Wadau/wajasiliamali wa humu kuweni makini sana!

Wadau/wajasiliamali wa humu kuweni makini sana!

Pendo Julliet

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2017
Posts
243
Reaction score
324
Kutokana na umaskini imefikia hatua ukitaka Mtanzania akuskilize na kufata yako mueleze iko fursa ya kupata/kuvuna hela kwa mafankio makubwa sehemu fulani yani kwenye biashara nk.

Mueleze kile kizuri ambacho kitampendeza maskioni na kitaleta faraja kubwa ya maisha kwake naye bila kufikiri vizuri atafurahi na kukuona wewe ni nabii mpya na mkombozi kwake.

Mbinu hii hutumiwa na wengi wenye akili ili kufikia malengo yao kupitia Watanzania wanaohitaji relief kwenye maisha yao.

Hapa nawatahadharisha wadau watafutaji na wajasiliamali wote kuwa makini sana kabla ya kuitikia wito wa fursa zinazotangazwa na kupambwa kwa hadithi nzuri zenye kuvutia kama harufu ya maua mazuri kwa nyuki ukizingatia matukio ya kutekana, kupotea kwa watu nk yanayotokea kwenye jamii kila uchao.

Dunia imebadilika sana usipofikiri vizuri unaeza kujuta na wahenga wasema majuto ni mjukuu!

Hii ni tahadhari kabla ya hatari mwenye kuelewa na aelewe!
 
Upo sahii mkuu. Na sio JF tu... huvi karbuni nimeshriki seminar. Kilichoniacha mdomo wazi, ni wale waliokuwa wameandaliwa watoe ushuhunda wa mafanikio yao .. dahhha watu wanatririka vizuri sana... cha ajabu nilikuwa nawafahamu kiundani zaid. Mmoja ninaishi naye nyumba moja. Kila siku ni kukwaluzana na mwenye nyumba. Kashindwa kulipa ela ya pango. Mke wake anakosaga hata mia anakuja niomba mimi nimsaidie hata anunue mboga alishe familia.
 
Kuna nini jamani?! Nani kalizwa tena! Tuwekeni wazi jamani maana fursa za humu zinajulikana ati !!
 
reasoning vs emotion.
inabidi kipindi hiki reasoning iwe juu ya emotion.
maana propaganda nyingi za sasa za kijasiliamali na biashara zinasinyaisha kufikiri na kusisimua hisia ili mtu afikiri baada ya kutenda.
 
Kuna nini jamani?! Nani kalizwa tena! Tuwekeni wazi jamani maana fursa za humu zinajulikana ati !!
ni tahadhari tu kabla ya hatari mzingatie katika kuchangamkia hizo fursa zinazojulikana.
 
Hapana umetufananisha tu ndugu, mie nashughulika na kilimo na ufugaji huku kijijini.
Afuu wewe nimekuona hadi kule jukwaa la elimu unakipigia upatu chuo chako Dit.
uko kijiji gani mkulima mwenzangu Nije kukutembelea
 
Afuu wewe nimekuona hadi kule jukwaa la elimu unakipigia upatu chuo chako Dit.
uko kijiji gani mkulima mwenzangu Nije kukutembelea
emoji3.png
emoji3.png
kwani na wewe ni mkulima?
nikirudi kutoka shambani nafatilia masuala mbalimbali na muhimu yalojiri kwa siku hapo ndiyo nikapata kuifahamu DIT.
 
Back
Top Bottom