Fredrick Nwaka
Member
- Jul 8, 2013
- 54
- 76
Na Sophia Kiyenze
Tuzo ya amani ya Nobel ni mojawapo ya tuzo kubwa na zenye heshima kubwa duniani ambazo zimekuwa zikitolewa kwa zaidi ya miaka mia moja sasa.
Wako watu mashuhuri duniani waliowahi kutunukiwa tuzo hiyo ambayo hutambua mchango wa mtu katika nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, sanaa, sayansi n.k.
Kwa sasa nikiwa hapa nchini Norway nimetembelea kituo cha Nobel Peace Center kilichopo jijini Oslo na nakuletea kumbukumbu za baadhi ya waafrika waliowahi kutunukiwa tuzo hiyo.
Nelson Mandela.
Hakuna mtu duniani asiyemfahamu Nelson Mandela, shujaa wa siasa za mapambano ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Mandela ambaye alifungwa gerezani kwa miaka 27 mwaka 1993 alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel kwa jitihada zake za kutumia njia ya amani kumaliza siasa za ubaguzi wa rangi. Aidha Mandela alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake wa kuihiza maridhiano baina ya watu wa Afrika Kusini. Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini na aliliongoza taifa hilo kutoka mwaka 1994 hadi mwaka 1999 alipokabidhi kijiti kwa Thabo Mbeki.
Abiy Ahmed
Ahmed ni waziri mkuu wa Ethiopia na anawakilisha kizazi cha sasa cha viongozi wa Afrika. Mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 42 Ahmed alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na jitihada kubwa alizofanya za kumaliza mzozo baina ya Ethiopia na jirani yake Eritrea. Aidha kiongozi huyo alitajwa kuanzisha maridhiano muhimu yaliyotoa matumaini ya maisha mema kwa raia wa mataifa hayo.
Wangari Maathai
Huyu anasalia kuwa mwanamke wa kwanza kutoka barani Afrika kuwa kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. Pia ilikuwa mara ya kwanza kwa tuzo ya Nobel kutunukiwa kwenye eneo la mazingira. Mwaka 1977 Maathai aliaznisha vuguvugu la Green Belt. Jitihada zake za kutafuta suluhu dhidi ya changamoto za kimazingira ikiwemo ukataji wa miti zilitambuliwa kama sehemu ya jitihada za kidemokrasia ambazo zilikabiliwa na udhibiti kutoka kwa serikali ya Kenya.
Sophia Kiyenze ni mwanafunzi wa shahada ya umahiri ya mawasiliano kwa umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa sasa yupo nchini Norway kwa mafunzo ya muda mfupi ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Oslo Metropolitan.