Wafahamu waarabu/usiyoyajua kuhusu waarabu

Huenda ni kweli Japo nami niliaminishwa hivyo shule, lakin hata ukiangalia vitabu vya history picha nyingi za warabu ni zakuchora tu. Ila wazumgu ni picha kabisa zilizopigwa na camera. So, huenda ni kweli na bado natamani kujua zaidi black and white kuhusu wahusika wa utumwa baina ya warabu na Wazungu.
 
mkuu Kilawo na tupo wengi tu kaka. Jirani zangu hapo mama yao alikuwa mtumwa kutoka kilwa. Aliolewa na Muarabu na watoto wakabahatika kwenda shule mmoja wao ni Meneja wa Bank moja kubwa tu huku tulipo ni juzi tu nimetoka kula futari kwenye villa yake. Mwegine ni mchezaji mpira analipwa fedha ndefu na ako na maisha mazuri sana tu. Mkuu Kilawo hizi huwa ni dhana tu za watu wanazipata kupitia vitabu tu lakini ukweli ndio huo. Wapo walioowa na kuolewa ingawa inawezekana ni kwa idadi ndogo lakini wapo.
 
Mashuleni wanafundisha Historia kupitia story ambayo Serikali inataka iwe. Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli tu, aliekuwa akiuza na kununua watumwa ndio hao hao wazungu wanaoabudiwa leo na kuonekana wa maana. Wamekuja Afrika wakafisidi rasilimali zetu, wakawachukuwa waafrika na kwenda kuwatuma marekani mashambani. Mwarabu kaja hata hakufika mbali, kaishia Lamu hapo basi tena utakuta story zinavozungumzwa kumfanya muarabu aonekane kinara wa utumwa, watu hata hawafikirii, kinara wa utumwa ata Uganda hajafika? Je wale waliotawala Afrika Nzima wao watakuwa nani? Tusirudi nyuma sana, SA tu apo si juzi jamaa katiwa kwenye shimo la mavi na wazungu?

Mwarabu kaja Zanzibar, kapapenda, akaleta Maendeleo, TV channel ya Kwanza Zanzibar, Taa barabarani kabla New york ni Zanzibar, Gorofa EA nzima ni Zanzibar, Mifereji majumbani kwanza Zanzibar, Zanzibar hio hio ilikuwa ikitoa misaada kwa uingereze wakati wa Vita, Leo eti wanasema Mwarabu kinara wa utumwa, Utumwa huo kamtuma nani? Hebu na waje waniambie, mwarabu kaondoka Zanzibar au Afrika na rasilimali gani? Karafuu zenyewe pemba kazileta Mwarabu kutoka bara la Asia uko.

Waniambie rasilimali waliowapokonya waafrika hawa waarabu ni ipi kiasi kwamba waitwe vinara wa utumwa?

Mpaka Kesho Afrika inaibiwa rasilimali na Wazungu, nenda Congo tu apo uone ukoloni wa mamboleo!

Walisema kuwa Beit Al Aab (house of Wonder) Nguzo zake zilijengwa kwa vichwa vya watumwa. Mungu Kawadhalilisha lile jengo miaka michache nyuma liliporomoka Nguzo, hakuna ata kipande cha mfupa wa kuku. Zile zama za kudanganywa zimekwisha, siku izi mambo yapo wazi!

Walisema Bi Khole alikuwa analala na mtumwa kila siku akisha anamkata uume wake..... Ukiwauliza ushahidi hawana! Wapo kuchafua historia ya watu tu, wanataka tuamini kuwa utawala wa kisultani ulikuwa wa kidhulma, huu wa saivi tuuite vipi basi? Zanzibar ipo nyuma kwenye kila kitu.
 
Nimekuja mbiyo nikijua utazungumzia adhabu za kukata kichwa, kukata mikono na kuua kwa kuponda na mawe
 
Mkuu nitakupa dokezo kwa swali lako.
1. Biashara ya Utumwa iliyofanyika Afrika Magharibi inaitwa WEST AFRICAN SLAVE TRADE
2. Biashara ya Utumwa iliyofanyika Africa Mashariki inaitwa EAST AFRICA ARAB SLAVE TRADE

Unapata hisia yoyote kwanini ile # 1 hamna neno European?? Ila kwenye hii # 2 neno Arab ni MUHIMU?? Ukiwaza vyema utajua.
 
