Ninayezungumza hapa pia ni kijana sio kwamba ni mtu mzima sanaa kivile, hapana. Naanza kwa kusema hili; ili kuondoa ile dhana ambayo kwa sasa inalalamikiwa na vijana wengi mitandaoni kwamba "Wazee" na "Watu wazima waliofanikiwa" wanawaonea vijana kwa kuwasema sema na kuwanyanyasa kama hivi post ambazo kwasasa zimetapakaa mitandaoni 👇👇👇
Na hata hapa jukwaani kuna kijana mmoja juzi kati kaleta hoja kwamba "Mabroo" wamekuwa wakiwasakama tu ila hawatoi michongo yoyote pindi wanapoombwa kufanya hivyo, uzi huu ulioletwa na member Natafuta Ajira 👇👇👇
Kumekua na kasumba ya mabroo ambao washatoboa kutushambulia wadogo zao ambao bado tunajitafuta bila kuangalia kwa upana utofauti wa mazingira ambayo wao walikutana nayo na sisi tumekutana nayo Mabroo ukweli ni kwamba wengi wenu mmeingia mtaani zama za kitonga (awamu za Mkapa na Kikwete), hamjua...
www.jamiiforums.com
Lakini kiukweli, vijana kwasasa wana tatizo la kujiamini kupitiliza kiasi kwamba tafsiri rahisi na ya haraka unayoweza kupata ni kwamba "Don't care". Sijui sababu ni nini hasa maana kunaweza kuwepo na zaid ya moja, mfano;
1. Kujikinai/kujikatia tamaa
Sababu ya kuleta hoja hii ni tukio nililokutana nalo ofisini kwangu juzi siku ya mechi ya Simba na Waarabu. Iko hivi;
Kwa mwezi mzima toka September kuna kijana wa chuo alikuja kuomba kufanya field, na baada ya kum-study nikagundua kuwa ni mtu ambaye alichelewa kuanza field na mpaka wakati huo hakuwa amepata.
Sababu ni nyingi lakini moja wapo ni ishu ya kipato mambo ya nauli alikuwa amelenga kupata hapa centre ambako atapanda gari 1 tu kwenda na kurud nyumbani kuepuka ghara nyingi za usafiri na hana mkopo shuleni, hivyo hana fungu la field toka bodi.
Nilimu-asses kwa namna nilivyotaka ili kujiridhisha kisha nikaona sio mbaya akatu-join afterall uhitaji wa mtu kama wake kwetu ungetupa manufaa katika namna fulani.
Basi bwana tukafanya kazi weee mpaka juzi kati ambapo akawa amemaliza field yake na vyuo vinafungua so anaenda kumaliza masomo yake.
So hii siku ya mwisho nikawa na mazungumzo nae kwa ajil ya tathimini mbali mbali kulingana na majukumu aliyokuwa nayo ofisini ili kupata feedback, lakini pia kuangalia namna gani ya kuingiza tathimini hizo katika Logbook yake ili ikasahihishwe na supervisor wake.
Sasa hii siku ndio ilikuwa inachezwa mechi ya Simba na Mwarabu, na mida kama hii ya 11 kwenda 12 ndio tulikuwa kwenye discussion. Sasa katikati ya mazungumzo, kwanza dogo full time kuchat chat.
Hii kitu nilishawahi kumuona nayo hata katika vikao vya kawaida vya ofisi na nikampa warning na kumfunza ni namna gani anapaswa kuwa ana-behave anapokuwa katika mazingira ya kikazi haswa kwenye vikao akiwa na sie seniours wake.
Sasa siku hii aliniacha hoi huyu bwana mdogo, ghafla katikati ya maongezi akainuka na kusema "Bosi, nafikiri hayo mengine nitatafuta muda mwingine tumalizie, mimi nataka niwahi kumuona Rais wa FIFA hapo Taifa maana muda umeenda sana na mechi itaanza sitaki kuikosa, unaonaje Boss?" 😂😂😂😂😂😂
Honestly, nilipigwa na butwaa sana kwa hizi guts alizonazo huyu dogo, nikamtazamaa kisha nikasema sawa haina shida, unaweza kwenda.
