Wadudu wa Arusha ni janga jipya la kimaadili nchini. Acheni kuhalalisha uwepo wao

Wadudu wa Arusha ni janga jipya la kimaadili nchini. Acheni kuhalalisha uwepo wao

Zamani ilikuwa inajulikana kuna vijana wa hovyo walikuwa wakijiita wadudu wa dampo jijini Arusha ambao hasahasa walikuwa wakijihusisha na muziki wa Hiphop. Na hata wengi wao walikuwa wakivuka adolescence hubadilika na kuwa na tabia za kiutu uzima ikiwamo kuacha kujiita mdudu wa dampo. Hawakuwa na impact kubwa sana. Lakini miaka ya hivi karibuni ndo upuuzi ukaongezeka kiasi kwamba hata baadhi ya mijitu mizima inajiita WADUDU.

Kichaa anachekesha kama sio ndugu yako. Hata wadudu wanachekesha sana kama hakuna ndugu yako kwenye lile kundi la wadudu. Vijana wanajiharibu kwa kuongea, kuvaa, kutembea na mambo mengine ya hovyo ili kujipatia sifa kuwa yeye ni MDUDU WA CHUGA. Kwa sasa hizo tabia zimeenea kuanzia Arusha mjini, Monduli, Boma, Moshi, Babati, Mto wa Mbu hadi Karatu. Sio Arusha jiji peke yake. Maadili yanazidi kuvurugika.

Viongozi mnaowapa uhalali hao vijana wadogo kuwa na tabia za kishenzi hamtendi haki. Mtafurahi kuona watoto wenu nao ni WADUDU? Wewe RC utajisikiaje kumuona Keagan kwenye kundi la wadudu? Mwenyekiti wa UVCCM Arusha ni mtoto wa Meya wa jiji. Kwanini naye asiwe mwenyekiti wa wadudu kama ingekuwa ni jambo jema?
Umenena vema
 
Hivi wadudu wa Arusha na chawa wa mama/ccm wapi ni washenzi.?
hamuoni chawa ni janga kuliko hao wasanii /wadudu
 
Kuna watu wazima wana nafasi za utumishi katika jamii wanajiita chawa wa mama wale huwashangai unahangaika na wadudu wa Arusha? Chawa sio wadudu?
 
Back
Top Bottom