Wadogo zangu, kabla TV hazijaja enzi hizo mgeni alikuwa anapewa album atazame picha za zamani. Yaani umpe Mtanzania album asichomoe picha hata moja?

Kipindi hiko sherehe ni sherehe kweli Christmas, iddy kubwa na ndogo sijui sabasaba na nanenane zilikuwa zinaheshimiwa sana na ilikuwa fahari kupika pilau siku ya nanenane au sabasaba.
 
They were so proud of their son.
Na haijalishi chuo upo certificate au dip au degree ukisema upo chuo ni heshima sana mtaani na wanachuo walikuwa ni watu wenye adabu kwelikweli kuanzia muonekana hadi kuongea smart kweli.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 mwaka huo nlikua mtu mzima, nakumbuka omar ali juma alifariki sjui alikuaga waziri a nn, nyerere anafariki mimi ndo nlikua nimetahiriwa
Mimi nyerere anafariki nipo la tatu.

Ilikuwa kama mwisho wa nchi vile maana kengere ya shule ilipigwaa wote tukusanyike kisha kwa masikitiko makubwa sana mkuu wa shule akaeleza sababu ya kuitwa pale yaani nchi imepoteza kiongozi mkuu then tuliruhusiwa kurudi nyumban hadi tutapotangaziwa tena kurejea shule.
 
Kuchomoa ukumbusho muhimu. Picha zangu nilizopiga masomoni Australia zote zilichomolewa
 
Na haijalishi chuo upo certificate au dip au degree ukisema upo chuo ni heshima sana mtaani na wanachuo walikuwa ni watu wenye adabu kwelikweli kuanzia muonekana hadi kuongea smart kweli.
Halafu picha yako utakayopiga siku unachukua degree yako au diploma yako inawekwa kwenye frame halafu inatundikwa ukutani sitting room.
 
We utakuwa wa miaka ya 1998, sqsa huyo Enrique Iglesias si wa juzi tu hapa miaka ya 2000s. Sisi tunamjua Baba yake, Julio Iglesias
 
Picha zinapigwa siku ya sikukuu tu...halafu kwenye maua au sebuleni kwenye makochi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…