Wadau mnishauri hivi January hii naweza kupiga lenta

Wadau mnishauri hivi January hii naweza kupiga lenta

Nimepata vijisenti vya kuniwezesha kufunga lenta sasa naona hali ya hewa imekunja sana mvua zimeanza vipi nikifunga itakuwa poa? maana kukaa na pesa nako ni kipaji
Si unafunga siku hakuna mvua baada ya hapo mvua ikiwa inanyesha inakusaidia kuimarisha.
Mimi nimejenga mwaka jana si masika si jua ili mradi nina pesa nasukuma tu maana pesa haikai. Sasa hivi niko npga tiles already
 
Attachments

  • Screenshot_20250105-195235.png
    Screenshot_20250105-195235.png
    134.1 KB · Views: 5
Anhaa!! Piga mkuu, sasa nyumba si itaweza kuanguka na mvua.

Unapoamua kufanya kitu usibabaishe, fanya kweli!!

Option ni mbili Fanya kwa ubora au Usifanye kabisa!! Na mvua ndiyo hua inakomaza cement!!
 
Si unafunga siku hakuna mvua baada ya hapo mvua ikiwa inanyesha inakusaidia kuimarisha.
Mimi nimejenga mwaka jana si masika si jua ili mradi nina pesa nasukuma tu maana pesa haikai. Sasa hivi niko npga tiles already
Hongera mkuu na ahsante kwa ushauri
 
Unaweza ila piga mbao za box nyumba nzima, siku ambayo kajua kametoka waambie wamwage zege..!! Kisha mvua zinakusaidia kuimwagilia ikomae..!!
 
Ndo vizur sasa inanyeshewa na kukomaa vizur kabisa
Inaweza ikawa ndiyo wamemwaga zege yakashuka maji moja mzee ikatepeta,lazima afanye timing.

Japo wakiweza kuitaim ikaja kunyesha masaa sita baada ya kumwaga zege kitatokea kitu kimoja bora sana.
 
Back
Top Bottom