Wadau wa Haki msiache machozi ya watu hawa yakaenda bure

Hii nchi sasa imekumbwa na laana ,hizi dam ambazo zinamwagika bila hatia , zitatafuna watu mpaka watajua hawajui mda mwalim mzuri
 
Mimi mpaka sasa sijaelewa Ghasia za Lamadi zilisababishwa na nini?!
 
Mimi ndiyo maana sina rafiki polisi. Hao siyo watu hata kidogo.
 
It might not make so much difference lakini inaweza kuwa muendelezo wa kufichua maovu ya Polisi hasa wa awamu hii, upload hizo footage za dashcam kwenye social media. Tag watu wenye influence and spread awareness ya Police brutality under Samia Suluhu's regime.
 
Maandamano ya amani yanaruhusiwa lakini maandamano yenye fujo kiasi cha kujaribu kwenda kuchoma kituo cha polisi hayo kisheria hayaruhusiwi maana unaweza kwenda kusababisha mauaji ya askari au watuhumiwa waliopo mahabusu ya polisi

Na ukumbuke kwa mujibu wa sheria CPA 21(2) cap 20 Revised edition 2022 polisi anaruhusiwa kutumia nguvu au hata kuuwa kabisa ikiwa ni kwaajili ya kuokoa maisha yake au maisha ya mtu mwingine.

Ndo maana hata kina mbowe kila wakiitisha maandamano huwa wanawaasa wananchi maandamano hayo yawe ya amani maana wanajua ikiwa hayatakua ya amani madhara yanaweza kutokea.
 
Hazitasaidia sana kwasababu zinahitaji uijue background story yote, ila zingethibitisha pale kituoni au mahakamani kwamba matumizi yao ya nguvu hayakuwa warranted na pia walipindisha story a.k.a kugeuza maneno.
 
Watu watatu walikufa papo hapo
 
Ukiwa mtu wa kutumia nguvu bila akili, madhara yake ndio haya. Hawa jamaa zetu wamejaaliwa nguvu nyingi, amini akili hawana.
 
Moderators punguzeni ujuaji.
Kichwa Cha habari kilikua

"Katika Kumlinda DC, Polisi ya IGP Wambura na Rais Samia, Walifyatua Risasi na KUMUUA Kijana alopata DIV ONE form Six huko Lamadi"

Uchaguzi wa Kichwa hicho cha habari ni Kwa sababu ..

Kwanza , ni kweli Risasi zilifyatuliwa baada ya DC kuanza kuzomewa.

Pili, Ni Polisi wa IGP .

Tatu, Ni katika Serikali hii hii ya Samia, Ndio haya yote yanaendelea


Nne, Uchaguzi wa Maneno hayo ilikua ni kuwavutia wasomaji wengi zaidi.


Kubadili Kichwa Cha habari, ni kuingiliwa Uhuru wa kuongea na kuheshim mawazo yangu lkn pia kuharibu maana nzima ya Uzi Huu.


Tupunguze ujuaji , Acheni Samia asemwe ,asemwe na asemweke kwelikweli, yeye Si ni kiziwi??? Kama ni kiziwi, sisi Kila jambo baya hapa Tanzania tunaliunganisha na Yeye Kwa majina yake.
 
CCM CCM CCM ccm wacheni kunywa damu za watanganyika zitawatokea kwenye tundu lolote mtake musitake
 
Hakuna damu isiyo na hatia itaenda bure. Huyo DC wakati wa Mungu utamfikia pia yeye na walioshiriki kuyapoteza Maisha ya huyo kijana.

Kama damu ya Abeli ilivyomlilia Mungu ndivyo wakati huu damu ya huyo kijana inamlilia pia.

Sifa na utukufu kwake Mungu. Amina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…