Ex Mayor Jacob na MMM wameandika katika mtandao wa X (formerly Twitter).
huyu ni kada kindakinda wa CCM!
Wanawalaumu wana CCM kuhusika na hilo.
NI TETESI MAANA HAKUNA NEWS FROM CONFIRMED SOURCE
Kupitia ukurasa wa X, Boniface Jacob ameandika haya
-
CCM KWANINI MNATAKA KUMUUA THADEI OLE MUSHI......!
View attachment 2782152
Nimepokea kwa masikitiko na mshangao mkubwa sana taarifa ya shambulio la ghafla linaloaminiwa kuwa la "SUMU" dhidi ya mwana CCM machachari na mkosoaji wa Serikali ya CCM ndugu yetu Thadei Ole Mushi
Baada ya kupata taarifa za siri kuhusu kulishwa/kunyweshwa au kushambuliwa kwa sumu ndugu Thadei Ole Mushi
Mimi Boniface Jacob nimefanya jitihada za kumtafuta Thadei Ole Mushi na kuchunguza ukweli wa taarifa hizo
Nimejiridhisha kwamba Thadei Ole Mushi yuko katika hali mbaya inayoonekana siyo ya kawaida kwake
Yupo mkoani Dodoma (sehemu ni siri) akiwa na mke wake ambaye nimepatiwa namba yake na mtoa taarifa wangu.
Kinacho nisikitisha ni ndugu Thadei Ole Mushi kukosa msaada wa kuletwa hospitali kubwa kama Muhimbili jijini Dar es Salaam
Wakati nikiwa nimejiridhisha kuwa Thadei Ole Mushi hayupo katika hali ya kawaida, ndugu na watu wale wa karibu wa Thadei Ole Mushi wanaonekana kujitahidi kumficha na kuficha taarifa za ugonjwa wa Thadei Ole Mushi na wakati mwingine kuogopa kutoa taarifa za nini kimemkuta ndugu yetu.
Thadei Ole Mushi ni mwana CCM kindakindaki na mkosoaji mkubwa wa chama chake na serikali yake ya CCM, lakini haiondoi ukweli kuwa Thadei Ole Mushi ni mtu muhimu kwa CCM na siasa za Tanzania kama mchambuzi wa siasa nilifikiri CCM na Serikali yake ilitakiwa kutoa umuhimu mkubwa kwa Afya ya Thadei Ole Mushi hata kama hawakubaliani naye baadhi ya misimamo na mawazo yake.
Nikifikiri Jinsi Thadei Ole Mushi alivyokaribu na baadhi ya viongozi wa CCM na Serikali kama katibu Mkuu wa CCM Bw. Daniel Chongolo, wabunge kama akina Charles Kimei, wakuu wa Mikoa kama Anthony Mtaka, Mawaziri na manaibu kama Ridhiwani Kikwete bado nashangaa kwanini Thadei Ole Mushi atelekezwe wakati muhimu kama huu wa kupigania Afya yake.
Kwa namna ambavyo marafiki zake wa CCM na viongozi Serikali wanavyo muacha Thadei Ole Mushi kwa kumuacha apambane na hali yake ni dhahiri huenda wabaya wa Thadei Ole Mushi wapo CCM au kutoka ndani ya serikali ya CCM
Ni wakati sahihi sasa familia ya Thadei Ole Mushi itoke hadharani ituambie nini kimemkuta ndugu yetu katika siasa na mtanzania mwenzetu haraka na mapema tuweze kushiriki kunusuru uhai wake kabla hatujaijumuisha familia yake kama sehemu ya watu wabaya wa Thadei Ole Mushi.
Sisi Watanzania tupo tayari kumpambania na kumuokoa ndugu yetu Thadei Ole Mushi
Mtoeni mlipomficha, mpelekeni hospitali na kama gharama za matibabu ni kubwa tujulishwe tuweze kuchangia haraka sana.
Boniface Jacob