Alipotoka ofisini nilijikuta nacheka sana lakini hakikuwa kicheko cha furaha bali ni mshangao na huruma pia. Nikajiuliza hivi ni mimi tu ndio nilikuwa fala linapokuja suala la kazi au? Hivi huu ni ujasiri au recklesness?
I was about to let him know kwamba we would love him to join us us next year akimaliza chuo maana mapungufu yale madogo madogo ningejua namna ya kum-shape maana bado ana mindset ya kitoto kama mwanafunzi, ila kwa hiki kilichotokea nikashindwa hata kufika huko kote.
Sasa hapa vijana unawaza, unasema hivi wanataka nini tena?
Anyway ni hayo tu, na by the way sio vijana wote wako hiv!
Ipo kazi jamani, yaani serikali inahitaji mkakati wa malezi nyumbani na shuleni. Pasipo hivyo waajiri wataendelea kuwa kataa Hawa vijana wa kileo. Hali ni mbaya kuliko deni la taifa linavyokua, vijana hawaajiriki bse hawaaminiki, simu kwao ndio boss na wengine mtasubiri, masihara ndio usiombe yaani I kama serikali haitaweka mkakati wa malezi utegemee kuona mabaya zaidi
Mie mwenyewe ni kijana ila madogo ni miyeyusho sana.
Kuna kijana wa diploma kutoka chuo fulani alikuja kufanya field ofisi moja niliyokuwepo kwa wakati ule, katika kumpangia majukumu tulimpeleka mji wa jirani, tofauti na mji wao ( ambapo ofisi ilipo).
Alipokuwa huko tulikua tunamlipia lodge, chakula cha siku na pocket yake 15k. Kazi ilikua ya three weeks lakini baada ya siku 4, tukapata taarifa kaondoka tena kasema tu " mie nimechoka kukaa huku sipaelewi "
Aliporudi ofisini hakua na valid excuse, isipokuwa sababu za kitoto tu mara chakula kibaya, mara pocket yake ndogo e.t.c
Logbook yake hatukusaini ofisini, alisainia mitaani huko, bad enough ht supervisor wake hakufika ofisini aliishia kupiga simu tu kwa excuse ya ratiba.
Elimu imebadilika sana, sio kila mtu amesoma shule za kata, watanzania wamebadilika na pia uwezo wa kiuchumi umeongezeka, hivyo huwasomesha watoto wao shule zenye mitaala ya kuwa karibu zaidi na maendeleo ya mwanafunzi na kumjenga kujiamaini, sio kuchapwa na vitisho vinavyomfanya mtu kukua na nidhamu ya uoga.
Mabadiliko mengi ya leo ni social engineering zaidi...Na wengi wenu vijana sio kwamba mnajiaminnkwa maana ya kuwa na CONFIDENCE bali ni watu RECKLESS mliojizira HAMJALI na tena mmekosa SOCIAL ETHICS linapokuja suala la kazi. Jitazamen madogo.
Social Engineering ndio inayoendesha soko la leo, if you have to put things into scale, itaonenyesha ni jinsi gani dunia imebadilika haraka sana katika maendeleo ya kitechnologia ndani muongo mmoja kati ya 2010-2020.
Wenye mitazamo kama yenu wapo, lakini muda unavyozidi kwenda ndio mnazeeka na kupotea.
Na kama ungekuwa umewahi kuishi nje ya Tanzania, ungeona ile mitazamo ambayo tumekuzwa kufikiri kumkosoa mkubwa wako hata kama amekosea, ni kukosa adabu, ndio hapo mnakuwa na kuona vijana wa leo hawana social ethics.
Huu msimamo wawe nao hawa ambao boss akiwaongelesha wako radhi walale hapohapo ofisini wasiondoke?
Boss akiwa na mke mkorofi nyumbani aamue kujichelewesha alete story muda wa kazi umepitiliza basi mfanyakazi akae naye mpaka usiku. Mtu ashindwe kuwa na private life kisa boss atanuna. Eti ndio heshima na kunyenyekea kazi, huo ni utume au wito sio ajira.
