Wadogo zangu, kabla TV hazijaja enzi hizo mgeni alikuwa anapewa album atazame picha za zamani. Yaani umpe Mtanzania album asichomoe picha hata moja?

Ulipotaja RTD, umeinikumbusha hadithi za shangazi Halima Kiemba, na Eda Sanga... hadithi ya ua jekundu
 
Hapo kwenye picha, utasikia hii siwezi kukupa kwa sababu nega yake haipo.

Na ilikuwa inachukiza kweli, umepiga picha leo unaipata baada ya mwezi, kila ukikutana na mpiga picha anakwambia mkanda haujajaa.

Mbaya zaidi siku unategemea kupata hizo picha unaambiwa mkanda umeungua na lilikuwa ni tukio la muhimu sana.

Yalikuwa maisha fulani hivi matamu na yenye uhalisia sana. Kwa kizazi hiki ni ngumu sana kuweka hizo kumbukumbu.
 
Dogo umeelewa vibaya. We utakuwa wa miaka 1998 kuzaliwa.
 
Sasa utamu na uharisia ni upi hapa hivi watanzania wanaweza sifia mambo ya uzamani
 
Ajabu akija kwenu kachomoa

Anaenda kwake anaiweka kwenye album yake

Siku ukienda kwake anakupa album yake uangalie ghafla unakuta ile picha ambayo huionagi nyumbani
Hahahahaaaaa mara nyingi ndio inavyokuwaga mkuu.
 
Watoto wa siku hizi hawajui that struggle ya kumpata mpiga picha


Aisee hadi leo nna album yangu ya picha za utotoni nimeihifadhi kwa kumbukumbu
Umenikumbusha jambo la muhimu sana mkuu. Ngoja na mimi nikusanye picha zangu zoooote za utotoni niziweke pahala pamoja.
 
Ukiachana na haya ya album, hivi hawa watoto waliozaliwa juzi juzi wanajua kwamba hawa tunaowaita Wapiga debe jina lilitokana na kitu flani cha pembe nne kinachioitwa debe? Waliwahi kuliona debe? Siku hizi yapo wapi madebe wahenga?
Nacho jua mimi madebe ni magari yote yanayouzwa chini ya Tshs milion 50, uongo Jamani

Natania
 
Woow..hii safi sana,niyakumbukayo;
1. Ndala za "Skyway"
2.Raba za "DH"
3.Suruali za "Tokyo & Beauct"
4.Mafuta ya kujipaka "Rays"
5.Tanbond sio blue band
6.Soda ya double cola na fahari.
7.Negro arushaa aliitwa " Masawee"
8.Peugeot 403 & 404[emoji3]
 
Hahahahaaaa hao ndio watanzania mkuu
 
Nimemiss nega za picha
Nimemiss kombolela na kidali poo.
Kujipikilisha michanga
Kuiba mchele kwa mpemba
Kujipikilisha kwenye vikopo vile vya bati (vya tomato sauce)

Ukipiga picha leo waipata baada ya siku 5 hadi week😂😂😂

Maisha ya zamani yalikuwa ya Raha sana
 
Nakumbuka mzee alikua na video tapes za enrique iglesias kulikua na videos kama bilamooooooos, sad eyes, maria maria za kina santana, kina britney spears
Mama yangu mdogo alienda kusoma Ulaya akaja na TV, deki pamoja na mikanda ya akina Michael Jackson pamoja na Lionel Richie.
 
Ila hata siku hizi zipo albums but zipo vizuri zaidi, ni picha zinapigwa halafu inakuwa kama kitabu iliyochapishwa, ikishachapishwa huwezi kuweka picha zingine hadi kitabu kingine.
 
Hakika ya kale ni dhahabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…