Wadau nisaidieni ushauri kimawazo kwenye jambo hili

Ndiyo maana nikasema hyo nyumba ni ASSET kuliko aiuze Bora aifanye kama Security ya kuchukulia mkopo lakini akiuza trust me kuja kupata nyingine au kujenga au Incase mtu akiumwa kama ni inahitajika Hela ya matibabu ataingia katika shida nzito Bora achukue mkopo kama mil 10 afanye analysis ya biashara hata mkoani ila sio kwa Dar akuze mtaji atafanikiwa tu Tambua kinachopatiakana kwa Nguvu na Juhudi hata Mungu hukibariki na kukizidisha
Mkuu naomba nishaur nichukue wapi mkopo wa milioni 10,
 
Mkuu nyumba ipo wapi hyo DALALI nipo hapa nikuletee mtejaa [emoji91]
Iko mkoa wa paul makonda mkuu..
Kama kweli mtu yupo siriaz ninamuachia kwakwel
Mimi naona naitaj hela nikapambane , siwez kusubiri laki nne na 20 kwa miez mitatu na itoke kws mafungu, hata hio hela ukitoa matumiz yote ya kifamilia , huwez hata kufungua genge kidogo
 
Mkuu naomba nishaur nichukue wapi mkopo wa milioni 10,
Kwanza kama nilivyokueleza fanya analysis vizuri kuhusu mkopo unaotaka uchukue pamoja na benki unayotaka kukopa pamoja na riba, Kwa hizi microfinance sikushauri kabisa hizi ni kausha damu haswaa pili usichukue mkopo mkubwa sababu ya Hyo Asset ulonayo kumbuka kuliko baadae ije ipotee ushindwe kuirudisha itakua ni hatari lakini pia fanya biashara hakikisha Kila siku ya Mungu usiache kutenga faida hata kama Tsh5000-10000 kuwa bahili Yani Discipline Yan assume hiyo biashara yako uko kwa mhindi anadai hesabu jioni Pia ishi kiuhalisia Yan hata kama ulikua graduants sijui una Ma CPA,ACCA,Masters tupa kule piga kazi Yan kama ukipewa hizo Hela kama unaendesha bajaji au Bolts yako weka akiba kumbuka hapo Pana Marejesho Kuna ada pia ikizidi usile bata Weka pia kwenye Account kama Saving sema hii ni ya Tahadhari
 
Iko mkoa wa paul makonda mkuu..
Kama kweli mtu yupo siriaz ninamuachia kwakwel
Mimi naona naitaj hela nikapambane , siwez kusubiri laki nne na 20 kwa miez mitatu na itoke kws mafungu, hata hio hela ukitoa matumiz yote ya kifamilia , huwez hata kufungua genge kidogo
Mkuu tena huo mkoa pia ni Rahisi sana kwako kuwa mbunifu na hyo nyumba yako unaweza ongea hata na hawa ma tour guide ukafanya renovation ikawa inachukukua wazungu yeye unampa ten percent yake cha msingi kuongea na watu vizuri ndani unapamba na Culture kibao za kimasai na tamaduni unaingia mtandaoni then unatangaza apartment for rent unajua wazungu hawapendi mavitu makubwa angalia Fursa hiyo nmekuachia
 
Kwanza kama nilivyokueleza fanya analysis vizuri kuhusu mkopo unaotaka uchukue pamoja na benki unayotaka kukopa pamoja na riba, Kwa hizi microfinance sikushauri kabisa hizi ni kausha damu haswaa pili usichukue mkopo mkubwa sababu ya Hyo Asset ulonayo kumbuka kuliko baadae ije ipotee ushindwe kuirudisha itakua ni hatari lakini pia fanya biashara hakikisha Kila siku ya Mungu usiache kutenga faida hata kama Tsh5000-10000 kuwa bahili Yani Discipline Yan assume hiyo biashara yako uko kwa mhindi anadai hesabu jioni Pia ishi kiuhalisia Yan hata kama ulikua graduants sijui una Ma CPA,ACCA,Masters tupa kule piga kazi Yan kama ukipewa hizo Hela kama unaendesha bajaji au Bolts yako weka akiba kumbuka hapo Pana Marejesho Kuna ada pia ikizidi usile bata Weka pia kwenye Account kama Saving sema hii ni ya Tahadhari
Sasa benki nilienda nikakwama. Unajua kwanini..wanataka biashara yani waone biashara duka lile.pale plus bank statement , tena biashara uwe umeifanya kwa angalau miaka kadhaa zaidi ya mitatu, na muda wote huo waone kwenye hizo bank statements pesa iliyokua inaingia na kutoka
 
Mkuu utaipenda kweli ? Mana wengi leo wanapenda nyumba yenye tailes, aluminium windows, mabati ya msauzi n.k, Nilijenga kwa tabu tabu si unajua tena kujitafuta ila inaishika, standard house, japo haina tiles, na madirisha ni ya kawaida sio aluminium windows, hati ninayo, sio kubwa kama mabangaloo, ina vyumba viwili vya kulala, seble, kisehem cha jiko ,bafu na choo,
Iko kwa mkoa wa paul makonda ..
Wala usihofu
Unajua nyumba sio madirisha na tiles tu bali location nzuri
Fikiria zile nyumba za kizamani Kariakoo watu waliuza kwa bei gani
Baada ya hapo mtu anashusha nyumba au ghorofa na kurudisha hela yake kwa miaka mitano tu

Ila nashukuru kwa kuweka wazi
Kama haotakupa hela nzuri kwa sasa wala usiiuze
 
Mkuu tena huo mkoa pia ni Rahisi sana kwako kuwa mbunifu na hyo nyumba yako unaweza ongea hata na hawa ma tour guide ukafanya renovation ikawa inachukukua wazungu yeye unampa ten percent yake cha msingi kuongea na watu vizuri ndani unapamba na Culture kibao za kimasai na tamaduni unaingia mtandaoni then unatangaza apartment for rent unajua wazungu hawapendi mavitu makubwa angalia Fursa hiyo nmekuachia
Naitaji renovation ya angalau milioni 5 minimum, naipata wapi, fikiria hapo wapangaji wamekaa sana na mna watoto humo ubadilishe choo, unaitaj kufanya renovation ya kueleweka, wazungu hawapendi sehem chafu
Tutoke hapo kwanza.
Kuongea na tour guide ni rahis mkuu kama hapo juu hio step umeshaiweza na kuifanikisha.
 
Tena wao wanaweza kuuza fasta sana [emoji23]
Ila haya maisha nyie acheni tu. Unajibana bana mwisho wa siku unaondoka duniani,wengine ni mwendo wa kufanya maamuzi tu waendelee kula.raha.
Yaani hadi nimemwambia hivyo nimekumbuka kuna mzee amefariki March ameachia watoto mashamba na viwanja,yaani watoto wanavyouza utasema walikuwa wanangoja mshua aende zake...dunia hii
 
Ndiyo maana nikasema hyo nyumba ni ASSET kuliko aiuze Bora aifanye kama Security ya kuchukulia mkopo lakini akiuza trust me kuja kupata nyingine au kujenga au Incase mtu akiumwa kama ni inahitajika Hela ya matibabu ataingia katika shida nzito Bora achukue mkopo kama mil 10 afanye analysis ya biashara hata mkoani ila sio kwa Dar akuze mtaji atafanikiwa tu Tambua kinachopatiakana kwa Nguvu na Juhudi hata Mungu hukibariki na kukizidisha
Brother, bank hawatoi mkopo kisa una nyumba tu,lazima uwe na biashara yenye thamani ya million 20 ili upewe hiyo million 10,na nyumba ndio inaweza tumika kama security,bank hawatoi pesa ya kuanzisha biashara bali kuendeleza biashara.
 
Yani kama ulikua pembeni yangu wakati naongea na ma-bank officers, yan maelezo hayo hayo,,, benki kwenye mkopo aise unakuta mtu anaomba milioni 5 tu ila faili lake ni kama anaomba milioni 100, madokument kibao
 
Kaka yangu,Nina experience nao hao wenye mashati ya blue na meupe,.watu wengi hudhani ukiwa na nyumba tu unakopesheka hapana,nyumba haitoi rejesho,wanataka waone rejesho linapatikanaje kwanza ndio watoe pesa,ndio maana wanakagua mauzo ya mwaka,wanataka bank statement ya mzunguko wa biashara,wanataka kujihakikishia hiyo biashara hapo ina zaidi ya mwaka yaani mambo ni mengi
 
Mkuu utaipenda kweli ? Mana wengi leo wanapenda nyumba yenye tailes, aluminium windows, mabati ya msauzi n.k, Nilijenga kwa tabu tabu si unajua tena kujitafuta ila inaishika, standard house, japo haina tiles, na madirisha ni ya kawaida sio aluminium windows, hati ninayo, sio kubwa kama mabangaloo, ina vyumba viwili vya kulala, seble, kisehem cha jiko ,bafu na choo,
Iko kwa mkoa wa paul makonda ..
Halafu ulitegemea kodi kubwa zaidi?
 
Mkuu tena huo mkoa pia ni Rahisi sana kwako kuwa mbunifu na hyo nyumba yako unaweza ongea hata na hawa ma tour guide ukafanya renovation ikawa inachukukua wazungu yeye unampa ten percent yake cha msingi kuongea na watu vizuri ndani unapamba na Culture kibao za kimasai na tamaduni unaingia mtandaoni then unatangaza apartment for rent unajua wazungu hawapendi mavitu makubwa angalia Fursa hiyo nmekuachia
Mara nyingi inategemea na eneo, sio mahali pote ni salama kwa wageni
 
Hii nayo ishu nyingine. Hadi mzungu akae kwako aise, anyway hizo huani mambo ya konekshen na matour guide, pia renovation ya uhakika sana.
 
