Marcy
JF-Expert Member
- Aug 12, 2013
- 2,430
- 5,910
Kuna dada yangu mmoja alinunua kiwanja miaka ya 96 hivi na aliuziwa na mzee mwenye hilo shamba pamoja na mtoto wake wa kiume ambapo kwa sasa wote ni marehemu. Leo hii ndugu wanaanza kujitokeza na kusema hawamtambui sister katika kile kiwanja na aliuziwaje na wanasema ikiwezekana sister apigiwe hesabu na ahamekatika kile kiwanja ikishindikana watapanda mahakaman ukizingatia sister ameshajenga katika lile eneo na mpaka sasa ni miaka 20 imepita na baada ya wahusika kufariki ndio ndugu wanaanza kujitokeza. Naomba mnisaidie hapo sister ana haki gani na kwa vile walisema watampigia hesabu ahame pale utaratibu unakuwaje hapo kwa kile kiwanja kitapigiwa hesabu ya thamani ya kiwanja cha sasa au zamani?? Na hesabu yenyewe ni pamoja na nyumba na thamani nyingine????
Naomba mnisaidie kwa hili
Naomba mnisaidie kwa hili