Acha ubishi usio naamaana wewe "" ..kutetea tetra ujinga tu ....""" Yule billali bin wabaa ...swahaba wa mtume ambaye alikuwa na asili ya Ethiopia alifikaje Makkah...wakati alikuwa mtumwa kule
 
Too bad hujasoma Historia....kamsome Tippu tippu kwanza.
 
Acha ubishi usio naamaana wewe "" ..kutetea tetra ujinga tu ....""" Yule billali bin wabaa ...swahaba wa mtume ambaye alikuwa na asili ya Ethiopia alifikaje Makkah...wakati alikuwa mtumwa kule
Sijasema kuwa waarabu hawakufanya utumwa totally, waarabu hawakufanya utumwa kama mnavojidai. By the way, Who freed Bilal?
 
Too bad hujasoma Historia....kamsome Tippu tippu kwanza.
Historia mnayofundishwa mashuleni? Nimeisoma hio, lakini ndio yale yale nloyasema, ni historia ambayo Serikali inataka iwe hivo.

Tulifundishwa mashuleni kuwa House of Wonder Nguzo zake zimejengwa kwa vichwa vya watumwa ndio maana zile nguzo zipo very strong, miaka michache nyuma jumba liliporomoka upande mmoja, mfupa wa jogoo hamna ndani yake, saa bufur la hao watumwa liko wapi kwenye izo nguzo kama wanavofundisha watoto?
 
Pale kanisa la Anglican Mkunazini kuna caves zinaenda mpaka darajani na ndio ilikuwa njia ya kupitishia watumwa kuwaingiza kwenye majahazi ni nani alikuwa anafanya hiyo biashara?
 
Nakuelewa! Ila mkuu naomba niambie, hao wazungu walipokua wakifanya hiyo biashara hapa EA, warabu walikua wameshaondoka? Ina maana hawakuhusika hata kidogo? Au walihusika lkn si kwanamna wanvyozungumzwa?
Kuna taarifa kuwa wao walikua madalali.
 
Nakuelewa! Ila mkuu naomba niambie, hao wazungu walipokua wakifanya hiyo biashara hapa EA, warabu walikua wameshaondoka? Ina maana hawakuhusika hata kidogo? Au walihusika lkn si kwanamna wanvyozungumzwa? Kuna taarifa kuwa wao walikua madalali.

Kwanza ieleweke hamna jamii ambayo inawza kujitoa kwenye lawama za biashara ya utumwa. Lakini inabidi kuelewa kuwa majina ya East Africa ARAB slave Trade dhidi ya West African Slave Trade ni mkakati wa wazungu hususan Wamissionary wa enzi zile kuwachora Waarabu kama kuwa ndio pekee waliokuwa wakifanya jambo hili. Wazungu WOTE waliokuja kutafuta vyanzo vya Nile au kuiona Milima na Maziwa kama Tanganyika walielekezwa na Waarabu hapo Unguja. Lakini HAMNA walipodiriki kulipa fadhila kwa kuwataja HAO waliowaelekeza.

Cha kukusaidia ni kwamba JIULIZE mbona pamoja na Waarabu kuwatangulia wazungu huku kwetu kwa miaka karibia 800, mbona HAMNA historia ya waarabu WAKIZIPIGA na wabantu?? Kwanini?? Kama kweli walihamisha wabantu wote kama watumwa (sisemi hawakufanya!!) mbona hamna mahali walizipiga?? Kuna mtu anapandikiza FITNA
 
Acha ubishi usio naamaana wewe "" ..kutetea tetra ujinga tu ....""" Yule billali bin wabaa ...swahaba wa mtume ambaye alikuwa na asili ya Ethiopia alifikaje Makkah...wakati alikuwa mtumwa kule
Du kumbe unamfahamu huyu Jamaa. Kweli alikuwa mtumwa. Ila Mtume Muhammad Akamkomboa kutoka utumwani ila wengi hutaka kuhusisha kuwa waislam ndio walikuwa wanawafanya watumwa.
 
Umeleza ilivyo vizur mno kama vile ccm kwa nje hujasema kwa ndani ila tuyaache hayo
 
Umekazania zanziba zanzibar zanzibar zanzibar...



Nakukumbusha pia Mwarabu pia Alipita Ujiji,kilwa,Kondoa,kilosa,Bagamoyo,tabora,nzega,Mtwara n.k


Sasa naomba hoja zako zijikite na hayo maeneo mengine.



Hiyo Zanzibar yenyewe Njaa tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…