Waendesha mashtaka mnapaswa kushikamana na haki, usibadili msimamo hata kama watu wengi wanakupinga

Waendesha mashtaka mnapaswa kushikamana na haki, usibadili msimamo hata kama watu wengi wanakupinga

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
Shikamana imara na msimamo na usibadilishe msimamo kwa kuwa watu wengi wanakushambulia, au wanakasirishwa na maneno yako.

Maadam uko kwenye Haki, basi shikamana nayo na kuwa na msimamo, kwani Haki haishindwi (Na Baatwil).

Kwa hiyo, pigania (Haki) hata katika hali ya udhaifu (uko peke yako).

Hakuna zaidi ya kutetea Haki.
Lakini ukiwa katika hali ya uimara, basi usiache kuipiga vita (Baatwil).

Kwa kuwa siku zinabadilika (kuna wakati siku zinakuwa upande wako, na kuna zenye kuwa kinyume nawe).

Lakini kumbuka kitu muhimu hata pale katika wakati mgumu na udhaifu, usiyumbe wala kutetereka na shikamana na Haki. Na daima usiseme: ‘Ah, watu wote wanapingana na hili (ninalolisimamia). Bali, kuwa na msimamo.

Kutetea haki kuna gharama zake ikiwemo kususwa, kutengwa, kufungwa, kuadhibiwa, kudhalilishwa na kuuwawa. Lakini jambo jema ni kwamba Historia yako haitafutika, jina lako litaendelea kubakia.

Pigania haki popote ulipo na wala usiikwepe haki na ukatetea dhulma.

BAKIIF ISLAMIC
+255755351262


1666013607458.png
 
Back
Top Bottom