Wadau waisihi serikali kuridhia itifaki ya haki za watu wenye ulemavu

Wadau waisihi serikali kuridhia itifaki ya haki za watu wenye ulemavu

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Katika juhudi za kukabiliana na mila potofu, imani zisizo sahihi na ushirikina unaodhuru watu wenye ulemavu, wadau wametoa wito kwa serikali kuhakikisha inakamilisha mchakato wa kuridhia Itifaki ya Haki za Watu Wenye Ulemavu Afrika kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la 12, ili kulinda haki za kundi hilo.

Itifaki hiyo ni sehemu ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, uliopitishwa Januari 2018 katika Mkutano wa 30 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika. Hadi sasa, Tanzania bado haijaridhia itifaki hiyo.
1742219845766.png


Akizungumza jijini Dodoma wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Sightsavers kwa waandishi wa habari na wadau wa haki za watu wenye ulemavu, Wakili Gideon Mandes, Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya watu wenye ulemavu, alieleza kuwa itifaki hiyo inatambua na kulinda haki za watu wenye ulemavu katika nyanja za elimu, ajira, afya, fursa za kiuchumi, na miundombinu inayofikika.
 
Back
Top Bottom