Wadogo zetu msidharau shule. Tunapowakazania msome ni kwamba huko angalau kuna uhakika, nje ya huko uhakika upo ila ni mdogo na wenye misukosuko

Wadogo zetu msidharau shule. Tunapowakazania msome ni kwamba huko angalau kuna uhakika, nje ya huko uhakika upo ila ni mdogo na wenye misukosuko

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin

Kuna kitu huwa kinaitwa probability, hii ni kipimo cha uwezekano wa kitu kuwa.

Nikija kwa mrengo wa maana yangu ni kwamba wapo wasanii waliofanikiwa, wapo wafanya biashara waliofanikiwa, wapo wanamichezo walioanikiwa, hao watu wapo lakini probability ya kuwezo kuingia katika hayo makundi ni ndogo mno.

Kuwa makundi hayo walau kwenye level zenye nafuu naweza kusema ni 1 pekee katika 100 ndio atafika huko, na kipimo ni mtu kuwa stable walau kwa miaka hata 10 tu, kuna wengine kwa miaka michache ni top ila upepo wa kisuli suli ukiwapitia kwisha.


Inapokuja suala la elimu ukiwa na degree yako haimaanishi kwamba lazima utapata ajira, wapo majobless wengi tu lakini huku kuna unafuu, uwezekano upo kwa probability yenye angalau hasa ukizinvgatia kuna taasisi, mashirika na vitengo kibao vyenye matawi karibu kila wilaya. Hali si poa lakini huku kuna nafuu.

Pia wanaoajiriwa kwa siku hizi huwa hawabweteki na kazi, wnapiga hybrid, wakishapata ajira mlango wa mshahara, posho na mkopo wa fasta unafunguka, hapa ndipo wenye akili wanapochomokea kwa kuanzisha biashara (mfano akiwemo vunja bei, Mengi, na hata yule mzee wa rich dad poor dad)
 
Back
Top Bottom