Hivi hawa wanatofauti gani na wale waliokuwa wanafanyia promo ufugaji wa sungura?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kule Kenya wiki jana tu wameililia serikali kwa mradi kama huu.
Bet on what you afford to lose.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa jamaa sijui wanapataje faida
Wanadai wanatoa 70% baada ya 4 month's, Halafu ukisubiri tena baada ya miezi 6 unapata 100% kama profit
Ukijumlisha hapo ni 170% faida kwa miezi 10 hiki ni kiasi kikubwa sana cha faida ukilinganisha na biashara yenyewe tena ya ufugaji kuku + Muda wa investment
Yaani mfano niwekeze million 10 ndani ya muda wa miezi 4 nitakuwa na million 17 nikiacha tena hiyo million 17 baada ya miezi 6 nitakuwa ninetengeneza million 34
Pia Instagram kule watu wanalalamika kuwa wana hide comment za baadhi ya watu, inaonekana kuna jambo hawataki kuliweka wazi.
Pia kwa experience yangu kwenye mambo kama haya wanaofaidika ni wale wanaowekeza mapema sana sana yaani sana kabla mambo hayajaharibika, ule muda ambao kampuni haijatengeneza faida kubwa ianze janja janja, ule muda kampuni inahangaika kutafuta watu unakuta wajanja wamewekeza wanakula faida.
Mpaka sasa Mr kuku ina miaka 3 na ukiangalia vizuri bado hawajapata faida kubwa ya kusema wakimbie ndio wako katika harakati za kupanua kampuni hii ni wazi kwamba wale waliowekeza miaka 2 nyuma bado wanapiga profit inaweza kuwachukua miaka 4 mbele mpaka kampuni kufirisika unaweza kuona jinsi gani profit watakayo tengeneza waliowahi kuiona fursa
Ukiona watu wamejaa sana ujue puto limejaa upepo linakaribia kupasuka huo muda ndio nyumbu unakuta wamejazana balaa wajanja wameshajitoa hapo ndio unasikia mara kampuni imefirisika wajanja wamekimbia na pesa.
Pia kwa wale watakao enda kuwekeza nawashauri someni mikataba vizuri maana wabongo wengi hawapendi kusoma pengine wengine hawajui umuhimu wa mikataba. Kunauwezekani mkubwa mikataba yao imejaa uhuni sana wa kulinda kampuni yao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo kuna uwezekano hawa jamaa ni wana mpango wa kuwapiga watizii sio? 😂😂😂
Juzi kuna jamaa yangu kanipigia simu akawa ananieleza vitu sivielewi elewi.
Ni kitu kinaitwa Mr. Kuku Farms akidai ni mradi mkubwa wa ufugaji kuku una physical presence na ni kampuni iliosajiliwa ndio inaendesha huo mradi.
Yeye ameshawishika kuwekeza huko kwamba kuna faida nzuri compared na kuweka hela benki tu ikiwa baada ya miezi 3 unaweza draw 70% ya ulichowekeza na baada ya miezi sita una uwezo wa kuchota 100% ya pesa yako.
Kama tujuavyo kwamba mtu alieng'atwa na nyoka huwa haishi maseke hata anapotambaliwa na jani, basi lazma atarusha miguu tu.
Naomba kwa heshima na taadhima niambiwe na wadau wenzangu wajasiriamali kwa wafanyabiashara. Je, huu mradi ni halisi?
Ni business model gani wanatumia? Na je, kuna hiyo leverage ya kupelekea kutoa gawio kwa rates hizo kwa muda wanaodai wanaweza?
Kama kuna ambaye amepiga hela kupitia hao jamaa aje amwage terms zao na ushuhuda kuwa kapiga dough kweli.
Tokea nipigwe laki nane yangu ya DECI na CCM...... Sitakaa nishawishike na upuuzi huu tena
Sent using Jamii Forums mobile app
Wasiwasi ndio akili babu 🤣🤣🤣🤣Kama tujuavyo kwamba mtu alieng'atwa na nyoka huwa haishi maseke hata anapotambaliwa na jani, basi lazma atarusha miguu tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hio kampuni nimefatilia inafanya chini ya kampuni ya mwarabu kama sio muhindi wa kuitwa somebody Tariq limited. Huyo ndio mkulungwa kwa hio hawa Mr.Kuku Limited ni boloka tu au bosheni ila mwenyewe yupo behind.Ingeweza kuwa viable kama wangesema wana raise mtaji kiasi hiki, kwa ajili ya huo uzalishaji wa kuku. Na kuku wakiiva wauzwe watu wapewe fedha kama gawio.
Ila kwa kutoweka kikomo maana yake watapokea kila pesa watakatopewa, sasa wana facilities za unlimited production? Wana unlimited market? Are they assured kwamba uzalishaji utakuwa kama wanavyotaka?
Mwisho wa siku watakuwa wanawalipa watu gawio kutoka kwenye wanachopokea kutoka kwa watu, then wale wa mwisho ndo itakuwa faida yao jamaa, maana watakavyopotea!
Hio kampuni nimefatilia inafanya chini ya kampuni ya mwarabu kama sio muhindi wa kuitwa somebody Tariq limited. Huyo ndio mkulungwa kwa hio hawa Mr.Kuku Limited ni boloka tu au bosheni ila mwenyewe yupo behind.
Nadhani kuna mchezo wa ki makaratasi umefanyika kwa baraka za wanasheria na mwisho wa siku yatakuwa yale yale ya jamaa kusepa na kiswaufu huku wawekezaji wakiwa hawaamini kilichowakuta. Kutumia public figure kama Joti ni kuwanyawisha tu raia ili waone kwamba kuna uhalisia.
Nimeingia maseke kuwa mwisho wa huu mchezo kuku watauzwa wote kisha mradi uta shut down ghafla. Zikianza court procedures kutakuwa na namna jamaa hawatakuwa hatiani kutokana na michezo ya kimkataba. The same as kijana wenu wa Jangid Plaza yule.
Kwa maelezo yao ni kwamba wata shut down kupokea wawekezaji ati by mid 2020 hapo. Sasa najiuliza ambao wameweka hela ndefu zaidi itakuwaje?