuwaje. Hivi Zanzibar kuna viongozi wakuu wangapi ?
 
Seif atawekwa na labda kufukuzwa chama maana amepata amani na kula kwa mgongo wa marehemu walio mwaga damu. Waha tuone na majibu ya CUF yatakuwaje. Hivi Zanzibar kuna viongozi wakuu wangapi ?

Wapo wachache lakini nguvu zao ni kubwa kiasi kulitikisa Bunge la Tanzania na Rais wake, mfano mmoja ni ule wa BUTIAMA walipofoka kidogo tu Bunge zima lilitulia kama vile wapo kwa kinyozi.
 
sidhani kama mkutano wa seif na karume ulikuwa na lengo la kuunda serikali ya mseto, ule mkutano ulikuwa na mamlaka makugwa zaidi, and that was interest of zanzibaris

Tuache kauchochezi
 
Wewe yanakuhusu nini? yako ya Chadema yanawashinda.....

Nd. Masatu,
Tafadhali zihurumie mbavu zetu!!!
Hayo aliyoyasema Shamhuna ndio msimamo wa SMZ na yale ya Karume ilikuwa babaisha ***** tu! Kwa kweli inatia uchungu, Maalim Seif baada ya miaka zaidi ya 10 ndio sasa anajua maslahi ya Wa-zanzibari? Sasa zogo lote lile lilikuwa la nini? Kwa mimi Seif ndio awe wa mwanzo kupandishwa mahakamani kwa kuwarejesha nyuma Wa-zanzibari kwa ugomvi ambao kumbe sio wa kweli.
 
sidhani kama mkutano wa seif na karume ulikuwa na lengo la kuunda serikali ya mseto, ule mkutano ulikuwa na mamlaka makugwa zaidi, and that was interest of zanzibaris

Tuache kauchochezi

Utashangaa wengi wanye maoni hasi kuhusu Znz ni watu wa bara! Wengi wao wanayajua yanayotokea Znz kwa kusoma magazetini...(waandishi wetu mnawajua vizuri)...hawana taarifa sahihi kuhusu hali za wazanzibari na ugumu wa maisha yao. Shamhuna! Kati ya wote! Hivi yeye na dada yetu "Asha Ngedere" wana tofauti?
 
habari za siasa jamani zinaumiza kichwa huwezi fanya jambo likaonekana zuri
na huwezi kumfurahisha kila mtu
 
si jambo la kushangaza kuona Shamhuna hayuko na Karume katika hilo lakini nashangaa kusikia Mohamed Khatibu naye yumo. Niliamini kwamba Khatibu amewiva kisiasa na anapenda maendeleo kumbe sivyo. Maamuzi ya Karume na Maalim Seif ni ya kushangiliwa na watu wote wapenda amani na maendeleo. Shamhuna siku zote hudhihirishwa kwamba ana mawazo mgando.
 
watu mnahukumu mambo yangali mapema tuvuteni subira tuoni yatakayoendelea, sisi tuombeni kwa MUNGU yawe mazuri ili watu waishi kwa amani na upendo na waijenge ZANZIBAR yao
 
Kuna chenga gani hapo?

Mkuu hata mimi nshangaa, hakuna chenga... sometime ukizoea sana jungu, hata ukiambia "habari gani" unaanza kuhisi jamaa ananipiga jungu!!!

Tanzania ngumu sana aisee!!
 
Date::11/24/2009Shamhuna,Khatib watia doa shangwe ya Karume, Maalim Seif
broken-heart.jpg
Na Salma Said, Zanzibar
Â
WAKATI Zanzibar ikiendelea kushangilia maafikiano ya kihistoria baina ya Rais Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Serikali ya Mseto, mawaziri wawili wamejitokeza hadharani kutia doa shangwe hizo.

Wameeleza bayana kuwa Serikali ya Mseto si muhimu visiwani hapa.

Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Muungano), Mohammed Seif Khatib, wametofautiana na msimamo wa Karume ambaye alisema kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali ya Mseto ni wa Wazanzibari wenyewe.

Tamko hilo la Karume alilitoa siku chache baada ya kukutana kwa faragha na Maalim Seif, ambaye baadaye aliitisha mkutano wa hadhara na kueleza kuwa CUF imeamua kumtambua rais huyo kwa kuwa kufanya hivyo kutarahisisha mazungumzo ya kutafuta muafaka.

Lakini Shamhuna, ambaye pia ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali kinachotakiwa ni kujenga utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi ya kushinda na kushindwa.

Alisema hayo katika kipindi cha âHarakati za Kisiasaâ kinachorushwa hewani kila siku ya Jumanne na kituo cha redio cha Zenji FM, ambacho kinamilikiwa na Waziri Seif.

