Juzi kuna jamaa yangu kanipigia simu akawa ananieleza vitu sivielewi elewi.
Ni kitu kinaitwa Mr. Kuku Farms akidai ni mradi mkubwa wa ufugaji kuku una physical presence na ni kampuni iliosajiliwa ndio inaendesha huo mradi.
Yeye ameshawishika kuwekeza huko kwamba kuna faida nzuri compared na kuweka hela benki tu ikiwa baada ya miezi 3 unaweza draw 70% ya ulichowekeza na baada ya miezi sita una uwezo wa kuchota 100% ya pesa yako.
Kama tujuavyo kwamba mtu alieng'atwa na nyoka huwa haishi maseke hata anapotambaliwa na jani, basi lazma atarusha miguu tu.
Naomba kwa heshima na taadhima niambiwe na wadau wenzangu wajasiriamali kwa wafanyabiashara. Je, huu mradi ni halisi?
Ni business model gani wanatumia? Na je, kuna hiyo leverage ya kupelekea kutoa gawio kwa rates hizo kwa muda wanaodai wanaweza?
Kama kuna ambaye amepiga hela kupitia hao jamaa aje amwage terms zao na ushuhuda kuwa kapiga dough kweli.