Boss asiyejua kutofautisha muda binafsi na muda wa kazi wa mfanyakazi wake mnamuona yuko sawasawa. Kama kutofautisha muda huwezi, kuendeleza taasisi utawezaje. Muda ni rasilimali, hata nyinginezo kama fedha na watu utashindwa kutofautisha. Fedha za miradi utanywea pombe sababu huelewi, maisha binafsi na kazi unaona vyote sawa.
Elimu imebadilika sana, sio kila mtu amesoma shule za kata, watanzania wamebadilika na pia uwezo wa kiuchumi umeongezeka, hivyo huwasomesha watoto wao shule zenye mitaala ya kuwa karibu zaidi na maendeleo ya mwanafunzi na kumjenga kujiamaini, sio kuchapwa na vitisho vinavyomfanya mtu kukua na nidhamu ya uoga.
Social Engineering ndio inayoendesha soko la leo, if you have to put things into scale, itaonenyesha ni jinsi gani dunia imebadilika haraka sana katika maendeleo ya kitechnologia ndani muongo mmoja kati ya 2010-2020.
Wenye mitazamo kama yenu wapo, lakini muda unavyozidi kwenda ndio mnazeeka na kupotea.
Na kama ungekuwa umewahi kuishi nje ya Tanzania, ungeona ile mitazamo ambayo tumekuzwa kufikiri kumkosoa mkubwa wako hata kama amekosea, ni kukosa adabu, ndio hapo mnakuwa na kuona vijana wa leo hawana social ethics.
Inategemea na kama nimewahi kuishi au ninaishi nchi tofauti na wewe unapoishi kwa zaidi ya nusu ya umri wangu.
Kwa hiyo mitazamo yetu haiwezi kulingana na ibakie hivyo....
Boss wako anakufuga kwamba kila akitaka mazungumzo nawewe nje ya muda wa kazi ni lazima uache mambo yako umsikilize yeye?
Lolote analoongea ni lazima uwe interested nalo ukae mpaka akiamua uondoke?
inawezekana umezaliwa kwenye gud tym kweli ila wazee wako hawakua na mindset hii ndio maana akaweza fanikiwa.am not judging ila nahis wewe uko na shida.
Sitoki familia ya kipato cha juu. Ukiamua judging mbona hata mimi nimekuchukulia namna fulani.
Nakuona mwenye umwinyi nyinyi ndio baba zenu walikuwa wanakula mapaja ya kuku nyie mnapewa miguu hivyo una hiyo mentality kichwani kwamba ukiwa mkubwa unatakiwa usikilizwe kila kitu.
Uko arrogant, ukitaka kumsaidia mtu unampima kwa "ukondoo" wake na sio kwa uwezo wake wa kufanya kazi. Uchawa kwanza, utendaji baadae. Nyinyi kawaida yenu msiponyenyekewa mnajifanya basi hamtoi hizo ajira, wakati unakuta hujawahi toa hizo ajira hata kwa hao wanyonge.
Na watu kama nyinyi mnaongoza kwa sexual abuse kazini. Kumtaka mtu kimapenzi ndio umpe ajira mnafanya sana. Akikataa mnamuona jeuri na "hasaidiki".
Na vijana wanawajua, huwa wanajifanya kondoo kuliko kuwa competent kazini. Mtu genuine na mwenye uwezo anakuwa real siku zote. Maskini akipata matako hulia mbwata. Jipime unataka heshima au unataka performance.

Ukifanya utafiti kidogo unagundua sisi Kama Taifa ni lazima tufanye kitu juu ya hawa vijana. Hali ni mbaya fikiria hawa wachache hapa wanaowakilisha Wenzao majibu yao. Hili ni janga kubwa kuliko tunavyofikiria na wao wanajiona wako sahihi sana. With age comes wisdom and experience.
Boss wako anakufuga kwamba kila akitaka mazungumzo nawewe nje ya muda wa kazi ni lazima uache mambo yako umsikilize yeye?
Lolote analoongea ni lazima uwe interested nalo ukae mpaka akiamua uondoke?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.