Wadau waulizia alipo Mwana CCM Thadei Ole Mushi

Wadau waulizia alipo Mwana CCM Thadei Ole Mushi

Post ya mwisho na HALALI ya Thadei Ole Mushi ni Ile ya tarehe 19th September (baada ya mtumiaji mpya wa account hii kuifuta post kuhusu timu ya simba).

Anayeiendesha account yake kwa sasa anajitahidi ila kuna makosa anayoyafanya (siyataji ataedit) ambayo wale wafuatiliaji wa karibu (wasio washabiki maandazi) wa kada huyu tunajua MWANDIKO na utaratibu wake SI HUU unaoendelea katika ukurasa wake. Mashabiki mbuzi ndio watakaoamini Thadei ndiye anaandika, kwa kuwa hawajui anaandikaje na jinsi anavyofikiri.

Lakini, hapa duniani unaweza kudanganya watu, ukageuza uongo kuwa ukweli kwa MUDA tu. Ipo siku ukweli utadhihirika.

Nadhani, kama mwenye account hawezi kuiaccess, anayefanya hivyo, hawezi kuuvaa uhalisia wa mtu mwingine. Bora kuiacha ikae bila kuandikwa chochote. Kuna vile Mungu katupa kila mtu upekee wake, na huo hakuna awezaye kuurekebisha.

Hata post hii kuhusu kurejea kwake ni kichekesho. Hii si akili ya Ole, Kuna vile anavyowasilisha mawazo yake, Kuna Aina za uchaguzi wa maneno, Kuna mpangilio nk... ni wazi kuwa huyu anayeitumia HAMJUI Ole Mushi kimaandishi, ametumia muda kupitia post zake za zamani akaigiliza ila nimwambie tu amefeli sana

NB uandishi ninaouzungumzia SI CONTENT ni PRESENTATION

Nakuombea kheri Ole.
Wako,
Bibi Happy Wa JosephView attachment 2783329

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah hakika ule mwandiko hakuwa wa Ole Mushi

Inafikirisha na rumours zilizopo. Mazingira yanaonyesha wamemuua
 
Kama hazina Kama hii itapotezwa kisa siasa basi tuna safari ndefu ya kwenda .

Malisa Gj na Thadei Mushi ni hazina Kwa Taifa Sana I Appreciate them .
 
Dah hakika ule mwandiko hakuwa wa Ole Mushi

Inafikirisha na rumours zilizopo. Mazingira yanaonyesha wamemuua
Ratiba ya mazishi ya ndugu @ole_mushi

Ibada ya kuaga mwili itafanyika kanisa la St.Peters Oysterbay leo saa 5 kamili asubuhi hadi saa 7 mchana.

Baada ya hapo mwili utapelekwa airport ukisindikizwa na ndugu wa karibu pamoja na mke wake.

Mwili utawasili KIA saa moja na nusu jioni na utapokelewa na wanafamilia waliopo Moshi na baadhi ya waliotoka Dar.

Mwili utaenda kulala nyumbani kwao Uru, Kitandu karibu na shule ya msingi Chombo Uru.

Kesho tar.7 January 2024 maziko yatafanyika hapohapo nyumbani kwao Uru Kitandu. Kwa watu wote wanaotoka DSM kama unahitaji kusafiri kwenda Moshi wasiliana na ndugu Deo Mushi⁩ kwa nambari 0719 780 033.
FB_IMG_1707204406800.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumemuaga ndugu yetu @ole_mushi hapa Muhimbili. Tunasafirisha msiba leo kwenda kumpumzisha kijijini kwao Uru, Kitandu. Tunamshukuru Mungu kwa maisha yake hapa duniani. Japo yalikua mafupi lakini yalikua ya msaada kwa wengi. Mungu ampumzishe kwa amani [emoji120]
FB_IMG_1707241604899.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kada wa chama cha mapinduzi Ole Mushi amejitokeza kwenye Ukurasa wake wa Facebook na Kukanusha kuhusu kulishwa Sumu

Hivi karibuni kuliibuka kumeibuka taharuki kuhusu alipo kada huyu baada ya kupotea kwenye mitandao ya kijamii muda mrefu ambapo wakati mwingine alikuwa mkosoaji wa baadhi ya Viongozi wa chama Chake, hata hivyo Jana iliibuka taarifa kuwa Ole Mushi alilishwa sumu na watu wasiojulikana.

Hata hivyo lao mapema Kada huyo aliibuka kwenye mtandao wa Facebook na mada ya kumpinga Martin Maranja kuhusu Kuongezeka kwa Deni la Taifa.

'' Ufafanuzi wa mimi kulishwa Sumu'

Naomba kuwapa taarifa kuwa jambo hili ni Uzushi usiokuwa na Maana lililoibuliwa na watu kwa nia wanazozijua wao wenyewe. Mimi nipo salama kabisa japokuwa nilikuwa nimepumzika kidogo kuandika kwenye Social Media.

Hata hivyo nawashukuru nyote kwa kuonyesha upendo wenu kwa kunitafuta hapa na pale pindi mlipoona nipo Kimya kwa Muda Mrefu. Kunitafuta kwenu bila kuchoka kumenionyesha pia thamani yangu katika kuwasiliana na ninyi kupitia Ukurasa huu. Niwape taarifa kuwa nimerudi na tutaendelea kusomana hapa katika majadiliano ya mambo mbalimbali yayohusu jamii yetu kwenye nyanja zote (Siasa, Uchumi, Michezo nk)

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Ole Mushi
0712702602
Kumbe walishikilia hadi account
 
Back
Top Bottom