Wadau wenzangu.. Hivi mnamuona kweli Ibrahim Ajib?

Wadau wenzangu.. Hivi mnamuona kweli Ibrahim Ajib?

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Narudia tena..
1. Hivi Wadau wa kandanda mnamuona kweli Ajibu?.
2. Hivi mna taarifa kua kwa sasa katika VPL hakuna deadly straika kama Ajibu?

Hebu imagine.. Kijana wa kitanzania [mwenye umri wa miaka 20 tu] anafanya haya katika ligi kuu ya Tanzania [miongoni mwa ligi ngumu ukanda kabisa huu wa CECAFA].

1. Katika misimu yake miwili tu katika VPL.. Ajibu ana hat-trick 2!!
2. Katika mechi 2 zilizopita za VPL.. Ajibu ana Goli 5!!
3. Katika mechi 3 zilizopita za VPL + 1 ya Kirafiki.. Ajibu ana goli 6!!
4. Leo kainyanyasa ipasavyo defence bora kabisa kwa sasa katika VPL.. inayoongozwa na beki bora kuwahi kushuhudiwa katika VPL.. Pascal Wawa!!

KWENU WADAU.
Tumekua tukilalamika Mara kibao kua hatuna "mtupiaji" katika Kikosi chetu cha Taifa.. Nadhani sasa upele umepata mkunaji, tena mkunaji haswaa.. Na mkunaji mwenyewe ni Ibrahim Ajibu.. Asante Mola kwa kutuletea huyu kijana katika wakati muafaka.

KWAKO Master MKWASA.
Najua ni kwa kiasi gani una kubali kipaji cha Ajibu.. na hii inajidhihirisha kwa kumjumuisha katika Kikosi chako kila Mara. Ila ni mda muafaka wa wa kumuamini zaidi na kumuweka moja kwa moja katika 1st eleven.

Ibrahim Ajibu ni kipaji adhimu kwa sasa katika ardhi yetu ya Tanzania.. Tunatakiwa Tukitunze na Tukilinde ili soon tuweze kujivunia kama tunavyofanya kwa Samata na Thomas.

Nakutakia mafanikio Mema, Ibrahim Ajibu a.k.a Mzee wa Ma Hat-Trick
 
Ni mchezaji mzuri wa kawaida sana kama alivyo John Bocco. Wote hawa walikuwepo kule Ethiopia hatukuona jipya sana zaudi ya kutolewa kizembe kabisa.

Afanye juhudi zaidi katika timu ya Taifa badala ya kusubiri na kukamia mechi za ligi.
 
Mbona ni mchezaji wa kawaida sana huyo...au unazi ndo umeweka mbele...hizo takwimu unazotoa ni za kijana wa miaka 16 au 17
 
Mbona ni mchezaji wa kawaida sana huyo...au unazi ndo umeweka mbele...hizo takwimu unazotoa ni za kijana wa miaka 16 au 17

Duh.. Hizi takwimu ni za mtoto wa miaka 16 au 17 kweli??!
Kwenye mazuri tusifie.. Weka unazi pembeni.
Hivi ni mchezaji gani katika VPL mwenye hizi takwimu?
 
huyu mchezaji kibongo bongo yupo juu tusemeni ukweli tu. ila tukitaka kumlinganisha na hao wengine wa 'majuu' tutakuwa hatumtendei haki hata sisi vilevile. Ndo wachezaji wetu hao tulionao tujivunie kwao
 
Mbona ni mchezaji wa kawaida sana huyo...au unazi ndo umeweka mbele...hizo takwimu unazotoa ni za kijana wa miaka 16 au 17

hebu tuonyeshe huyo kijana wa kibongo wa miaka 16 au 17 tumfahamu! tunaongelea wachezaji wetu wa kibongo sio wa mbele huko mkuu
 
hajibu bado mfungaji wa kawaida bado ajawa mfungaji hatari kuna vitu anatakiwa azingatie mazoezi ya kujenga mwili uwezi kushindana na mabeki wa kazi kazi kwa mwili ule kingine nasikia mvivu sana mazoezini
 
Ni mzuri ila umemsifia sana hadi umepitiliza kwenu
 
hajibu bado mfungaji wa kawaida bado ajawa mfungaji hatari kuna vitu anatakiwa azingatie mazoezi ya kujenga mwili uwezi kushindana na mabeki wa kazi kazi kwa mwili ule kingine nasikia mvivu sana mazoezini

Mkuu hizo zilikua ni story za msimu uliopita.. Hata Mimi nilizisikia sana.. Ila nadhani sasa kajitambua ndo maana sasa tumeanza kuona matokeo yake uwanjani.. Pia pongezi nyingi ziende kwa Dylan Kerr.
 
Back
Top Bottom