Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,196
Hakuna Mwenye nafuu naona mnahangaika tu ,..na kupaza shingo zenu kwa kusifia watu ""... waarabu na wazungu wote walifanya biashara ya utumwa ""... waliwatesa mababu na mabibi zetu vile walivyojisikia...so kutaka kutetea upande huo "" ni ujinga ...ukisoma vitabu vya dini kama Qur'an vinasema wazi kuwa mtume alikuta "" biashara ya utumwa ikiwa inafanyika "" na yeye ndiye aliye ikomesha katika wakati wake "" lakini alipoondoka biashara hii ilirudi tena kwa kasi "" tu " kama mlikuwa hamjui waarabu walikuwa wana wanunua Hawa watumwa toka kwa machifu wa wakati huo "" .... mkwawa amefanya sana biashara hii na waarabu ...na mtu mpaka unafnywa mtumwa means lazima "" kuna mates makubwa utakayo yapitia na hali ya kutendewa ubaya uliovuka utu ......"" wazungu washenzi na waarabu pia ni washenzi ....hakuna Mwenye nafuu tusiongopeane hapa
Mkuu, asante kwa hoja nzuri. Hakuna anayekataa kuwa hakukuwahi kutokea utumwa. Wala hamna anayedai Uafadhali wa utumwa fulani. NO. Ushahidi wa utumwa na madhila yake kihistoria upo. Ni kama mchangiaji mmoja alivyoonyesha kuwa maeneo ya Iraqi kuna weusi wa kiafrika (Zanj) ambao walifika huko kama watumwa, alichokiacha ni kuwa hawa Zanj baadae waliasi na kujitwalia maeneo ya Iraq na Iran japo baadae walishindwa kivita Zanj rebellion | ʿAbbāsid history. Ila kuwapo kwao hawa Zanj hadi leo hii ni dalili kuwa simulizi za KUWAHASI waafrika wanaume WOTE huko bara Arabu sio kweli. Wapo pia Weusi barani Hindi wakijulikana kama Siddi India’s forgotten African tribe ambao pia walifika huko kama watumwa. Hawa pia hawaishi kwa RAHA. Waingereza wanajulikana kwa kuwauza WAZUNGU wenzao (Irish Slaves) utumwani White Cargo japo ukiwasoma siku hizi ni kama vile wanaelekea kukana kwamba vijana wa Ki-Irish waliowauza utumwani kwenye mashamba ya tumbaku na sukari hawakuwa watumwa.
Tofauti iliyopo ni kuwa;
1. Wazungu hawaweki neno "European" kwenye ile biashara waliyoifanya West Africa ila wanaweka neno "Arab" kwenye hii ya East Africa, lengo halijulikani
2. Hakuna maelezo kwanini waafrika (popote) HAWAKUZIPIGA na hawa Waarabu waliowafanya watumwa ila WAKAZIPIGA (sehemu nyingi sana) na Wazungu, tatizo lipo hapo