Wadau nisaidieni ushauri kimawazo kwenye jambo hili

felakuti

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
659
Reaction score
1,207
Hamjambo wana JamiiForums

Wakati mwingine unaweza kuwaza sana hadi kichwa kinataka kubasti, kuna kipindi kabla sijawa mtu mzima nilikua napishana na mtu anaongea mwenyewe na kurusha mikono hewani, nilikua najiuliza sana, ila badae sana nikapata majibu.

Wadau nina nyumba mbili katika kupiga kazi za hapa na pale nilizijenga, ila kwa sasa mambo yamekua magumu wakuu, niko benchi, mpaka najiuliza ni mimi tu au kila mahali, nyumba moja ndio naishi na familia, nyingine nilisema nipangishe, yapata miaka 5 sasa, ila wakuu embu niambieni sio biashara kichaa hii kweli, kodi 140,000/- mtu analipa miezi mitatu, hela yenyewe anatoa kwa mafungu, hivi wakuu kuna ku survive hapa kweli? Naona kama namfaidisha tu mpangaji na hainilipi kabisa bora hata labda angekua anatoa kodi ya mwaka mzima, kodi za mafungu, ila sio kwamba ana shida

Je wadau mnanishaurije, niuze nyumba hela nusu ya nitakayopata nianzishe biashara niendeleze gurudumu la maisha au mnasemaje wadau? Kichwa kinapata moto wakuu, muda unaenda, sioni nikisogea, au nichukue maamuzi haya kwenye thread inayofata

Nishaurini.
 
Hamjambo wana jf

Wakati mwingine unaweza kuwaza sana hadi kichwa kinataka kubasti, kuna kipindi kabla sijawa mtu mzima nilikua napishana na mtu anaongea mwenyewe na kurusha mikono hewani, nilikua najiuliza sana, ila badae sana nikapata majibu.

Wadau nina nyumba mbili katika kupiga kazi za hapa na pale nilizijenga, ila kwa sasa mambo yamekua magumu wakuu, niko benchi, mpaka najiuliza ni mimi tu au kila mahali, nyumba moja ndio naishi na familia, nyingine nilisema nipangishe, yapata miaka 5 sasa, ila wakuu embu niambieni sio biashara kichaa hii kweli, kodi 140,000/- mtu analipa miezi mitatu, hela yenyewe anatoa kwa mafungu, hivi wakuu kuna ku survive hapa kweli? Naona kama namfaidisha tu mpangaji na hainilipi kabisa bora hata labda angekua anatoa kodi ya mwaka mzima, kodi za mafungu, ila sio kwamba ana shida

Je wadau mnanishaurije, niuze nyumba hela nusu ya ntakayopata nianzishe biashara niendeleze gurudumu la maisha au mnasemaje wadau? Kichwa kinapata moto wakuu, muda unaenda, sioni nikisogea, au nichukue maamuzi haya kwenye thread inayofata

Nishaurini.
Usiuze. Wapangaji wamekuzoea hao! Wape miezi mitatu waondoke utafute Mpangaji mpya na uwe na Mkataba unaojieleza vizuri.
 
Biashara ya Nyumba kwa asilimia kubwa ni ya Washua Yan watu walostaafu wanasubiri kula penshen zao ila kwa vijana na wafanyakazi wa kazi na mishahara hii ya Samia hii biashara ni Headache Fikiria gharama ulizo invest kma ungeweka kwenye biashara kwa miaka yote Turnover yake ungekuta imeshakulipa kitambo cha msingi hapo usiuze hyo nyumba maana kuja kujenga tena nyingine so mchezo ukitegemea na gharama za maisha na ujenzi kupanda na hyo pia ukumbuke ni ASSET kwa ushauri kama una mkopo wa kazini chukua fanya biashara kwa moyo wako wote jitume tena kweli kweli shukuru Mungu as long as unakaa kwako
 
Amesema yupo bench mkuu ,kumanishaa Hana kazi ss atachukuwa wap mkopoo afanye hyo biashara..

Mtu chake mkuu km anaonaa akiuza akiwekeza Kwenye biashara itakayomlipa mbona fresh tu mkuu...
 
pangisha kwa Mkataba hii itakusaidia na utaona faida

Pia usiache nyumba ikawa na muonekano mmoja (KUDODA)ipe ukisasa ikarabati mara kwa mara kufanya ivutie ili hata ukimtajia mtu kodi na akiangalia muonekano wa nyumba na mazingira anaona ni sawa kutoa bila shida.
 