Tamko hilo la Shamhuna lilirudiwa kwa siku tatu mfululizo; Jumapili, Jumatatu na jana asubuhi, kuonyesha kuwa hakuna haja ya ajenda hiyo ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwenye mazungumzo ya muafaka baina ya vyama hivyo viwili vikuu visiwani Zanzibar.
Â
âZanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa wala serikali ya nini hapana, la msingi ni tujenge utamaduni wa kukubali kushindwa na kushinda... tukijenga utamaduni huo tutafanya kazi kwa pamoja na rais atakayeingia madarakani atachagua watu wenye uwezo wa kufanya kazi,â alisema Shamhuna.
Â
Shamhuna alisema watu wengi wanafikiri kwamba suluhisho la mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na serikali hiyo ndio itakayoweza kuondoa matatizo yaliyopo, lakini hilo sio sahihi kwa kuwa hata ikiundwa serikali ya umoja matatizo bado yataendelea kuwepo.

âMasuala yaliyopo yanatokana na baadhi yetu kuweka mbele umimi na si utaifa kwa hivyo kuundwa au kutokuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hakutusaidia,â alisema.

âKadiri umimi utakavyokuwepo miongoni mwetu wana siasa, tatizo bado litaendelea. Solution (suluhisho) ni kuondoa umimi. Hakuhitajiki hotuba wala hakuhitajiki mikutano, kunataka management,â alisema Shamhuna kwa kujiamini.

Shamhuna alikwenda mbali zaidi na kusema watu wanasahau kwamba Zanzibar ni nchi ya kimapinduzi na wanadhani kwamba ni nchi ya watu kupiga kura na kutangazwa tu huku wengine wakifikiri kuwa Zanzibar ni nchi yenye watu walegevu legevu.
Â
Lakini hakufafanua anamaanisha nini, ingawa suala la mapinduzi limekuwa likizua mgogoro baina ya wafuasi wa vyama hivyo viwili, baadhi wakipinga mapinduzi hayo na wengine wakiunga mkono.

Akizungumzia urais, Shamhuna alisema Zanzibar haihitaji rais kijana wala mzee, lakini inahitaji rais meneja ambaye ataweza kuwakusanya watu wote pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Â
âKarume anamaliza muda wake; nikiulizwa tunataka rais wa aina gani nitajibu tunataka rais meneja (kiongozi) sijui nimefahamika,â alisema waziri huyo machachari.
âKwa hapa tulipofikia, tunataka tuwe na kiongozi meneja na sio lazima awe kijana kama wengi mnavyodhani. Zanzibar hatutaki rais kijana wala mzee, tunataka meneja ili aweze kuondoa challenges (changamoto) zote...sasa nani ana quality (ubora) ya umeneja,â alihoji.
Â
Alisema rais wa aina hiyo atachagua watu wenye kuweza kufanya kazi hata bila ya kujali ametoka wapi.
Â
âSio huyu anatoka wapi na huyu anatoka wapi watu ni inclusive government (serikali inayojumuisha) na sio idadi ya watu kutoka chama cha siasa... tufanye hivyo kwa matakwa yetu na sio kulazimishwa, hapo tutajenga umoja na tutafanya kazi.â
Â
Shamhuna alisema mbio za urais kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2010 tayari zimeshaunda makundi zaidi ya matatu na kwamba tayari wapo watu wameshaanza kupigia debe viongozi wao. Alisema watu hao wameanza kutoa lugha za vitisho kuwa mgombea wa kundi lao asipopitishwa na CCM, hawatakipigia kura chama hicho.
Â
âTunawasikia wanasema hivyo wengine wanasema sasa ni zamu yetu; wengine wanasema sisi vijana tuchagueni ili tufanye mabadiliko ya nchi; wengine wameamua kunyamaza kimya; tegemeo lao hatulijui. Sasa tuna makundi matatu mpaka manne hivi yanayotafuta urais wa Zanzibar,â alisema Shamhuna. Â
Â
Akizungumzia suala linalopendekezwa na baadhi ya watu kuwa safari hii rais atoke Pemba ili kupunguza joto la kisiasa, Shamhuna aliwaita watu wenye mapendekezo hayo kuwa wamefilisika kisiasa.
Â
âZanzibar hatuchagui rais kwa zamu na suala la kusema sasa zamu yetu Wapemba; zamu yetu  Waunguja limekwisha. Hiyo ni hoja batili na anayezungumza lugha hiyo sijui nimuite kwa lugha gani,â alisema Shamhuna.
Â
âRais Amani anaondoka na Rais Kikwete anaendelea kipindi cha pili na hapa mitazamo tofauti kwa kuwa anayeondoka anataka arithiwe na ni nani huyo wa kurithi?

