Wadau wa Haki msiache machozi ya watu hawa yakaenda bure

Wadau wa Haki msiache machozi ya watu hawa yakaenda bure

TLS, LHRC , Vyama vya Siasa na wadau wote wa Haki Nchini.

Haya Machozi ya Hawa wazazi yasiende Bure .

Wakati tunapaza sauti zetu kuhusu yule Binti alobakwa, Tukumbuke hapa Kuna Kijana Mdogo ambaye Ameuliwa kama alivyouliwa yule Binti wa Chuo wakati wa maandamano.



View: https://youtu.be/oTXNjAP1CAU?si=ONrlrRVCRxZkRWJx

Hii nchi sasa imekumbwa na laana ,hizi dam ambazo zinamwagika bila hatia , zitatafuna watu mpaka watajua hawajui mda mwalim mzuri
 
Mimi mpaka sasa sijaelewa Ghasia za Lamadi zilisababishwa na nini?!
 
Mimi ndiyo maana sina rafiki polisi. Hao siyo watu hata kidogo.
 
Business as usual. It seems there is a systemic abuse of police power mkoa wa Simiyu.

Less than 2 weeks ago askari wa huo huo mkoa wa Simiyu, makao makuu yao Bariadi, waligeuza simple traffic offence - fender bender ya parking - kuwa kipigo kizito, wakanijeruhi, mixer kunikalia kooni nilipotaka kusimama ili tuendelee na mazungumzo. Mwishowe waliniweka ndani, na ilitumika backup ya mwenyeji wangu, mtu mzito hapo wilayani ili mimi kutoka.

Nakumbuka vizuri askari aliyekuwa mstari wa mbele kunipiga kesho yake aliniambia "yani wewe una bahati, sisi huwa tunapiga sana bro"

Nilieleza kituoni kwa mkubwa wao kuwa tukio zima limerekodiwa video na sauti kwenye dashcam za gari yangu, kama wakitaka tu open up evidence. Niliachiwa bila masharti, nikabaki na majeraha yangu. Jicho, mdomo, shingo, na visigino vya miguu yote miwili. Mguu wa kushoto ulipata 'pitting edema', and As I write this, bado unatoa usaha na damu kwa mbali.

Sishangai askari hao hao kumuua huyu kijana, kwani kwa maneno yao ni fahari wao kupiga watu pale wanapojiskia.

Twisting ya maneno niliyoishuhudia pale, sidhani kama nitakuja kuamini lolote askari wanalosema.
It might not make so much difference lakini inaweza kuwa muendelezo wa kufichua maovu ya Polisi hasa wa awamu hii, upload hizo footage za dashcam kwenye social media. Tag watu wenye influence and spread awareness ya Police brutality under Samia Suluhu's regime.
 
Maandamano ya amani yanaruhusiwa lakini maandamano yenye fujo kiasi cha kujaribu kwenda kuchoma kituo cha polisi hayo kisheria hayaruhusiwi maana unaweza kwenda kusababisha mauaji ya askari au watuhumiwa waliopo mahabusu ya polisi

Na ukumbuke kwa mujibu wa sheria CPA 21(2) cap 20 Revised edition 2022 polisi anaruhusiwa kutumia nguvu au hata kuuwa kabisa ikiwa ni kwaajili ya kuokoa maisha yake au maisha ya mtu mwingine.

Ndo maana hata kina mbowe kila wakiitisha maandamano huwa wanawaasa wananchi maandamano hayo yawe ya amani maana wanajua ikiwa hayatakua ya amani madhara yanaweza kutokea.
 
It might not make so much difference lakini inaweza kuwa muendelezo wa kufichua maovu ya Polisi hasa wa awamu hii, upload hizo footage za dashcam kwenye social media. Tag watu wenye influence and spread awareness ya Police brutality under Samia Suluhu's regime.
Hazitasaidia sana kwasababu zinahitaji uijue background story yote, ila zingethibitisha pale kituoni au mahakamani kwamba matumizi yao ya nguvu hayakuwa warranted na pia walipindisha story a.k.a kugeuza maneno.
 
Haya ni madhara ya kua na askari Dara la Saba , ambao kwao hutanguliza Nguvu .

Hivi Kesho la Polisi lilishindwa kutumia Mabomu ya machozi, au Risasi baridi ,au maji washawasha??.

Mpaka mfyatue Risasi??.

Inawezekana kabisa, Kukawa na mauaji Kadhaa yalotokea kwenye Sakata hil, na huyu Kijana ni Mmoja wao.
Watu watatu walikufa papo hapo
 

Attachments

  • IMG-20240820-WA0000.jpg
    IMG-20240820-WA0000.jpg
    291.1 KB · Views: 2
Ukiwa mtu wa kutumia nguvu bila akili, madhara yake ndio haya. Hawa jamaa zetu wamejaaliwa nguvu nyingi, amini akili hawana.
 
Moderators punguzeni ujuaji.
Kichwa Cha habari kilikua

"Katika Kumlinda DC, Polisi ya IGP Wambura na Rais Samia, Walifyatua Risasi na KUMUUA Kijana alopata DIV ONE form Six huko Lamadi"

Uchaguzi wa Kichwa hicho cha habari ni Kwa sababu ..

Kwanza , ni kweli Risasi zilifyatuliwa baada ya DC kuanza kuzomewa.

Pili, Ni Polisi wa IGP .

Tatu, Ni katika Serikali hii hii ya Samia, Ndio haya yote yanaendelea


Nne, Uchaguzi wa Maneno hayo ilikua ni kuwavutia wasomaji wengi zaidi.


Kubadili Kichwa Cha habari, ni kuingiliwa Uhuru wa kuongea na kuheshim mawazo yangu lkn pia kuharibu maana nzima ya Uzi Huu.


Tupunguze ujuaji , Acheni Samia asemwe ,asemwe na asemweke kwelikweli, yeye Si ni kiziwi??? Kama ni kiziwi, sisi Kila jambo baya hapa Tanzania tunaliunganisha na Yeye Kwa majina yake.
 
CCM CCM CCM ccm wacheni kunywa damu za watanganyika zitawatokea kwenye tundu lolote mtake musitake
 
Hakuna damu isiyo na hatia itaenda bure. Huyo DC wakati wa Mungu utamfikia pia yeye na walioshiriki kuyapoteza Maisha ya huyo kijana.

Kama damu ya Abeli ilivyomlilia Mungu ndivyo wakati huu damu ya huyo kijana inamlilia pia.

Sifa na utukufu kwake Mungu. Amina.
 
Back
Top Bottom