Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kutambulishana sio dalili ya kujielewa au kumuonyesha mwenza unampenda.Kutambulishana ni sign ya wote kuwa mnajitambua na ndio namna kumuonyesha mwenza wako kuwa unampenda na kumthamini na upo proud kumtambulisha kwa watu wako wa muhimu kama wazazi.
Upendo na mapenzi ya Watu wawili hayapimwi na external Factors ikiwemo hao wazazi. Mapenzi ya kweli na ishara ya Watu wanaopendana ni vile wanavyotendeana wema wao kwa wao.
Ndio maana haohao Wazazi unaosema Watu wanajitambulishe wanaweza kuzuia au kupinga binti asiolewe au kijana asimuoe huyo mwenza aliyemleta na zuio au pinga yao ikakataliwa na kupuuzwa na na hao vijana wao.
Huwezi ukavunja ndoa Mahakamani ambayo sio Rasmi. Ili ndoa ivunjwe mahakamani lazima iwe RasmiNdoa zinazofika mahakamani kwa ajili ya talaka ni chache sana kulinganisha na wale wanaokubali yaishe kutumia kigezo cha takwimu za mahakamani sio sawa kwanza kibongo ndoa nyingi sio rasmi maana watu wanaishi kama mke na mume na hawana cheti cha ndoa.
Ni kweli ndoa nyingi hazipo Rasmi yaani hazijasajiliwa Mahakamani hivyo ni kama hizo za sogea tuishi tuu kwa sababu muda wowote lolote laweza kutokea.
Ndoa za sogea tukae mostly umri wa wahusika huwa ni chini ya 30 vijana ambao wameanza kupata pesa za kujikimu lakini wengi wanakuwa hawapo tayari na ndoa furaha yao ni uhakika wa kupata sex masaa 24 sasa majukumu yanapoongezeka na uchumi unapokuwa tight wanakuwa sio wepesi wakuvumilia.
Ni kweli kwa umri huo vijana wengi ndio wamepata uhuru na wanaonja matunda ya kujitegemea hivyo wanapaparika na kukurupuka kuwa na wenza kwaajili ya starehe.
Narudia tena,
Asilimia 90% ya ndoa unazozijua zinaukatili, manyanyaso, uonevu, usaliti, ushenzi wengi wao wametambulishana kwa wazazi.
Na kwa bahati mbaya kabisa haohao Wazazi kwa sehemu wamekuwa na mchango katika mambo hayo Mabaya