Wadau tumvike Dully Sykes Mataji Haya

blogger

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
12,112
Reaction score
15,060
Taji la u-legendary, 'Hall of Fame' wa Bongo Flavour.

Kwanini?

1. Tumekua nae katika tasnia hii.

2. Hajawahi kukata tamaa kupigania tasnia ya Bongo Flavor.

3. Ameyahimili mabadiliko ya kisayansi na ki teknolojia bila kutetereka.

4. Anawaimbia wote, watoto, vijana, wazee.

5. Nyimbo zake ni za kudumu, kama mwazikuambuka, Nyambizi, Leah umekwenda, Skufahamu, Hi!, etc.

6. Hana kashfa wala skendo chafu mtaani.

7. Anawasaidia wasanii chipukizi bila kujali uwezo wao kifedha.

8. Ni Mwanajamii (Socially interactive). Hana majivuno na habagui watu. Focus yake ni Music.

9. Tumekuwa nae tangu mwaka 96, 97, 98 na bado anawakilisha To-date. Nakumbuka Nyambizi nilikuwa naimba nikiwa form two, sasa mtoto wangu anaimba 'Ntizame', Togola togola.

9. Hana tuzo nyingi, sijui kwanini lakini hilo pia halimkatishi tamaa.

10. Ni baba wa wake watatu na analea family zote kupitia Bongo Flavor.

Hitimisho:

Kwanini tusimvike taji hili la 'Hall of Fame', 'Bongo Flavor Legendary'?

Ujumbe huu uwafikie Kili Awards na All Media.

Nawasilisha.
 
.., yes yes yoh
.., kila mwita nau nao naoo kila mwiti nao nau nau...

Kuna ngoma yake hii imekaa ki mahadhi ya ragamafin. Aliifanya kwa P FUNK.
 
Jamaa alikuwa anatoa ngoma tamuu na kaanza kulijua game kitamboooo sana..kawapa watu wengi chanel za kufata na ushauriii....

Nyambiziiiii, ilikuw shidaaaa.

Ukija Bijuee.....hatari sana.

Ilaaa kaaanz kuimba malugha ya kuzimu sijui
 
.,, nashukuru nimeisearch hii ngoma kwa LIBRARY yangu nimeikuta, yaitwa HANDSOME...

ameongea humu ndani ni noumer. Nimeweka repeat.

Fagilia fagilia.,, biti ilismama haswaa
 
huyu ni legendary wa ukweli hakuna ubishi kabisa

Anastahili aisee,, ametoka mbali sanaa.. Na bado yupo.

Kipindi hicho cha handsome tigo ilikua yaitwa BUZZ if im not mistaken, kaitaja kwa wimbo huu wa handsom
 
.., yes yes yoh
.., kila mwita nau nao naoo kila mwiti nao nau nau...

Kuna ngoma yake hii imekaa ki mahadhi ya ragamafin. Aliifanya kwa P FUNK.

Kuna wakti bongo flvor ilikua tamu sana....
 
.,, nashukuru nimeisearch hii ngoma kwa LIBRARY yangu nimeikuta, yaitwa HANDSOME...

ameongea humu ndani ni noumer. Nimeweka repeat.

Fagilia fagilia.,, biti ilismama haswaa

Kuna wimbo wake mmoja 'ASHA MAPROMISE' ,, kuna story nzuri sana mule. Akijaribu wakanya vijana wanaopenda kula vya wanawake... Very good song
 
Jamaa ana consistence ya hali ya juu, wenzake alioanza nao wengi wamesahaulika but yeye bado yupo anakomaa na madogo. Sema watu hawamchukulii siriaz sana coz nyimbo zake nyingi zimekaa kitotototo
 
Jamaa ana consistence ya hali ya juu, wenzake alioanza nao wengi wamesahaulika but yeye bado yupo anakomaa na madogo. Sema watu hawamchukulii siriaz sana coz nyimbo zake nyingi zimekaa kitotototo

Mkubwa nyimbo za dully hazijakaa kitoto, huenda wewe ndo unamfaham leo. Si tulie toka nae kitambo tunamjua.

Anabadilika kufutana na upepo na soko. Ndo maana yupo mpaka sasa.
 
Handsome
nasifika kwa mapenzi na mademu kila kona wananiita
haaaaandsoooome!!!!
Nafananishwa na masta
wachimba chumvi wanashanga
duly mr.kiki!!
Tunakomesha wale mabishoo wanaojifanya wanaleta ushindani na ilala k/koo
nipo na nitazidi kuepo
labda maisha yawe mwisho ndipo mimi sitokuepo
 
Jamaa ana consistence ya hali ya juu, wenzake alioanza nao wengi wamesahaulika but yeye bado yupo anakomaa na madogo. Sema watu hawamchukulii siriaz sana coz nyimbo zake nyingi zimekaa kitotototo

Nakubaliana nawe kwenye consistence. Yuko very focused.
 
Anastahili aisee,, ametoka mbali sanaa.. Na bado yupo.

Kipindi hicho cha handsome tigo ilikua yaitwa BUZZ if im not mistaken, kaitaja kwa wimbo huu wa handsom

piga BUZZ NNE TANO SITA SITA ZERO ZERO UTANIPATAAA
NASIFIWA KWA MAPENZI NA MADEEEMU
KILA KONA MPAKA WANANIITA HAAANDSOME
NANINAVYOJISHEBEDUA KWA POOOZI MPAKA SASA WANANIITA
 
@geniveros,

Anastahili heshima.
 
@geniveros,

Dully katambaa na biti ya P mule balaa!..hii ilikua nyimbo ya kwanza ya dully kuipenda kabla ya Sikufahamu.
 
Wimbo kama ule tunauita 'CLASSIC'. Wakudumu maisha.

aliimba kiutu uzima sana pale kwenye SIKUFAHAMU inawezekana ndio nyimbo bora kwake kuliko zote. mara nyingi Dully anaangalia soko ila pale ali focus kwenye ujumbe
 
piga BUZZ NNE TANO SITA SITA ZERO ZERO UTANIPATAAA
NASIFIWA KWA MAPENZI NA MADEEEMU
KILA KONA MPAKA WANANIITA HAAANDSOME
NANINAVYOJISHEBEDUA KWA POOOZI MPAKA SASA WANANIITA

p funk kinywele ki moja, lili bau wau...
Hahahahaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…