Wadogo zangu wa kike hata kama nyumbani kwenu maisha ni magumu usikubali ndoa ya sogea tukae

Kutambulishana ni sign ya wote kuwa mnajitambua na ndio namna kumuonyesha mwenza wako kuwa unampenda na kumthamini na upo proud kumtambulisha kwa watu wako wa muhimu kama wazazi.
Kutambulishana sio dalili ya kujielewa au kumuonyesha mwenza unampenda.
Upendo na mapenzi ya Watu wawili hayapimwi na external Factors ikiwemo hao wazazi. Mapenzi ya kweli na ishara ya Watu wanaopendana ni vile wanavyotendeana wema wao kwa wao.

Ndio maana haohao Wazazi unaosema Watu wanajitambulishe wanaweza kuzuia au kupinga binti asiolewe au kijana asimuoe huyo mwenza aliyemleta na zuio au pinga yao ikakataliwa na kupuuzwa na na hao vijana wao.


Huwezi ukavunja ndoa Mahakamani ambayo sio Rasmi. Ili ndoa ivunjwe mahakamani lazima iwe Rasmi
Ni kweli ndoa nyingi hazipo Rasmi yaani hazijasajiliwa Mahakamani hivyo ni kama hizo za sogea tuishi tuu kwa sababu muda wowote lolote laweza kutokea.


Ni kweli kwa umri huo vijana wengi ndio wamepata uhuru na wanaonja matunda ya kujitegemea hivyo wanapaparika na kukurupuka kuwa na wenza kwaajili ya starehe.

Narudia tena,
Asilimia 90% ya ndoa unazozijua zinaukatili, manyanyaso, uonevu, usaliti, ushenzi wengi wao wametambulishana kwa wazazi.

Na kwa bahati mbaya kabisa haohao Wazazi kwa sehemu wamekuwa na mchango katika mambo hayo Mabaya
 
Kumbuka huyo mtu unaishi naye upatapo dharula kama ya magonjwa ama ajali yeye ndio mtu wa kwanza atakayekuwa anawajibika moja kwa moja kwako.. je usipomtambulisha panapotokea sintofahamu kwa mwenza wako unawapa taarifa wazazi wake kama nani yake??

Ikumbukwe mnaishi pamoja mwanamke anaweza kupata ujauzito ukoo unaongezeka mtoto anapaswa kujua ndugu zake upande wa mama na ubabani ishu ya kutambulishana sio option ni lazima

Ndio yale baada ya kusolve tatizo lilopo mnaanza na utambulisho wakati iliwezekana kufahamiana kabla ya changomoto.
 
Ubarikiwe ndugu
kama anakupenda lazma atafika kwenu , mahari ni maonezi tu zitalipwa baadae, from there piteni kanisan fungeni ndoa hata ya watu sita maisha yaendelee....hizi mambo za njoo tuishi zinawaponza sana wadogo zetu
.,..From there piteni kanisani fungen ndoa hata watu sita maisha yaendelee....

Mkuu Ndoa ya hv bajeti inaweza kugharimu kiasi gani ?
 

Sijakupinga Mkuu.
Nilikuwa nakusahihisha kuwa utambulisho haya uhusiano na future ya ndoa.

Ila ni ku-connect past na present.
Utambulisho ni muhimu sana kwa heshima ya wazazi na kujuana basi.

Kutambulishana ni option Mkuu haiwezi kuwa lazima wakati tayari kuna Watu maelfu wanaishi na hawajatambulishana.

Pia kisheria za asili kutambulishana haipo hiyo kanuni.

Miaka mia ijayo hayo mambo hayatakuwepo kabisa.

Ukitaka binti au kijana mnakutana juu kwa juu na mnamalizana juu kwa juu kama mkipishanana.
 
Hapana kimsingi maisha ya sogea tukae yanakuwa yametawaliwa na hisia na motivation kubwa ni ngono na sio upendo wa kweli na case nyingi za sogea tukae zinwakuta vijana wadogo walioanza kujitegemea ni mara chache ndoa za namna hiyo kutoboa
Kweli kabisa
 
Kuna watu hapa mmetoa nondo zimesimamia kucha. Nimepata la kujifunza. Big up sana.
 
Mi siwezi na nashangaa sana watu wanaokaa na mtoto Wa mtu kwao awakujui akifa je
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…