WWE ni kampuni inayofanya mambo mengi, mojawapo ndo hili la mieleka.
Upande wa mieleka WWE kwa sasa ina brands tatu (Raw, Smack down na NXT). Kila brand ina makombe/mikanda yake ambayo yanatakiwa kuwepo yenye hadhi tofauti, (Hadhi ya dunia, kawaida, wanawake na team)
Upande wa RAW mkanda wenye hadhi ya dunia ni Universal championship, hadhi ya kawaida ni Intercontinental championship, ndo unakuwepo ule wa wanawake na tag team championship. Kwa sasa cruiser weight division imeunganishwa na raw hivyo kufanya idadi ya mikanda hapa kuwa mitano ukiwemo na cruiserweight championship.
Smack down mkanda wenye hadhi ya dunia ni WWE championship, hadhi ya kawaida ni united States championship na ule wa wanawake na tag team.
NXT ambayo ni kama kituo cha kuibua/kukuza vipaji cha WWE pia ina mikanda yake.
Hata hivyo, mfumo wa uendehaji wa hizi brands za WWE hubadilika mara kwa mara tangu kuanzishwa kwake. Huu mfumo uliopo umewekwa mwaka 2016. Mda wowote unaweza kuona mabadiliko.
Pamoja na hayo zipo kampuni nyingine za mieleka duniani ambazo hushindana na WWE, mfano TNA, World Pro wrestling, n.k