Wadhamini wa Tundu Lissu wawasilisha maombi ya kibali cha kumkamata

Wadhamini wa Tundu Lissu wawasilisha maombi ya kibali cha kumkamata

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiomba itoe kibali ili makamu mwenyekiti huyo wa CHADEMA kukamatwa.

Awali mahakama ilitaka kuwakamata wadhamini hao baada ya kushindwa kumpeleka waliyemdhamini mahakamani hapo.

Mmoja kati ya wadhamini wa Tundu Lissu, Robert Katula aliieleza Mahakama juhudi walizofanya kuhakikisha mshtakiwa anafika Mahakamani ni pamoja na kumwandikia barua Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Lissu anakabiliwa na Kesi ya Uchochezi yuko nchini Ubelgiji alikokwenda kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa Risasi Septemba 7, 2017 akiwa kwenye makazi yake Area D Jijini Dodoma akitoka kuhudhuria Vikao vya Bunge.

Pia soma

Wadhamini wa aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutaka itoe kibali ili makamu mwenyekiti huyo wa Chadema akamatwe.

Januari 30, 2020 Robert Katula ambaye ni mdhamini wa Lissu aliieleza mahakama hiyo kuwa juhudi walizofanya ni pamoja na kuwasiliana na mshtakiwa bila mafanikio pamoja na kumuandikia barua mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwasaidia ili Lissu arejee nchini.

Akizungumza leo Alhamisi Februari 20, 2020 wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Saimon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini wameshapokea nyaraka iliyowasilishwa mahakamani.

Katula amedai wamefanya jitihada za kumleta Lissu lakini imeshindikana na kuomba mahakama itoe kibali cha kukamatwa, “ tumefanya jitihada za kumleta lakini imeshindikana tunaiomba mahakama itoe kibali cha kukamatwa ili tuweze kuwa huru na kufanya shughuli zetu.”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWA UPANDE WA USALAMA, MAHAKAMA INAONA NI SAHIHI T LISU AKIRUDI TANZANIA WAKATI HUU ATAPONA??
Je waliotaka kumuuwa wameishakamatwa??
Je akirudi wakamuuwa, maana nia bado ipo, mahakama itaona ni sawa??
Kwa nini kama mahakama inafanya haki, isiisisisitize serikali ikakamata wauwaji wafikishwe mahakamni ili T Lisu arudi bila woga???
Au wanataka arudi ili wamkabidhi kwenye mikono ya wauwaji watimize malengo yao??
Sio busara kiusalama ulete mtu wauwaji wake wapo hapo hapo ili wamuuwe hadharani kama walivyo kusudia kufanya!!
MAHAKAMA PIA ITATHIMINI SWALA LA USALAMA WA LISU UKOJE??
 
Nafikiri Lissu anaweza kuomba mahakama itoe amri ya kupatiwa ulinzi na serikali, kisha nayeye ana wajibu wa kufika mahakamani baada ya kupewa ulinzi.

Ni mawazo tu ya bush lawyer hata sijui sheria inasemaje.
 
hao watu walimdhamini Tundu Lissu kwa nia njema ila kwa mazingira yalivyo wao ndio wanabanwa itafutwe namna ya busara kuwaondoa kwenye hili janga
 
Back
Top Bottom