Wafadhili Kutoka Uswisi Wachimba Visima vya Maji 4 Jimbo la Ulanga, Morogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAFADHILI KUTOKA USWISI WACHIMBA VISIMA VYA MAJI 4 JIMBO LA ULANGA, MOROGORO

Wakazi wa wilaya ya Ulanga wamepata visima vya maji vinne kutoka kwa wafadhili kutoka nchini Uswisi ambao wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka. Mwakilishi wa wafadhili hao Bi Rubab Jawad Aziz amesema hatua hiyo imekuja baada ya kuona Changamoto ya maji imekuwa kubwa katika wilaya hiyo licha ya Serikali kupambana kuitatua mara zote.

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Ulanga wamesema wanayofuraha kuona wadau wanajitokeza kuwasaidia kwani ni kweli wanapata adha kubwa ya maji hususani kipindi cha kiangazi licha ya kuwepo na miundombinu ya maji lakini haitoi maji kabisa.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo la Ulanga Mhe SALIM Alaudin Hasham amesema Changamoto ya maji katika jimbo hilo ni kubwa hivyo hawezi kuiachia Serikali pekee bali ataendelea kutafuta wadau wengi kwa lengo la kuhakikisha Changamoto hio inapungua kama sio kuisha kabisa.

Visima hivyo vinne vimechimbwa katika kata tatu ambazo ni EUGA, Chilombora, Uponera na Kichangani na tayari vinaendelea kutoa huduma za maji. Wilaya ya Ulanga ina wananchi zaidi ya laki mbili (200000) ambao wanahitaji maji kiasi cha lita 1,600,000 lakini kwasasa wanapata lita 9000 pekee ambazo hazitoshelezi mahitaji yao.
 
Attachments

  • IMG-20230630-WA0028.jpg
    IMG-20230630-WA0028.jpg
    119.8 KB · Views: 7
  • IMG-20230630-WA0027-768x512.jpg
    IMG-20230630-WA0027-768x512.jpg
    86.7 KB · Views: 7
  • IMG-20230630-WA0024.jpg
    IMG-20230630-WA0024.jpg
    138.5 KB · Views: 7
  • IMG-20230630-WA0025.jpg
    IMG-20230630-WA0025.jpg
    103.7 KB · Views: 7
  • IMG-20230630-WA0020.jpg
    IMG-20230630-WA0020.jpg
    124.9 KB · Views: 6
  • IMG-20230630-WA0022.jpg
    IMG-20230630-WA0022.jpg
    119.7 KB · Views: 7
  • IMG-20230630-WA0011.jpg
    IMG-20230630-WA0011.jpg
    127.7 KB · Views: 6
leo wafadhili, kesho mabeberu, keshokutwa wahisani, siku inayofuata wakoloni..
 
WAFADHILI KUTOKA USWISI WACHIMBA VISIMA VYA MAJI 4 JIMBO LA ULANGA, MOROGORO

Wakazi wa wilaya ya Ulanga wamepata visima vya maji vinne kutoka kwa wafadhili kutoka nchini Uswisi ambao wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka. Mwakilishi wa wafadhili hao Bi Rubab Jawad Aziz amesema hatua hiyo imekuja baada ya kuona Changamoto ya maji imekuwa kubwa katika wilaya hiyo licha ya Serikali kupambana kuitatua mara zote.

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Ulanga wamesema wanayofuraha kuona wadau wanajitokeza kuwasaidia kwani ni kweli wanapata adha kubwa ya maji hususani kipindi cha kiangazi licha ya kuwepo na miundombinu ya maji lakini haitoi maji kabisa.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo la Ulanga Mhe SALIM Alaudin Hasham amesema Changamoto ya maji katika jimbo hilo ni kubwa hivyo hawezi kuiachia Serikali pekee bali ataendelea kutafuta wadau wengi kwa lengo la kuhakikisha Changamoto hio inapungua kama sio kuisha kabisa.

Visima hivyo vinne vimechimbwa katika kata tatu ambazo ni EUGA, Chilombora, Uponera na Kichangani na tayari vinaendelea kutoa huduma za maji. Wilaya ya Ulanga ina wananchi zaidi ya laki mbili (200000) ambao wanahitaji maji kiasi cha lita 1,600,000 lakini kwasasa wanapata lita 9000 pekee ambazo hazitoshelezi mahitaji yao.
Tumelogwa
 
Back
Top Bottom