Ndiyo hali ninayoipitia kwa sasa ila namshukuru Mungu nakaribia kuruka kiunzi maana namimi niliwaza kuuza au kuchukulia mkopo kajumba kangu ka 3 bed room

Nakushauri ukomae tu mkuu tafuta namna nyingine ondoa mawazo kuwa una nyumba halafu pambana kivingine huwezi kosa mwanya wa kutokea ninachoongea ni uhalisia hata sikupangi mkuu
 
Pamoja mkuu..
Ila ngumu sana mkuu, unajua kuandika rahisi sana ila ground level ni suala lingine kabisa...

Nb: ungeweza kuniambia umerukaje kiunzi kama yafaa kusema hapa..
 
Hamjambo wana JamiiForums

Wakati mwingine unaweza kuwaza sana hadi kichwa kinataka kubasti, kuna kipindi kabla sijawa mtu mzima nilikua napishana na mtu anaongea mwenyewe na kurusha mikono hewani, nilikua najiuliza sana, ila badae sana nikapata majibu.

Wadau nina nyumba mbili katika kupiga kazi za hapa na pale nilizijenga, ila kwa sasa mambo yamekua magumu wakuu, niko benchi, mpaka najiuliza ni mimi tu au kila mahali, nyumba moja ndio naishi na familia, nyingine nilisema nipangishe, yapata miaka 5 sasa, ila wakuu embu niambieni sio biashara kichaa hii kweli, kodi 140,000/- mtu analipa miezi mitatu, hela yenyewe anatoa kwa mafungu, hivi wakuu kuna ku survive hapa kweli? Naona kama namfaidisha tu mpangaji na hainilipi kabisa bora hata labda angekua anatoa kodi ya mwaka mzima, kodi za mafungu, ila sio kwamba ana shida

Je wadau mnanishaurije, niuze nyumba hela nusu ya nitakayopata nianzishe biashara niendeleze gurudumu la maisha au mnasemaje wadau? Kichwa kinapata moto wakuu, muda unaenda, sioni nikisogea, au nichukue maamuzi haya kwenye thread inayofata

Nishaurini.
"kuna kipindi kabla sijawa mtu mzima nilikua napishana na mtu anaongea mwenyewe na kurusha mikono hewani, nilikua najiuliza sana, ila badae sana nikapata majibu", na bado. Ila ujue tekinolojia imekua, kunavijisimu vidogo sana ambavyo humezwa kisha kukufanya mikono yako iwe huru, ukipigiwa unapokea na unaweza ukapiga na kuongea bila watu kuiona simu yako, wanaweza wakadhani umechanganyikiwa kumbe ni kibano cha maisha.
 
Pamoja mkuu..
Ila ngumu sana mkuu, unajua kuandika rahisi sana ila ground level ni suala lingine kabisa...

Nb: ungeweza kuniambia umerukaje kiunzi kama yafaa kusema hapa..
Ni ngumu kweli yaani ni msoto ila ukiamua unaweza

Iko hivi, mwanzoni mwa mwaka huu mwezi wa kwanza nilikuwa na mtaji mzuri wa kueleweka(wa biashara za kawaida sio izo za mamilion) sasa nikaona niboreshe nyumba huku nikiweka balance ya mtaji nikafanya ivo

Nilichokuja kuharibu akaja mtu anauza kiwanja location nzuri hapa dar kwa bei nafuu nikaingiwa na tamaa nikakinunua na kubakisha kamtaji kadogo nikiwa na pesa za watu(kuna watu wanawekaga pesa zao kwangu wananiamini) nikiwa na matumaini naweza pambana nikarudi kwenye reli kabla hawajazichukua

Aisee sijakaa hata mwezi jamaa wakaja kuchukua pesa zao kichwa kikaanza kuwaka moto hapohapo pango zote zimeisha muda wake kazini na home nanipokaa(nimepanga ile nyumba nimepangisha) nikalipa madeni yote nikabaki mtupu kazi nikiwa nimefunga

Hiyo ilikuwa mwezi wa 3 kufupisha story ni kuwa niliamua nikaushie mambo zote na kupunguza matumizi to the minimum nikaomba msaada wa pesa kwenye kikoba(anachezaga wife) kama 300k nikaanza nao hadi sasa nipo napambana kurudisha mtaji na bado natarajia hadi mwakani mwezi wa kwanza huenda ndio naweza kusimama kama mwanzo
 
Pole na hongera mkuu.
Ila naona kama tuna situation mbili tofauti kwa % fulani. Ila yote vyema kama umepata solution
 
Back
Top Bottom