Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Hilo jimbo lilikuwa linamfaa Abui Mukadam Nyuki wa Runzewe
 
Ni haki yake na anafaa upinzani sababu ni critic ila hasira za hivi hazina mwisho mzuri. Siasa zina hesabu zake, hata akienda upande mwingine kwa CCM ya awamu hii atashindwa tu! Akijichanganya tu ameharibu mazima.
Ccm ya sasa inanini kwamba inakubalika labda tu nikupe pole subir uone katambi akishinda hapa shinyanga nilipo Mimi nakunya hazarani
 
Haya CDM mchukueni..mnapenda makapi
 
Anaandika Dr. Christopher Cyrilo,

Adadi Mohammed Rajabu Meta, mkurugenzi mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa zamani, mbunge wa jimbo la Muheza aliyemaliza muda wake, pia aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya ndani na usalama.

Huyu aliwahi kuitaka serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani itoe maelezo ya kutosha kuhusiana na matukio ya utekaji, utesaji na mashambulizi kwa viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge. Ni baada ya tukio la kushambuliwa Tundu Antipass Lissu.

Akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya ndani, ulinzi na usalama, ripoti yake ya uchunguzi wa matukio ya utekaji na mashambulizi yaliyofanywa na watu "wasiojulikana" ilinyofolewa na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, hukohuko bungeni.

Kwenye kura za maoni alipata kura 597, dhidi ya mtia nia mwingine Hamis Mwinjuma (Mwana FA) aliyepata kura 296.

Hamis Mwinjuma ameteuliwa kuwania ubunge Jimbo la Muheza.

Nampongeza Hamis Mwinjuma kwa kupewa nafasi hii ya kugombea ubunge nyumbani kwetu Muheza. Lakini niseme tu kwamba mazingira ya kupata nafasi hii si mazuri sana. Kijana kama anayajua mambo haya basi atakuwa mtu mwenye kutafakari sana wakati huu, ila kama haelewi atakuwa mwenye furaha. Kuhusu ushindi, kwake litakuwa jambo la bahati.

Tukutane Muheza!
FB_IMG_1597941073982.jpg
FB_IMG_1597941381608.jpg
 
Yani kwa Shinyanga mjini meza imepinduliwa vibaya mno.

Huyu jamaa akibaki CCM nameza kisu!
Mkuu kwa ninavyo mfahamu Masele, sidhani kama atathubutu kuhama. Ila tusimalize maneno ngoja tuone..
 
Dar es Salaam
Jimbo la Kawe
- Askofu Josephat Gwajima

Tanga
Jimbo la Muheza
- Hamis Mwinjuma (Mwana FA)

Mbeya
Jimbo la Tunduma
- David Silinde

Manyara
Jimbo la Babati Mjini

- Pauline Gekul

Kilimanjaro
Jimbo la Vunjo

- Charles Kimei

Shinyanga
Jimbo la Shinyanga Mjini
- Patrobas Katambi

Mtwara
Jimbo la Ndanda
- Cecil Mwambe

Geita
Jimbo la Busanda

- Tumaini Braison Magesa

Kagera
Jimbo la Bukoba Mjini
- Stevine Lujahuka Byabato

Katavi
Jimbo la Kavuu
- Jofrey Mizengo Pinda

Kigoma
Jimbo la Kusini/ Uvinza
- Nashon Bidyanguze

Rukwa
Jimbo la Nkasi Kusini
- Vincent Mbogo

Ruvuma
Jimbo la Mbinga Mjini

- Jonas Mbunda

Jimbo la Namtumbo
- Kawawa Vita Rashid

Njombe
Jimbo la Wanging'ombe
- Dk. Festo John Dugange

Tabora
Jimbo la Kaliua
- Aloyce Kwezi

Shinyanga
Jimbo la Kishapu

- Boniface Butondo

Wafuatao ni wagombea Waliogongana idadi ya kura za maoni lakini akapitishwa mmoja:
Morogoro
Jimbo la Mlimba

- Godwin Kunambi

Mwanza
Jimbo la Buchosa

- Erick Shigongo

Mara
Jimbo la Mwibara
- Charles Kajege


= Orodha zaidi inakujia hivi punde =

Pia Soma
= > Uchaguzi 2020 - Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020

= > Uchaguzi 2020 - Yanayojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Wagombea Ubunge na Uwakilishi kujulikana leo
Nimefirahi silinde kupitishwa.
 
Dogo hafiki mbali...kazi ishaisha Muheza!!
Kama unabisha sawa ila ubishi wako utakiwa ni wa ukoo!!

Hongera uliyeongoza na ukapotezewa ushindi, historia itakukumbuka!! ulifanya kwa HAKI ila kamati roo mbaya ya chama chako imefanya yake!!
 
Masele kuama hawezi atavumilia hivyo hivyo lakini Katambi asijiakikishie kuwa tayari ashakuwa mbunge
 
Ni haki yake na anafaa upinzani sababu ni critic ila hasira za hivi hazina mwisho mzuri. Siasa zina hesabu zake, hata akienda upande mwingine kwa CCM ya awamu hii atashindwa tu! Akijichanganya tu ameharibu mazima.
CCM-MPYA haina kitu. Ni nguvu ya mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom