SoC04 Wadudu protein(Edble insects) wanaweza tusaidia kupunguza kiwango cha utapia mlo kwa Watoto Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Utapia mloa ni changamoto kubwa sana Tanzania, na utapia mloa ni ukosefu wa virutubiaho muhimu mwilini hasa sana Protein. Utapia Mlo ni ugonjwa wa Aibu kubwa sana hivyo ni lazima tuchukue hatua sasa.

MWaka 2023 Wakati Raisi Samia akizima Mwenge kule Babati Manyara alikili kwamba Pamoja na na jitihada kubwa za Serikali kupambana na utapia mlo Tanzania bado tatizo ni kubwa sana.

Mikoa yenye kiwango cha juu cha cha utapiamlo ni;
Iringa, Njombe, Rukwa, Geita, Ruvuma, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi, Manyara, Songwe na Mbeya.

KWa mujibu wa Twaweza Tanzania hupoteza Watoto 43,000 kila mwaka kutokana na utapia mlo.

Nini kinasababisha utapia mlo?

Sababu kubwa hapa ni moja tu Umasikini ambao hupelekea jamii kuto mudu kuwapatia watoto chakula Bora au Chakula chenye virutubisho hasa Protein na kujikuta watoto wanapewa chakula cha wanga wakati wote hivyo kudumaa na hata kupoteza maisha pia.

Wadudu Protein(Edble Insects) ni wapi?
Hawa ni wadudu ambao wanaweza kutupatia Protein na virutubisho vingine na ambao wanapatikana kwenye mazingira yetu.

Wadudu hao ni kama vile,Panzi,Senene,Crickets na Kumbikumbi.

Kumbikumbi; Picha kwa mujibu wa mtandao.

Senene; Chanzo cha picha ni Wikipedia.

Nini kifanyike?

Wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ihamasishe sana uvunaji wa hawa wadudu;
Wavunwe kwa wingi ili wasaidie katika swala zima la lishe. Hawa wadudu wapo mitaani wamejaa na sana wengi wanakuwepo wakati wa mvua nyingi.

Ni sehemu chache sana ambako hawa wadudu wanavunwa hasa Kanda ya Ziwa, Mikoa ya magharibi kama Kigoma.

Elimu ya matumizi ya hawa wadudu.
Bado pamoja na kwamba wanavunwa kwa kiwango kidogo sana, ila matumizi yake bado hayajajullikana sana, wengi huokota na kwenda kuuza au kula kama wanavyo kula Karanga,kumbe wanaweza vunwa wakakaushwa na kuchanganywa kwenye unga wa Ugari au Uji kwa ajili ya watoto

Unga wa Senene,Panzi,Kumbikumbi, na Criket unaweza changanywa pamoja na unga wa ngano kwa ajili kupikia Mandazi,Chapati,au unga wa mchele kwa ajili ya kupikia Vitumbua pia.

Unga wa Panzi: Picha kwa mujibu wa Mtandao.

Wadudu hawa wamekuwepo sana, kabla hata ya ujio vyakula vya kigeni amnavyo asilimia kubwa havima virutubisho na ni hatari sana.

Tuanze sasa kuangalia namna tunaweza punguza utapia mlo kwa kuwekeza sana kwenye wadudu hawa ambao kwanza ukiachana na Protein ila pia watatusaidia kuhifadhi mazingira.Hatutahitaji kufyeka mapori ili kulima Protein.

Wadudu hawa ni zawadi kutoka kwa Mungu tunaweza wapata Bure kabisa endapo tutahamasisha uvunaji wake.

Wadudu hawa ni salama, ni Chakula salama walicho kula Babu zetu kabla ya ujio wa Wakoloni.

Picha kwa mujibu wa mtandao.

Tukiamua tunaweza maliza utapia mloa kwa watoto kwa njia rahisi sana na rafiki kwa mazingira.
 

Attachments

  • Screenshot_20240519_134937_com.facebook.katana.jpg
    777.3 KB · Views: 4
Upvote 6
Naskia konokono ukimuwekea chumvi anayayeka, kwahyo mtamla bila chumvi?
Ana chumvichumvi kama ametiwa ndimu kwa mbali ila raha yake achemshwe au ukaange utamu mpaka kisogoni🤸
 
Hujanishawishi, dunia tunapita, acha tufe tu kuliko kuishi mda mrefu kwa kula konokono
Kuku wenyewe wa madawa, mleta uzi ana hoja huoni wachina wazee ni wengi sana wanaishi muda mrefu sababu ya kula protein nzuri konokono, panzi senene na nyoka
 

Kumbikumbi kuzalishwa inawezekana kabisa, nikuwatengenezea mazingiea tu basi. Ni vitu tunaweza fanya.
 
Mkuu, wadudu waliowao wana virutubisho sana,shida kubwa ni Mindset tulizo wekewa na watu wa Magharibi.
 
Kuku wenyewe wa madawa, mleta uzi ana hoja huoni wachina wazee ni wengi sana wanaishi muda mrefu sababu ya kula protein nzuri konokono, panzi senene na nyoka
Mkuu Asia wanakula sana wadudu, na sion Asia tu hata Wazungu wameshituka sasa wanakula sana wadudu. European Union imeisha ruhusu Wadud wauzwe.
 
Mkuu Asia wanakula sana wadudu, na sion Asia tu hata Wazungu wameshituka sasa wanakula sana wadudu. European Union imeisha ruhusu Wadud wauzwe.
Mkuu naweza kula wadudu ulioeataja kasoro konokono, nyoka etc
Nina kinyaa
Hiyo comment nilimpa mtu katika kutetea bandiko lako
 
Sasa nipige kura ya kula wadudu kweli? Ng'ombe, mbuzi, kuku, bata wamejaa, tuwaache hao tule wadudu kweli?
Mkuu, nazungumzia swala zima la kuoambana na utaoia mlo, yes nyama imejaa, ila nyama ni ghari sana, nyama mifugo inaharibu mazingira sana, nyama sio salama pia kwa sasa, Mifugo inapewa madawa sana hasa hizi antbiotic.
 
Haina shida ndugu tutakula tu hao wadudu wako.
Mkuu, nazungumzia swala zima la kuoambana na utaoia mlo, yes nyama imejaa, ila nyama ni ghari sana, nyama mifugo inaharibu mazingira sana, nyama sio salama pia kwa sasa, Mifugo inapewa madawa sana hasa hizi antbiotic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…