Wadau mnishauri hivi January hii naweza kupiga lenta

Wadau mnishauri hivi January hii naweza kupiga lenta

Inaweza ikawa ndiyo wamemwaga zege yakashuka maji moja mzee ikatepeta,lazima afanye timing.

Japo wakiweza kuitaim ikaja kunyesha masaa sita baada ya kumwaga zege kitatokea kitu kimoja bora sana.
Na huu ndio wasiwasi wangu
 
Hakuna mvua ya kuzuia ujenzi kuanzia January hadi March. Ukiona mawingu angalia weather at your location mtandaoni utapata live weather update. Jumapilj nilikuwa na kazibya plaster na kulikuwa na mawingu. Mafundi walikuwa na wasiwasi mvua itanyesha.
Nikaingia mtandaoni nikaangalia weather mvua ilikuwa na chance ya 10% kunyesha na ikinyesha ni 0.2mm. Nikawaambia mafundi mvua haitanyesha na haikunyesha wakaniona mchawi.
 
Kipindi hiki ndio unatakiwa kukamilisha boma ili linyeshewe mwezi wa tatu hadi wa tano huko. Au kama unaezeka flat roof inabidi uezeke ili mwezi wa tatu au wa nne upate majibu.
 
Nawashukuruni wote mlionipa ushauri nimeamua kupiga lenta as soon as possible
 
Back
Top Bottom