Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Habari Wakuu wa JF,
Niende moja kwa moja kwenye mada. Hii itaweza kuwa msaada kwa ndugu zetu wanaopanga kuja likizo ya sikukuu za mwisho wa mwaka maeneo ya Arusha na Moshi.
Kuna mambo kadhaa ni muhimu kuweza kuyajua hasa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri (magari) na wale wanaopendelea kwenda maeneo ya starehe nyakati za usiku.
Umewahi kusikia kuhusu kundi la vijana wanaojiita WADUDU?, basi ndugu yangu hili ni kundi hatari zaidi la vijana wanaojihusisha na mambo mengi kwa ukanda wa kaskazini. Achana na wale unaowaona kwenye mitandao ya kijamii.wakiwa na viongozi wa kiserikali.
Wale naweza kukwambia kuwa wale sio WADUDU wenyewe.
Sasa ndugu yangu ukija ukanda huu wa kaskazini inakupasa kuishi kwa tahadhari sana hasa nyakati za jioni, usiku, asubuhi na nyakati zote uwapo barabarani.
Ngoja nikupe picha ya namna rahisi ya kuwatambua.hawa ni WADUDU.
Kwanza ukikutana na piki piki mara nyingi huwa kwenye makundi, mbili na zaidi zinakimbia sana inawasha taa ya spot mchana na wamepakizana vijana wawili au watatu. Jua hapa nimekutana na WADUDU kama unaweza wapishe wapite usitake kuweka nao mashindano, kuna hatari kubwa ya kuharibiwa gari lako na hutawakamata.
Kwa haraka mtu anaweza kusema labda mmewalea hao WADUDU. Ni kweli kuna.uzembe mkubwa umefanyika kuanzia jamii hadi vyombo vinavyolinda raia na mali zao.
Sasa kwanini nilisema uwapishe sababu kuna hatari ukaharibiwa gari lako na usalama wako kuwa mdogo sana.
Hawa viumbe kwanza wanakuwa wamelewa na sio ajabu ukawakuta wanatafuna mirungi na kuvuta bangi wazi wazi, wapo na sime au mapanga, rungu zile za kimasai, minyororo yenye kufuli au mipini ya jembe.
Sasa wanavyokuwa spidi njiani na wamewasha hizo taa wakihisi umewaziba ni ama wapige gari lako na hivyo walivyovibeba au wakuzibe njia na kukufanyia uhalifu wa ajabu hasa kwa usiku.
Bara bara za kuwa makini sana ni barabara ya Moshi Arusha naweza kusema hiyo bara bara hazipiti dakika 10 hawajapita WADUDU.
Tukiacha haya ya bara barani sasa tuangalie ya usiku.
Kwanza usiende sehemu ya starehe usiyoijua na ikitokea ukaenda basi hakikisha upo na mwenyeji au kama upo mwenyewe wahi kuondoka na ukiondoka ondoka kwa tahadhari sana.
Kamwe usipishane kauli na mtu maeneo ya starehe, kama utani unaweza ukapoteza uhai wako hivi hivi ukiona.
Kama itatokea umetoka sehemu ya starehe usiku ukahisi kuna piki piki zinakufuata basi jua upo mtegoni, ikitokea piki piki ikaja mbele yako kamwe usijaribu kusimama wala usisimame.
Ukiwa unajua unapoelekea hakuna watu basi usiende huko bali badili safari elekea ama kituo cha polisi au sehemu yenye watu maana hapo wanakutegea ufike unapoenda wafanye uhalifu wao.
Visa ni vingi sana hivyo ni muhimu ndugu zangu muwe na hiyo tahadhari.
Niwatakie maandalizi mema ya sikukuu za mwisho wa mwaka.