Wadogo zangu, kabla TV hazijaja enzi hizo mgeni alikuwa anapewa album atazame picha za zamani. Yaani umpe Mtanzania album asichomoe picha hata moja?

Sio kuchomoa tu mi shangazi yangu alichukua album nzima na kupotelea nayo kijijini kisa kulikuwa na picha yake moja tu mpaka leo inaniuma sana picha zangu nyingi za utotoni zilipotelea huko.
 
Kitambo sana mkuu. Nakumbuka enzi hizo kila Christmas tulikuwa tunapiga picha ya pamoja familia nzima kama ukumbusho
Unakuta mama ndio amekaa katikati akiwa amempakata mdogo wenu wa mwisho daaah zamani raha sana
 
Hahahaha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Umenikumbusha mbali sana
 
Picha zote zilikuwa zinaoshewa Dar, sasa enzi hizo tukajua zinaoshwa na maji ya bahari.

Mzee wangu alikuwa na player yake ya santuri ingawa haikukaa sana akanunua radio National Panasonic yenye casset,

Nakumbuka mzee alinunua tape ya mbilia bel ilikuwa na nyimbo Nadina, Mobali Nangai wana, Nakai Nairobi nk aliipenda sana kila jioni hasa jmosi na juma pili alikuwa anaipiga mpaka wazee wengine wa mtaani wanakuja home kusikiliza na story zao ni za wanamziki wa zamani nk.

Siku moja militumwa chumbani kwa mzee kuchukuwa sikumbuki, badala ya kufanya kilichonipeleka nikanza kuplay ile tape ya mbila bel ilikuwa kwenye radio nikabonya chakuplay na kurewind sijui ikawaje kamba ya tape ikanasa kutaka kutoa ikatika duh hiyo siku ilikuwa chungu sana, mzee aliporudi kutola job alinioa kichapo cha mbwa mwizi sitasahau.
 
Dah, zamani ilikuw raha sana aisee,

Hivi hzi mikanda bado wanasafishaga kwel?? mana kuna pic zangu za sekondari enz hzo humu
 
Watoto wa siku hizi hawajui that struggle ya kumpata mpiga picha.

Aisee hadi leo nna album yangu ya picha za utotoni nimeihifadhi kwa kumbukumbu.
Mimi sina picha hata moja ya utotoni, umenikumbisha kitu, ngoja nikirudi nikaibe moja kwa mama mzazi
 
So mkuu unataka kusema ccm ishu za kuweka mpira kwapani walijifunzia huko?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lol
 
Ya kale ni dhahabu, mwezi December nilienda kwa ndg. yangu kumsalimia, nikauliza habari za mtoto aliyekuwa amehitimu chuo mwaka jana, nikaletewa album ili niangalie mahafali yalivyofana.
Teknologia imeturahisishia maisha lakini tutauenzi ukale.
 
Sisi wa mikoani!Kama ulikuja Dar na haukupiga picha Daraja la Manzese Basi hata utembee uchi huwezi kuaminiwa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah nimecheka wallah mbavu sina mweeeh
 
Nakumbuka enzi hizo nikiwa darasa la tano (S/M), tulikuwa tunaenda shule na kidumu cha maji na mzigo fito, Nyazi za kujengea uzio wa Nyumba ya mwalimu Haya mambo siku hizi hayapo watoto wa 2003 hawawezi kuelewa kabisa [emoji3][emoji3][emoji3] Basi mkishasoma mpaka saa tisa na nusu unatoka na kidumu chako alfu na mzigo wako unaufuata ulipouweka asubuhi. Sasa hapo kwenye kuchukua mzigo ndio kuna mawili kuukuta au kukuta wamehamisha wahuni.
Daaah maisha ya shule yalikuwa raha tu. Ilikuwa mtu ukitoka hapo mnaenda kugaiwa vitengo vya kufanya kazi, wengine kujenga uzio wa mwalimu au Choo cha shule wakati mwingine hii ilitusaidia watu wengi kujua kufanya kazi za nyumbani ndogo kama kutengeneza uzio wa nyumba na bafu nyumbani.Ukiachana na Habari ya majukumu, ilikuwa ukimaliza kazi mapema unatelemka kwenda kucheza mpira wa mifuko na matambaa tulikuwa tunauita “Idaso” watu waliokulia Shy na Mwanza watakuwa wanaujua huu mpira na stori zake...


Ngoja nifanye moja nitarudi tena.....
 
Heheeee ...basi mme nikumbusha jambo,mwaka elfu 2005 nlipiga picha na Ray c akiwa na mwisho Mwampamba ,sasa ile picha niliweka kwenye albamu yangu, siku moja kademu flani katoto ka kota za tazara kakanitembelea ghetto bhana..acha kaibe😆😆ile naforce game mwe! Kumbe kameibana kwenye tight😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…