Niliwahi kufanya biashara maeneo ya tiptop ya duka la jumla nikawa napata faida nzuri tu, ila baadae yaanza mauza uza ya pesa kupotea bila kuonekana... Nikaanza kuamini kuna chuma ulete, mzee mmoja akaniambia niwe naweka mkaa kwenye droo ya hela ila holaaa, nikaanza kuaminishwa nalogwa ila baada ya kautafiti kangu nikabaini mdogo wangu mtoto wa mama mdogo ndio alikua ananiibia maana dogo alianza kua mcharo anatoa miofa kama hana akili nzuri
Nikafumba macho nikamlaza kituo cha police kama siku mbili akaongea kila kitu, ashukuru Mungu mama yangu ni mama yake mkubwa ndio alimuombea msamaha la sivyo dogo ningemtia adabu police
Sometimes hakuna cha chuma ulete wala nini, uchawi ni wewe mwenyewe kutokua makini na biashara yako though sometimes uchawi upo