Wadau wa mchezo wa mieleka (wrestling)

Wadau wa mchezo wa mieleka (wrestling)

WWE ni kampuni inayofanya mambo mengi, mojawapo ndo hili la mieleka.

Upande wa mieleka WWE kwa sasa ina brands tatu (Raw, Smack down na NXT). Kila brand ina makombe/mikanda yake ambayo yanatakiwa kuwepo yenye hadhi tofauti, (Hadhi ya dunia, kawaida, wanawake na team)

Upande wa RAW mkanda wenye hadhi ya dunia ni Universal championship, hadhi ya kawaida ni Intercontinental championship, ndo unakuwepo ule wa wanawake na tag team championship. Kwa sasa cruiser weight division imeunganishwa na raw hivyo kufanya idadi ya mikanda hapa kuwa mitano ukiwemo na cruiserweight championship.

Smack down mkanda wenye hadhi ya dunia ni WWE championship, hadhi ya kawaida ni united States championship na ule wa wanawake na tag team.

NXT ambayo ni kama kituo cha kuibua/kukuza vipaji cha WWE pia ina mikanda yake.

Hata hivyo, mfumo wa uendehaji wa hizi brands za WWE hubadilika mara kwa mara tangu kuanzishwa kwake. Huu mfumo uliopo umewekwa mwaka 2016. Mda wowote unaweza kuona mabadiliko.

Pamoja na hayo zipo kampuni nyingine za mieleka duniani ambazo hushindana na WWE, mfano TNA, World Pro wrestling, n.k
Hiyo Worl Pro ndo siijuagi kabisa
 
Wayaa
Screenshot_20180427-235626.jpg
 
Daaah huyu jamaa alistahili mkanda huu aisee...

Yaani linarusha tuwatu utafikiri anarusha vipepeo...!! Nusu ya watu wote kawatoa yeye pamoja na kunachangiwa na washindani wake bado kashinda...bhaneeee kuna miwatu inamiguvu aiseee..!!

Kongole Strowman
 
Halafu wamepora ushindi wa Roman reign kwa sababu yeye ndiye miguu imeanza kugusa chini!....Sheria haisemi alieanza kutoka kwenye cage ndiye mshindi bali alieanza kugusa chini kwa miguu yake ndiye mshindi kama ilivyokuwa kwa Roman!....hata makomentetor wanasema kuwa huo ushindi wa the beast ni controversial!
Me shabiki wa Roman ila Lesner ndio katangulia
 
Bronstronman kashinda royal ramble ya watu 50 ila bhana daniel brayn ni noma, ameingia wa kwanza katoka baada ya lisaa lizima na dakika kadhaa ametoka wa 48
 
Halafu hizi sheria zikoje guys...

Mbona kunakipindi strowman alitoka... kapumzika hukooo.. karudi tena uwanjani inakuwaje hapo
 
Kwa hiyo lesnar kaenda na mkanda wake? Mana sijaelewa apa kea sababu walikuwa wanashindania Universal champ’ rematch sasa kama kachezea kwa roman si manake roman kashinda? Na anatakiwa awe WWE universal champ. Inakueaje tena mnasena lesnar kauza mechi! Tuambieni mliotazama mech jaman. Mi ni team Rains [emoji23][emoji23][emoji23] the Big dog
 
Kwa hiyo lesnar kaenda na mkanda wake? Mana sijaelewa apa kea sababu walikuwa wanashindania Universal champ’ rematch sasa kama kachezea kwa roman si manake roman kashinda? Na anatakiwa awe WWE universal champ. Inakueaje tena mnasena lesnar kauza mechi! Tuambieni mliotazama mech jaman. Mi ni team Rains [emoji23][emoji23][emoji23] the Big dog
Inshort lesnar kashinda according to refa but kiukwel roman kashinda ila marefa ndio waamuzi wa mwisho
 
Angalia haya youtube pia uone aseee..., Mbona mwingine ubishi..., Marefa sometimes mihemko nao inawasumbua..., Leo brock kachezea vitasa kinoma hahaha
Sheria inasema kuwa alietangulia kugusa aridhi kwa miguu yote miwili ndiye mshindi,Lesnar alitangulia ila akabakia kwenye ule wavu!!
 
Back
Top Bottom