Wadau waulizia alipo Mwana CCM Thadei Ole Mushi

Wadau waulizia alipo Mwana CCM Thadei Ole Mushi

Post ya mwisho na HALALI ya Thadei Ole Mushi ni Ile ya tarehe 19th September (baada ya mtumiaji mpya wa account hii kuifuta post kuhusu timu ya simba).

Anayeiendesha account yake kwa sasa anajitahidi ila kuna makosa anayoyafanya (siyataji ataedit) ambayo wale wafuatiliaji wa karibu (wasio washabiki maandazi) wa kada huyu tunajua MWANDIKO na utaratibu wake SI HUU
Mkuu Mshana naomba hiyo post ya mwisho ya ndugu yetu Ole Mushi ya tarehe 19 September 2023.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
'' Ufafanuzi wa mimi kulishwa Sumu'

Naomba kuwapa taarifa kuwa jambo hili ni Uzushi usiokuwa na Maana lililoibuliwa na watu kwa nia wanazozijua wao wenyewe. Mimi nipo salama kabisa japokuwa nilikuwa nimepumzika kidogo kuandika kwenye Social Media.
Lakini Mwenyekiti wetu mstaafu alishaweka wazi kwamba hatuaminiani kabisa kiasi cha kutoachiana maji mezani
 
CCM KWANINI MNATAKA KUMUUA THADEI OLE MUSHI......!

Nimepokea kwa masikitiko na mshangao mkubwa sana taarifa ya shambulio la ghafla linaloaminiwa kuwa la "SUMU" dhidi ya mwana CCM machachari na mkosoaji wa Serikali ya CCM ndugu yetu Thadei Ole Mushi

Baada ya kupata taarifa za siri kuhusu kulishwa/kunyweshwa au kushambuliwa kwa sumu ndugu Thadei Ole Mushi

Mimi Boniface Jacob nimefanya jitihada za kumtafuta Thadei Ole Mushi na kuchunguza ukweli wa taarifa hizo

Nimejiridhisha kwamba Thadei Ole Mushi yuko katika hali mbaya inayoonekana siyo ya kawaida kwake

Yupo mkoani Dodoma (sehemu ni siri) akiwa na mke wake ambaye nimepatiwa namba yake na mtoa taarifa wangu.

Kinacho nisikitisha ni ndugu Thadei Ole Mushi kukosa msaada wa kuletwa hospitali kubwa kama Muhimbili jijini Dar es Salaam

Wakati nikiwa nimejiridhisha kuwa Thadei Ole Mushi hayupo katika hali ya kawaida, ndugu na watu wale wa karibu wa Thadei Ole Mushi wanaonekana kujitahidi kumficha na kuficha taarifa za ugonjwa wa Thadei Ole Mushi na wakati mwingine kuogopa kutoa taarifa za nini kimemkuta ndugu yetu.

Thadei Ole Mushi ni mwana CCM kindakindaki na mkosoaji mkubwa wa chama chake na serikali yake ya CCM, lakini haiondoi ukweli kuwa Thadei Ole Mushi ni mtu muhimu kwa CCM na siasa za Tanzania kama mchambuzi wa siasa nilifikiri CCM na Serikali yake ilitakiwa kutoa umuhimu mkubwa kwa Afya ya Thadei Ole Mushi hata kama hawakubaliani naye baadhi ya misimamo na mawazo yake.

Nikifikiri Jinsi Thadei Ole Mushi alivyokaribu na baadhi ya viongozi wa CCM na Serikali kama katibu Mkuu wa CCM Bw. Daniel Chongolo, wabunge kama akina Charles Kimei, wakuu wa Mikoa kama Anthony Mtaka, Mawaziri na manaibu kama Ridhiwani Kikwete bado nashangaa kwanini Thadei Ole Mushi atelekezwe wakati muhimu kama huu wa kupigania Afya yake.

Kwa namna ambavyo marafiki zake wa CCM na viongozi Serikali wanavyo muacha Thadei Ole Mushi kwa kumuacha apambane na hali yake ni dhahiri huenda wabaya wa Thadei Ole Mushi wapo CCM au kutoka ndani ya serikali ya CCM

Ni wakati sahihi sasa familia ya Thadei Ole Mushi itoke hadharani ituambie nini kimemkuta ndugu yetu katika siasa na mtanzania mwenzetu haraka na mapema tuweze kushiriki kunusuru uhai wake kabla hatujaijumuisha familia yake kama sehemu ya watu wabaya wa Thadei Ole Mushi.

Sisi Watanzania tupo tayari kumpambania na kumuokoa ndugu yetu Thadei Ole Mushi

Mtoeni mlipomficha, mpelekeni hospitali na kama gharama za matibabu ni kubwa tujulishwe tuweze kuchangia haraka sana.

Boniface Jacob
Mara ya mwisho alionekana kwenye ziara ya chongolo ….
 
Mwl.Ole Mushi-Afisa elimu hai na kada wa CCM ,Ni kweli alilishwa sumu

Alilazwa kcmc hospital ,na Sasa kahamishiwa dar,!

#CCM HOYEEEEEEEEEEEE
kama ni sumu basi itakua ni sumu ya panya, utitiri, viroboto, mende, kunguni....
 
Mwl.Ole Mushi-Afisa elimu hai na kada wa CCM ,Ni kweli alilishwa sumu

Alilazwa kcmc hospital ,na Sasa kahamishiwa dar,!

#CCM HOYEEEEEEEEEEEE
Waliosaidia taarifa zake kupatikana ni akina Bony Yai, Meya Mstaafu (CHADEMA). CCM walificha taarifa zake na Kwa tuhuma zilizopo ni kwamba "wanahusika"
 
Back
Top Bottom