Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema Wadau wa elimu nchini wameshauri elimu ya msingi ianze darasa la kwanza hadi la sita na kuondolewa kwa mtihani wa mchujo wa kuendelea na elimu ya sekondari ili kuifanya elimu hiyo kuwa elimu msingi.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema kuwa serikali inatazamia kuzindua sera mpya ya elimu kufikia mwezi Desemba, 2022 ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu na kwamba mabadiliko yataanzia elimu ya msingi.
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye elimu ya msingi itakomea darasa la 6.

Kauli hiyo ameisema hii leo Oktoba 20, 2022, na kuongeza kwamba sera mpya ya elimu itakapozinduliwa hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni wa kidato cha nne tu, huku akisema mwanafunzi akianza kidato cha kwanza atakuwa tayari ameshajiweka kwenye mchepuo maalum hadi kidato cha nne.

Haya ndio maendeleo, ila tulipaswa tuwe kama US, 8-4-4

Primary miaka 4
Mtoto anaanza la kwanza akiwa na miaka 4 na kumaliza elementary akiwa 12 anakwenda sekondari at 13 years for 4 years na kumaliza at 16 anaingia college at 17 years for 4 years na degree zao ni masters!.

US mtu haruhusiwi kusomea sheria kama hana degree nyingine, hivyo kule kwenye sheria, sciences na udakitari wa binadamu, hakuna kilaza atapenya! Sio hapa vilaza wanakimbilia LL.B na kupewa degree za michongo!, kufika LST wana stopishwa basi ni kelele mwanzo mwisho!.

Kule hawana A level!.

P.
 
Haya ndio maendeleo, ila tulipaswa tuwe kama US, 8-4-4 .
P
What is the Advantage of this education system compared to the current one we have?

By the way:
Pascal Leo tuongee kirafiki maana huwa nakubomu Sana.
1. Unaonaje video clips za Ansbert Ngurumo, zinaonesha weledi wa uhandishi wa habari of the highest caliber ever au Ni sawa na makala zako?

2. Unampa credit gani kwa maswali yake magumu? (Maswali magumu)

Hapo nawaunga mkono, ila waongeze masomo Kama coding na vingine vinavyoendana na teknolojia ya Dunia ya Sasa bila kusahau kuongeza vitendea kazi sambamba na kuboresha miundombinu wezeshi kwa Shule zote nchini kwani ni rahisi na inawezekana.
Kama serikali wanakata tozo inashindwa nini?
 
Yaleyale ya physics with chemistry. Elimu ya watoto inageuzwa jambo la majaribio, mtoto wa kidato cha kwanza anaweza vipi kuchagua mchepuo maalamu?? Wakati hata uwezo wake kwenye masomo hayo haujui.

Soon watakuja na upuuzi wao wa kiswahili iwe lugha ya kufundishia.
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye elimu ya msingi itakomea darasa la 6.

Kauli hiyo ameisema hii leo Oktoba 20, 2022, na kuongeza kwamba sera mpya ya elimu itakapozinduliwa hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni wa kidato cha nne tu, huku akisema mwanafunzi akianza kidato cha kwanza atakuwa tayari ameshajiweka kwenye mchepuo maalum hadi kidato cha nne.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema kuwa serikali inatazamia kuzindua sera mpya ya elimu kufikia mwezi Desemba, 2022 ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu na kwamba mabadiliko yataanzia elimu ya msingi.
kwa hiyo watoto wetu watamaliza elimu ya msingi wakiwa na miaka 11. Maana wengi wanaanza la kwanza na 5 yrs.
 
What is the Advantage of this education system compared over the current one we have.

By the way:
Pascal Leo tuongee kirafiki maana huwa nakubomu Sana.
1. Unaonaje video clips za Ansbert Ngurumo, zinaonesha weledi wa uhandishi wa habari of the highest caliber ever au Ni sawa na makala zako?

2. Unampa credit gani kwa maswali yake magumu? (Maswali magumu)
Uhandishi
 
Yaleyale ya physics with chemistry. Elimu ya watoto inageuzwa jambo la majaribio, mtoto wa kidato cha kwanza anaweza vipi kuchagua mchepuo maalamu?? Wakati hata uwezo wake kwenye masomo hayo haujui.

Soon watakuja na upuuzi wao wa kiswahili iwe lugha ya kufundishia.
Wakiamua hivyo basi na watoto wao warudi shule za umma.
 
Nursery 4yrs,
Primary 6yrs
Secondary 4yrs
University 4yrs

Umri wa kuanza Nursery 6 yrs old
Watoto kuanzia anazaliwa hadi 6 yrs apate muda wa kukaa na wazazi kuna vitu anajufunza Kwa wazazi au walezi ni mihumu sana.
Kijana atoke shuleni na 24 Hadi 26 wasiwahi sana mtaani hakuna kazi hata hivyo watatoka wakiwa mabarubaru.
Kuanzia 21yrs ruksa kuoa/ kuolewa,kuzaa na kuanza kazi
 
Back
Top Bottom