Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Ni jambo jema.. Ila sio tiba. Mitaala pia ibadilishwe,.. Kuanzia elimu ya sekondari wangeiunganisha na vyuo vya VETA na Kilimo&ufugaji,.. Pia yafundishwe masomo ya entrepreneurship,.. Tutaweza kupunguza fikra tegemezi ya ajira kwa serikali...
 
ni jambo jema sana maana Elimu ya Msingi ili kuwa inatumia miaka mingi sana.

ila sasa inapaswa Wizara itoe maelekezo kwenye mambo yafuatayo;

1. Umri wa kuanza Darasa la 1 ufahamike.

2.
 
20 October 2022

MTAALA MPYA WA ELIMU, ELIMU YA MSINGI KUISHIA DARASA LA SITA



Mh. Omari Kipanga naibu waziri wa elimu afafanua kwa kina mkakati huo na michepuo zaidi ya kumi na nne.
Source : mlimani tv
 
Naomba Kujua,Sijaelewa,
Mtoto akishafika Darasa La 6 anakwendaje Form-1?
Sababu Nimesoma Kuwa Hakutakiwa na Mitihani Shule ya Msingi,Kutakuwa tuu na Mtihani wa form 4!
Sasa Mtoto akimaliza Darasa la 6 Watajiunga Vipi na Sekondary,Na Sekondary Maalum Pia?
Then Atafanya Mtihani form 4 na Kwenda Form 5!
Anaenda moja kwa moja kidato cha kwanza kama alivyoingia la sita akitoka la tano.
 
Vyuo vya Ufundi vinatakiwa kuwa na route ya kwenda University within 2 - 3 years.
Kwa UK, kwa mwanafubzi aliyepita vyuo vya ufundi, huwa wanakuwa wakali mno kwenye vitu kama CAD, Programming and Computing, na project zao za kumaliza chuo huwa zinakuwa za hali ya juu sana.
Vyuo vya ufundi hivi hivi vinavyofundisha vifaa vilivyobuniwa vita vya kwanza vya dunia ?

Tatizo la elimu ya Tanzania siyo miaka ya kukaa shuleni.


Ni kukosa relevancy katika ulimwengu wa sasa.

Watoto wanafundishwa TEHAMA kwa TV za vichogo ambazo hata madukani hazipo tena.
 
sasa kiongozi huo utaratibu wa kufundisha kwa lugha mbili tofauti huoni ni mkanganyiko ambao unachangia kuzorotesha elimu yetu
Naona lugha inatakiwa iwe moja tu kwenye kufundisha either eng au kiswa
hatuzolesh wala nn hapo kunakuw na balance na watoto wataelw wanachkisoma kiingerz liwe somo km somo lkn kiswahl kitmike kufnfishia masom km kemia , fizikia na jiografia
 
hatuzolesh wala nn hapo kunakuw na balance na watoto wataelw wanachkisoma kiingerz liwe somo km somo lkn kiswahl kitmike kufnfishia masom km kemia , fizikia na jiografia
Embu iweke archmedes principle kwa kiswahili
 
Uchunguzi unaonyesha kuwa wananchi wameunga mkono Hoja hii kwa asilimia 100
 
Human resources IPO!? Walimu mtatoa wapi!??
Hawa hawa waliopo,asilimia kubwa ya walimu wanaofundisha english medium ni wale walimu waliomaliza vyuo na bado hawajapata ajira.
 
Hili limefikia wapi? utekelezaji wake si ilitakiwa tuone mambo yanaanza mwaka 2023?
 
Hii inatakiwa waipeleke fasta fasta shule ya msingi darasa la 6 inatosha na sekondari form 4 itoshe chuo Cha diploma miaka 3 na degree miaka 3 jumla miaka 16 Hadi 18 tu ukiweka na miaka ya chekekea vijana waingie mtaani wakiwa na miaka 22 Hadi 24 waanze ujenzi wa taifa

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom