Wadogo zangu msisome Degree za Afya na Elimu

Wadogo zangu msisome Degree za Afya na Elimu

Hiyo kweli mkuu, nina mdogoangu nae ana degree ya ualimu kahangaika mwisho katulia na kasaluni kake kamtaani maisha yaende
 
Hi wakuu,

Mimi ni mwananchi wa kawaida nimejiajiri maisha yanaenda.
Nakuja na ushauri wenye ushaidi kuonyesha ya kwamba kusoma degree ya ualimu na afya Tanzania, ni kupoteza muda hasa wanaopenda kuajiriwa serikalini.

kwenye ajira za ualimu nina wadogo zangu. Wale wote waliosoma certificate in primary education wote wameajiriwa, Waliitimu (2016 and 2017 )

Dogo langu mmoja aliferi form six hakupata marks za kwenda chuo kikuu, alienda Monduli teachets collage na kisoma diploma in secondary aliitimu 2019, ameajiriwa na serikali.

Sasa kuna watoto wa ndugu zangu wamesoma degreee za ualimu wa sayansi, mmoja kamaliza 2016 na mwingine 2017, wote wapo kitaa wamepauka hawana ajira. Serikali haitaki kuajiri walimu wa science wa degree, wakati ndo walifahuru vizuri.

Sasa baada ya maisha kuwapiga wenye degree imebidi wadogo zao waliosoma certificate na kuajiriwa serikalini wachukue mkopo na kuwapa kaka zao ili wawe ata machinga.

Kwenye afya hivyo hivyo, serikali kama ni nursing inajaza wenye certificate na diploma, wa degree wanabaki kitaa na kipauka.

Wadogo zangu someni certificate na diploma za elimu na Afya kama unataka kupata haraka ajira za serikali.

NB: serikali ya CCM na Samia haitaki wataalamu wenye shahada.

Ukibisha njoo na data
Atakae kubishia, huyo atakuwa na sababu zake binafsi.
 
Kama Unaenda chuo kusoma kwa matakwa ya wanasiasa unabidi kujitafakari Sana.


Mimi mtoto wangu lazima asome degree ya Afya MD.
 
Back
Top Bottom