âMuungano unataka apatikane mtu kutoka Zanzibar ambaye ataweza kufanya naye kazi hivyo ndio mitizamo miwili ya msingi hii, mitizamo ya kuwa anatoka Pemba au Unguja ni mitizamo ya umimi na huko ni kufilisika kisiasa kwa jinsi navyoangalia suala hilo haraka haraka.â
 Â
Naye Waziri Seif, ambaye anatajwa kama mmoja wa watu wanaoweza kujitokeza kuwania urais wa Zanzibar, aliwaambia wananchi wa kisiwani Pemba wiki hii kwamba umoja wa Wazanzibari hauhitaji kushirikishwa chama kingine chochote kwa kuwa CCM pekee inaweza kuweka umoja na mshikamano kwa kuwa hiyo ndio sera ya chama hicho.

Aliwaambia wananchi wa kisiwa hicho kwamba MwanaCCM wa Pemba anakuwa ni CCM wa kweli kweli kwa kuwa wanakabiliana na mambo mbalimbali yanayofanywa na wapinzani, lakini wameweza kumudu na kuvumilia bila ya kutoka katika chama hicho.

âNikwambieni ndugu zangu kuwa katika suala la umoja hakuna haja ya kushirikiana na chama kingine kwani CCM wenyewe tunaweza sana kuwaunganisha Wazanzibari wote. Na huku Pemba, CCM anakuwa wa kweli kweli maana vitimbi na vituko anavyofanyiwa na wafuasi wa CUF ni vingi, lakini bado anaweza kubakia kuwa CCM, hilo si jambo dogo,â alisema Khatib katika kipindi kilichorushwa na Zenj FM wakati wa ziara yake kisiwani Pemba.

Hii ni mara ya pili kwa Waziri Shamhuna kupingana na viongozi wakuu wa nchi katika kipindi cha miaka mitatu. Oktoba 5, 2006 Shamhuna alipingana na Rais Kikwete kuhusu suala la mwafaka wa Zanzibar.

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema utatuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar umefikia mahali pazuri, Shamhuna, aliibuka na kusema kamwe serikali ya umoja wa kitaifa au ya mseto haitaundwa visiwani.

Shamhuna alitoa msimamo alipokuwa akiwahutubia viongozi wa ngazi mbalimbali na wazee wa CCM wa Kikombweni Wilaya ya Kaskazini A, Unguja na hotuba hiyo kutangazwa na vyombo vya habari vya SMZ.
 "Hakuna Serikali ya Mseto itakayoundwa nchini kama inavyodaiwa na viongozi wa chama cha upinzani," alisema Shamhuna.

Zanzibari's must move on and forge unity.Retrogressive wabaguzu type who thrive on divisive politics wapuuzwe tu.Hawana jipya!
 
Nyote hamuelewi ya CCM (ZnZ), Karume anajaribu kuunda nguvu dhidi ya Bilal (mpinzani wake na mwenye nguvu zaidi) kwa kuwatumia CUF lakini sidhani kama itamsaidia. CUF hawana matatizo, ila mata6tizo anayo Maalim Seif kwa Kutaka madaraka ambayo hawezi kuyapata.
 
asojua kitu haambiwi kitu shamhuna ana ukweli gani ungekuwa unajua basi bora usingesema kitu la kushangaza wengi wanao leta mada ya zanzibar basi hata huko zanzibar hawajafika wao wanasikia kwenye news tu shamhuna si lolote si chochote yeye ni msaka tonge tu yuko katika kutapatapa tu ili aonekane nae kasema na jua kila kitu kina muda wake mabadiliko lazima yatakuja tu zanzibar ukipenda usipende huwezi kuzuia hilo
 
kwa uhalisia wa hali ya mambo ndani ya zanzibar na kauli ya mh. shamhuna wallah nakwambia cuf wameliwaaa....seif na karume wamepiga deal la kilevi baa kesho yake hakuna kinachoendelea...maana matarajio ya cuf ni serikali ya mseto ..wakati matarajio ya ccm ni uchaguzi uwe wa amani na kupata sifa za demokrasia huko kwa weupe..ili misaada na kuombaomba kwetu kuwe na justification tosha...

HAPA NDIPO TATIZO LINAPOKUJA.....wao ccm wanasema walileta mapinduzi kwa upanga unadhani ni lini watampisha cuf nchi kwa maongezi ya baraza la gahawa????.....WATCH THE SHOW ...soon sterling mmoja atakafa kwenye hili movie
 
Back
Top Bottom