Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Acha masihara mkuu?
Kwa maelezo yaliyopo shida sio Mr kuku, shida ni hujuma tu za wenye mamlaka, kama kitu kimefanyiwa uchunguzi wa awali na kuonekana kampuni haina shida kwanini msiachie waendelee kufanya kazi? Mwisho wa siku mali ya shambani itakufa yote kwa kukosa matunzo na hela za watu zitaishia juu kwa juu(wameshikilia account). Ni ngumu sana kuendelea nchi hii, jamaa kiukweli walikua wamejipanga, hata usipowekeza kwa pesa ukiwa mteja tu wa bidhaa zao kwa kununua kuku wengi na wewe kuuza walikua wanaokoa sana maana una uhakika wa kupata kuku kwa wakati bila longolongo.
 

Yes inawezekana kabisa in future lazima nifanye hii kitu,watu pesa wanazo ila hawajui wawekeze wapi ukija na idea nzuri utapata watu mpaka ushangae
Nina experience na hizi kampuni na nimetulia nikafanya tafiti za marketing plan zao,zipo ambazo ni legit na nyingine ni utapeli
Hii Mr kuku ni utapeli
Value of your money in exchange of what?kama ukiwekeza laki 7 exchange yake unapewa nini?hakuna pesa rahisi uweke na utulie usubiri ijizalishe [emoji3][emoji3]nashangaa kwanini watu hawaoni huu ni utapeli
Mwanzoni lazima wawalipe ili kujenga uaminifu baadae wataondoka na hela za watu na hakuna pa kuwapeleka
 
Mzee Baba umeleta kitu chenyewe kabisa.
 
Lakini ndugu hata Desi wale wa mwanzo wale wa mwanzo si walivuna vizuri tu.
Jamaa yupo kigamboni na hivyo usemavyo ni kweli na watu wengi wamewekeza pia anasema mradi ukiwekeza unakatia na bima kusudi kujikinga na hasara,wajumbe tusubiri walau walioanza watupe feedback...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! naanza kupata picha kwa mbalii. Naona wale wa mwanzo watakula faida ili kuwavuta wengine.
 
Umesema Point
 
Njoo tuungane bas kamwali, huenda
tukawa mfano wa kuigwa 🤣🤣🤣
 
Natanguliza pole on behalf of wawekezaji!
 
Hata biashara uione nzuri kiasi gani, kama haizingatii sheria basi ni haramu.

Nenda popote Duniani, hakuna biashara inafanywa kwa namna hiyo na ikitokea inafanywa basi haiwi tena biashara inakuwa ni ponzi scheme (upatu). Ambapo nchini Tanzania upatu ni haramu.

Kwahiyo wewe msikitikie vyovyote unavyotaka, ila biashara zote zinafanywa kwa kuzingatia sheria za nchi. Kama huyo Mt. Kuku alikuwa anahitaji mitaji ya watu ili akuze biashara yake, alipaswa kujisajili kwenye soko la hisa ili hao watu wake wampelekee pesa zote anazotaka. Ila sio ujanja ujanja tu wa kupokea pesa kutoka kwa watu bila kujua pesa hizo zimepatikana vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…