Usiuze. Wapangaji wamekuzoea hao! Wape miezi mitatu waondoke utafute Mpangaji mpya na uwe na Mkataba unaojieleza vizuri.
Kuna nyumba ya urithi naisimamia,nilipata wazo kama hili la kuwaondoa wote nianze upya na wengine,yaan wamenichosha nimeamua niwaache tu wakae

Nilkuwa nimepanga kila mpangaj anapotoka tusipangshe tena lakin naona niliemuweka anisaidie kuchukua kodi hatak kunielewa,akipata mtu anamuweka afu ndo wale wale
 
UZA..pakuishi si papo bwana,unateseeka wakati una asset ya kupata mtaji,usiwe kama wasukuma ng'ombe Mia hataki kuuza kisa prestige,nikukumbushe tu,usipouza wewe siku ukifa tu waliobaki wanauza
 
pangisha kwa Mkataba hii itakusaidia na utaona faida

Pia usiache nyumba ikawa na muonekano mmoja (KUDODA)ipe ukisasa ikarabati mara kwa mara kufanya ivutie ili hata ukimtajia mtu kodi na akiangalia muonekano wa nyumba na mazingira anaona ni sawa kutoa bila shida.
Mkuu mkataba upo, hua sipangishi bila mkataba sababu najua kadhia hizi za hawa wapangaji
Na pia mkuu.umeongea jambo zuri kuipa ukisasa, sasa kodi unayopata kwa mafungu hapo bado hujatoa hela ya chakula , mara hiki mara kile, unabakiwa na nini mkuu wangu? Hapo nazungumzia tuseme kodi kwa miez 3 ni karibia 420,000/-, hapo umepewa hela nusu, hadi akulipe nyingine mwezi umeisha, hapo uchukue mahitaj ya nyumbani na mengineyo, kwa maisha haya ya kitanzania, ni nini kinabaki hapo ? Na zaid nimepiga mahesabu, si chini ya milioni 3 inahitajika ya ukarabati
 
Weka picha na location huenda nikaipenda
Ina vyumba vingapi?
Kama ukiamua kuiuza na sio kwa dhihaka

Wapangaji njaa wakorofi sana ni kuwapa notice tu
Pangisha au uza utaangalia ipi inakufaa
Mkuu utaipenda kweli ? Mana wengi leo wanapenda nyumba yenye tailes, aluminium windows, mabati ya msauzi n.k, Nilijenga kwa tabu tabu si unajua tena kujitafuta ila inaishika, standard house, japo haina tiles, na madirisha ni ya kawaida sio aluminium windows, hati ninayo, sio kubwa kama mabangaloo, ina vyumba viwili vya kulala, seble, kisehem cha jiko ,bafu na choo,
Iko kwa mkoa wa paul makonda ..
 
Amesema yupo bench mkuu ,kumanishaa Hana kazi ss atachukuwa wap mkopoo afanye hyo biashara..

Mtu chake mkuu km anaonaa akiuza akiwekeza Kwenye biashara itakayomlipa mbona fresh tu mkuu...
Ndiyo maana nikasema hyo nyumba ni ASSET kuliko aiuze Bora aifanye kama Security ya kuchukulia mkopo lakini akiuza trust me kuja kupata nyingine au kujenga au Incase mtu akiumwa kama ni inahitajika Hela ya matibabu ataingia katika shida nzito Bora achukue mkopo kama mil 10 afanye analysis ya biashara hata mkoani ila sio kwa Dar akuze mtaji atafanikiwa tu Tambua kinachopatiakana kwa Nguvu na Juhudi hata Mungu hukibariki na kukizidisha
 
UZA..pakuishi si papo bwana,unateseeka wakati una asset ya kupata mtaji,usiwe kama wasukuma ng'ombe Mia hataki kuuza kisa prestige,nikukumbushe tu,usipouza wewe siku ukifa tu waliobaki wanauza
Tena wao wanaweza kuuza fasta sana [emoji23]
Ila haya maisha nyie acheni tu. Unajibana bana mwisho wa siku unaondoka duniani,wengine ni mwendo wa kufanya maamuzi tu waendelee kula.raha.
 
Back
Top Bottom