Hata mimi nimeshangaa sana kura za maoni zilihesabiwsa hadharani, mbele ya luninga na washindi wakapatikana live, leo unakuja kumkata na kumuengua mshindi unampachika aliyeshindwa! Mbaya zaidi kuna wengine waliorudishwa hata nafasi ya pili iliwakimbia! Pia sjajua kigezo hasa ni kipi maana kama kigezo ni rushwa , wapo waliotoa Rushwa na wakalalamikiwa lakini wamepitishwa!
Ushauri wangu ndugu zangu wanaCCM ambao mmekipigania chama hicho miaka kibao na kujiandaa kwa gharama za kiuchumi na kuutoa pia muda wenu, leo unatimiza ndoto yako ya kushinda, unakatwa kisha nafasi anapewa mamluki hata miezi 6 ndani ya CCM bado hajatimiza! Sasa chakufanya msianze kuhama wala kutoa matamko, bali shugulikeni mkiwa ndani humohumo, waelewesheni wanachama wengine wote uonevu uliofanyika kisha , waungeni mkono wapinzani kwa kuwapa kura zenu huku mkiwapa pia plani ya vita inayosukwa na CCM kuelekea uchaguzi mkuu!