Wadau naomba wazo la biashara, nina mtaji wa 10M-15M

Pesa hizo watu wanazitolea mate kila mtu Nipm Nipm tafuta zako na wewe tukuPM mtu kaomba ushauri hapa hadharani jitu linakuja Nipm.

Kuku kweli.

Pole mkuu, usikasirike ni kawaida sana kwa binadamu kutofautiana kimawazo.
Japo unachosema ni kweli kabisa, tena dunia hii ya sasa ni hatari, ni vigumu kumjua mwenye nia njema na mbaya!
 
Njoo ulime mpunga kisasa, Turiani.....Heka moja gunia 30....hapo utalima heka 10 gunia 300...ukiuza unakaribia milion 30
 
Hahahaaa, kuna watu mna maudhi ! Haya tufanye kashinda biko, mshauri sasa.
unajua nilishtuka kidogo nipate presha! namshauri kama yupo Dar atumie kama laki tano kule mkuranga anunue eka moja.shs mil moja achimbe kisima cha mkono,laki tano tenki la maji la lita 5000 na laki tano anunue pampu na aanze biashara ya kilimo cha matikiti kila baada ya miezi mitatu atakuwa anaingiza hela za uhakika.wanunuaji huwa wanakufuata shambani wewe waletee madalali pale kariakoo sample tu tikiti moja.ATUMIE MILIONI TANO TU KWANZA NA HIYO NYINGINE TANO AWEKE FIXED KWA MIEZI MITATU BENKI AKISIKILIZIA BIASHARA YA TIKITI KWANZA KUPATA UZOEFU WA KILIMO NA BIASHARA.
 
Kama ni nje ya dar, Fungua biashara ya soda za jumla hasa pepsi na banana na vinywaji vikali anza na konyagi, valuu, kvant na wine kama st,.ana, dodoma na nyinginezo fast moving,,, fanya tafiti eneo utakaloenda then ukiona hamna mwenye nalo weka ww ni biashara inayotoka sana hasa miji inayokuwa kama dodoma, manyara, karatu
 
kwan hizo hela umezipataje? si uendeleze hiyo biashara uliyokuwa unaifanya mpaka ukapata 15mln
 
Nitaftee nkupe bussnes plan kijana japo ni garama kidogo
 
kama unaweza kazi nakushauri uanzishe biashara ya viazi ulaya. Milioni tano tu inatosha kuanzia biashara. Bei ya shamba polo ndogo ni 20000 mpaka 25000. Bei ya sokoni ni 35 mpaka 45 inategemeana na mazingira ya soko kwa siku husika.
 
Mkuu mi nakushauri izo pesa wekeza kwenye elimu hutojutia
Ayo mamilioni yanatosha kabisa kukusomesha mpaka masters na
hapa huwezi kosa mshahara wa mil4 kwa mwezi
 
Fuga kambale, ni rahisi kuwafuga na pia hawazaliani, hivyo menejment yake ni rahisi. Anza na bwawa moja then utaongeza kidogokidogo
 
Hizo ten nikopeshe Mimi kwa muda wa Siku 90 nitakurudishia 15 na Mimi nitachukua ten zangu.
 
Nipo mm na mwenzangu, sisi tunaelimu ya marketing, tupo kwenye harakati za mwisho za kuanzisha biashara yetu ya chakula kwa hali ya kisasa,,yan tukizingatia vigezo vyote vya biashara ikiwepo packaging nzuri,,tupo mwanza hivyo tunakaribisha mtu mwenye kuweza kuwekeza(share holders),
Kama unaweza tutafutane kwa namba 0689672589.
Thanks
 
Mkuu its a lot of money kama hujawai kufanya biashara,ushauri wangu tumia nusu au robo ya pesa kuanzia kwani kwa uzoefu wangu mdogo(nina miezi sita tokea nianze biashara) huwa hivi
(1)mzigo wa kwanza huwa haunaga faida kwa sababu
(a)ndugu hutaka punguzo
(b)mtu huwa na huruma akijua anawavutia wateja kwa hyo hutoa mapunguzo
(c)majirani watajiaminisha kwako kwa kukopa na kulipa mara kadhaa ila atakupga moja nzito hutazpata ng'o
(d)waumin wenzako either wakanisani au wapga gambe hawataacha kukopa
(2)malipo ya pango
(3)malipo ya vibali vya TRA(hapa wengi hupgwa sana huonga mnoo)
so ukitumia zote mtaji utapuputka ila ilagmzigo wali mtajmtajirunarudadfaidaa utakutakua umejifunza mwanzoo hapo ongezea ile uloiweka
NB.hakuna wazo nimekupa mana sijui unaishi wapi na mazngizra yake yapoje ila nmekupa angalizo usije poteza peesa badala ya kuuuzalisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…