Wadau wa forex pitieni hapa

Messier 31

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2017
Posts
459
Reaction score
1,117
Mimi ni mmoja kati ya wanaojifunza hii biashara ya fedha za kigeni,
Katika kusomasoma vitabu na kupata uelewa kidogo kuhusu forex nimekuwa na sintofahamu moja ambayo nadhani kwa wale ambao kwasasa wanatrade wanaweza kunisaidia

Nataka kujua kama mimi mtanzania ambaye natumia Tsh naweza kutrade pairs kama EUR/USD or USD/JPY na kupata faida maana katika elimu niliyopata kidogo naona kama hamna faida kutokana na kuwa rate ya changes ya pair moja ni sawa na rate ya changes kwa currencies zingine.

(Tuchukulie mfano rahisi)
Nimesema tena mfano rahisi maana wabongo nawajua kwa ku kosoa

EUR/USD=1
EUR/TZS=2000
USD/TZS=2000

mfano, usd ikashuka thamani na pair ikawa EUR/USD=2
kwa maana hiyo us dollar itashuka thamani kwa rate hiyo hiyo kwa pesa zingine, na dollar kwa Tanzania itakuwa hivi
USD/TZS=1000

Hapo ukiwa ume buy
EUR/USD=1 kwa dollar moja ambapo kwa wakati huo us dollar ni sawa tsh 2000
na biashara ikawa upande wako na pair kuwa EUR/USD=2 utakuwa na faida ya $1 ambapo kwa kuwa dollar imeshuka thamani kwa Euro na kushuka thamani kwa rate hiyohiyo kwa currencies zingine ikiwepo TZS na kuwa $1 ni sawa na 1000 hivyo hizo usd 2 ulizozipata ukizi exchange kwa hela ya tanzania ambapo pia dollar imeshuka thamani kwa tzs na kuwa USD/TZS=1000 utakuwa na 2000 ileile ambayo uliitumia kununua EUR 1.
Sasa hapa sijui faida ikowapi,
Naomba kwa wataalamu wa frx waniondoe huu utata.
 
iyo we unazungumzia hard exchange yani unaenda bureau hapo posta
hi unatumia platform visent vyako vina exchenjiwa kuwa dola au euro kulingana na broker wako anavyotaka then iyo ndo unatumia kununu na kuuzia sarafu zilizo sokoni
 
kuna vitu vinaitwa pips leverage iyo levarage isingekuwapo ungekua ili uweze kutrade lazima uwe na dola buku ila kwakua ipo we umediposit 10$ kule inaweza soma 100$,300,500$,hdai 1000$ kulingana na umetumia levr ya ngapi
 
sa kule tunatumia pips( msogeo uliopo kati ya bei moja na nyingine either kwa kupanda au kushuka kwa sarafu ) mfano 1$ - 1.5472euro hiyo ni asubuhi unakuja mchana 1$-5490 toa jibu unalopata hapo ndo msogeo uliokuwepo kwa kupanda yani imepanda pips kadhaa
 
sas izo pips ndo kipimo cha je unataka ela ngapi wew kama ulianalysis zitapatikana pips kadhaa so ndo kinakuja kitu LoT size,iyo bureau haipo ndo maana hamna maana ya kuexchange hardly so lot ndo inadetrmine we wataka kiasi ganii
 
lot inaanzia 0.01 hadi 4,000,000,000,000trillion $.huko nimekadiria tu coz ndo mzunguko wa siku wa soko uo kwa siku sasa we na kamtaji ka 10$ mwisho lot yako ni 0.09 tu kadri mtaji unavopanda nawe unaongezewa kiwango cha lot
 
lot inaanzia 0.01 hadi 4,000,000,000,000trillion $.huko nimekadiria tu coz ndo mzunguko wa siku wa soko uo kwa siku sasa we na kamtaji ka 10$ mwisho lot yako ni 0.09 tu kadri mtaji unavopanda nawe unaongezewa kiwango cha lot
Acha kupotosha watu Mkuu,ushauri Wangu jisajili hapo kwenye hiyo site ya pipsology alotoa link @mwal Rct ,jifunze taratibu.....
 
Ngoja niendelee na mafunzo kabla sijaingia kwenye biashara yenyewe
Ni muhimu sana kufanya hivyo, Fx inahitaji muda mwingi wa kujifunza, ili ukifika wakati basi uweze kufanyamaamuzi sahihi ya kuingia na kutoka sokoni.

Fx haihitaji haraka kabisa.

Wengi waliokuwa na haraka waliishia kupoteza fedha bila kuona mafanikio.

Kila lakheri.
 
New fellas back in town, Forex not for everyone, teh teh teh......
 
Mkuu forex ni kitu kingine kabisa unatumia knowledge ya bureau de change kwenye forex huku wahuni wanachezesha soko kwa kanuni zao faida na hasara wanawatengenezea wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…