Hawa jamaa sijui wanapataje faida
Wanadai wanatoa 70% baada ya 4 month's, Halafu ukisubiri tena baada ya miezi 6 unapata 100% kama profit
Ukijumlisha hapo ni 170% faida kwa miezi 10 hiki ni kiasi kikubwa sana cha faida ukilinganisha na biashara yenyewe tena ya ufugaji kuku + Muda wa investment
Yaani mfano niwekeze million 10 ndani ya muda wa miezi 4 nitakuwa na million 17 nikiacha tena hiyo million 17 baada ya miezi 6 nitakuwa ninetengeneza million 34
Pia Instagram kule watu wanalalamika kuwa wana hide comment za baadhi ya watu, inaonekana kuna jambo hawataki kuliweka wazi.
Pia kwa experience yangu kwenye mambo kama haya wanaofaidika ni wale wanaowekeza mapema sana sana yaani sana kabla mambo hayajaharibika, ule muda ambao kampuni haijatengeneza faida kubwa ianze janja janja, ule muda kampuni inahangaika kutafuta watu unakuta wajanja wamewekeza wanakula faida.
Mpaka sasa Mr kuku ina miaka 3 na ukiangalia vizuri bado hawajapata faida kubwa ya kusema wakimbie ndio wako katika harakati za kupanua kampuni hii ni wazi kwamba wale waliowekeza miaka 2 nyuma bado wanapiga profit inaweza kuwachukua miaka 4 mbele mpaka kampuni kufirisika unaweza kuona jinsi gani profit watakayo tengeneza waliowahi kuiona fursa
Ukiona watu wamejaa sana ujue puto limejaa upepo linakaribia kupasuka huo muda ndio nyumbu unakuta wamejazana balaa wajanja wameshajitoa hapo ndio unasikia mara kampuni imefirisika wajanja wamekimbia na pesa.
Pia kwa wale watakao enda kuwekeza nawashauri someni mikataba vizuri maana wabongo wengi hawapendi kusoma pengine wengine hawajui umuhimu wa mikataba. Kunauwezekani mkubwa mikataba yao imejaa uhuni sana wa kulinda kampuni yao.
Sent using
Jamii Forums mobile app