Wafahamu Mawaziri na Manaibu ‘waliotemwa’ na Rais Magufuli katika Baraza jipya la Mawaziri

Wafahamu Mawaziri na Manaibu ‘waliotemwa’ na Rais Magufuli katika Baraza jipya la Mawaziri

Baada ya Rais Magufuli kuteua Baraza jipya la Mawaziri atakalofanya nalo kazi baada ya kuwa Rais katika muhula wa pili. Katika Baraza hilo jipya, Rais amewatema Mawaziri 7 na kuchagua wengine

Waliotemwa ni;

1. Aliyekuwa Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa


2. Aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina

3. Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla

4. Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi, Isaac Kamwelwe

5. Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Josephat Hasunga

6. Aliyekuwa Waziri wa Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu


Manaibu Waziri walioachwa kwenye Baraza Jipya la Mawaziri ni;

1. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza

2. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde

3. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya

4. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni

5. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo

6. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu

7. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atashanta Nditiye

8. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira, Mussa Sima

9. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa

10. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu

11. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji

12. Aliyekuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Sinkamba Kandege
Hii list ikimsahau naibu waziri wa utawala bora DK Mery mwanjelwa
 
Mavunde imekuwaje? Au ni mtafuta nafasi na yeye, ikaonekana akatwe mapema?? Maana hata uWaziri kamili hakupewa kipindi kile! Vijana bwana wana mambo.. akajiingiza na yeye Yanga sijui GSM [emoji2296]
 
Kigwangallah kapewa muda wa kutosha wa kujibizana na Mo Dewji huko Twitter kuhusu masuala ya uwekezaji wa bilioni 20 na muda wa kuongea na Shangazi wakifundishana lugha ya kingereza kwa kukosoana.
 
Waliotemwa ni;

5. Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Josephat Hasunga
HUYU SIKUELEWA HATA ALICHOKUWA ANAFANYA NA NILIHISI KABISA NAIBU WAKE BASHE ALIKUWA NA KASI NA MWELEKEO SAHIHI KUSHINDA BOSS WAKE. SIKUTEGEMEA KAMA ANGERUDI
Wakati wa intervention ya Serikali kununua korosho za wakulima huko Mtwara, Serikali iliwahi kutoa fedha ili wakulima walipwe kulingana na idadi ya kilo za korosho walizokuwa wameuza. Kwa hiyo hela ilitolewa kulingana na idadi ya kilo za kila mkulima aliyeiuzia korosho Serikali. Kwa hiyo pesa iliyotolewa ilikuwa inawiana na idadi ya kilo za Korosho. Hata hivyo, mara baada ya pesa kutolewa ili kila mkulima wa korosho aweze kulipwa, baadhi ya pesa hizo zikaibiwa tena, na baadhi ya wakulima wa korosho wakakosa tena pesa.

Sasa mimi sikuelewa hii pesa namna ilivyoibiwa. Hii pesa mpaka leo huwa najiuliza ilibiwaibiwaje? Kosa jingine tena likafanyika nikamuona mh waziri yuko mbele ya media anongelea swala la wizi wa pesa hizo.

Labda kama kuna mtu wa kunielewesha kuhusu swala hili, kwamba hizi pesa ziliibiwaje wakati idadi ya kilo na pesa vilikuwa vinawiana?
 
Dah.!! Kamwelwe huyu mzee mbona alikuwa akipiga sana kazi
Aliwahi kumdhalilisha waziri mkuu hadharani
kuna sehemu alifika akauliza,mbonammmefanya hivi,mtaalamu akajibu tumefanya kwa maelekezo ya waziri ya waziri mkuu,Kamwelwe badala ya kunywea akaumua na kufoka"waziri mkuu ndio nani"!!!!
 
Back
Top Bottom