Mnafiki Wa Kujitegemea
JF-Expert Member
- Dec 30, 2022
- 3,751
- 6,337
Kabla ya kufanyia kazi hayo mapendekezo yako,ACHANA NA HUYO ALIYEKUWA MKE WAKO.[6/17, 17:32] Steven Simon Lyimo: Najiuliza samahani naomba unisaidie:
Kuna mwanamke ambae nilioa nikaachana nae kurokana na tabia yake ya umalaya.
Mimi nimekuwa ktk malezi mazuri ya kidini, niliridhika kwa asilimia zote kwamba nimepata wangu kumbe niliingia ktk mwanamke ambae sijui kilimpata nini. Tumeishi miaka 9 lakini cha kushangaza amekuja kuondoka bila sababu maalum ya kueleweka, akaficha na sehemu alipofikia kwa miezi mitano nimekuja kujua alipo nikamkuta ana kitanda godoro, na vitu vingine anadai amenunua vya kwake na hakutoa maelezo ya kutosha kuhusu ununuzi huo.
Nilimwacha mpaka leo.
Shida sasa nampenda hadi jina lake.
Nimechoka kuvumilia nimebembeleza sana mpaka Sasa miezi sita ila haeleweki, mpaka simu kafunga hapatikani nahisi ana namba nyingine ambayo sina anatumia. Wazo nililonalo nitafute mwanamke kama yeye mwenye jina kama lake. Sasa
1.Je atakubali kulea watoto wangu wawili?
2.Je atakubali vipi kuolewa nami na mimi nilishawahi kuoa?
3. Je nitamsahau mkewangu ambae huwa namkumbuka kila siku na najitahidi kutompenda nashindwa?
4. Je akitaka kurudi mkewangu nitaweza kumkana na kumkataa?
5 Ni njia gani sahihi zaidi natakiwa niifanye ili nimwache kabisa bila kuumia kila siku?
Naomba msaada wako kwani sikuwa na tegemeo la kuwa na mwanamke wa namna hii mpaka natamani labda asingenizalia watoto pengine ingekuwa nafuu kwani sitaki hata kuja kuonana nae eti kwenye sherehe ya mwanetu, kikao au jambo lolote.
[6/17, 17:34] Steven Simon Lyimo: Pia nina upendo wa dhati sana kwa mwanamke nikimpenda mwanamke nampenda kweli
LEA WATOTO WAKO KTK HALI AMBAYO ITAWAFANYA WAWE NI IMANI KUBWA SANA NA WEWE,KUSIWEPO MAHANGAIKO HATA CHEMBE.
Baadae oa mke yeyote atakaye kufaa na umuambie kabisa ya kwamba una watoto kabla ya kumtia kibindoni.
Usionekane km una uhitaji wa lazima kwa mwanamke,akubali=akatae kwako safi tu.