Mashuleni wanafundisha Historia kupitia story ambayo Serikali inataka iwe. Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli tu, aliekuwa akiuza na kununua watumwa ndio hao hao wazungu wanaoabudiwa leo na kuonekana wa maana. Wamekuja Afrika wakafisidi rasilimali zetu, wakawachukuwa waafrika na kwenda kuwatuma marekani mashambani. Mwarabu kaja hata hakufika mbali, kaishia Lamu hapo basi tena utakuta story zinavozungumzwa kumfanya muarabu aonekane kinara wa utumwa, watu hata hawafikirii, kinara wa utumwa ata Uganda hajafika? Je wale waliotawala Afrika Nzima wao watakuwa nani? Tusirudi nyuma sana, SA tu apo si juzi jamaa katiwa kwenye shimo la mavi na wazungu?
Mwarabu kaja Zanzibar, kapapenda, akaleta Maendeleo, TV channel ya Kwanza Zanzibar, Taa barabarani kabla New york ni Zanzibar, Gorofa EA nzima ni Zanzibar, Mifereji majumbani kwanza Zanzibar, Zanzibar hio hio ilikuwa ikitoa misaada kwa uingereze wakati wa Vita, Leo eti wanasema Mwarabu kinara wa utumwa, Utumwa huo kamtuma nani? Hebu na waje waniambie, mwarabu kaondoka Zanzibar au Afrika na rasilimali gani? Karafuu zenyewe pemba kazileta Mwarabu kutoka bara la Asia uko.
Waniambie rasilimali waliowapokonya waafrika hawa waarabu ni ipi kiasi kwamba waitwe vinara wa utumwa?
Mpaka Kesho Afrika inaibiwa rasilimali na Wazungu, nenda Congo tu apo uone ukoloni wa mamboleo!
Walisema kuwa Beit Al Aab (house of Wonder) Nguzo zake zilijengwa kwa vichwa vya watumwa. Mungu Kawadhalilisha lile jengo miaka michache nyuma liliporomoka Nguzo, hakuna ata kipande cha mfupa wa kuku. Zile zama za kudanganywa zimekwisha, siku izi mambo yapo wazi!
Walisema Bi Khole alikuwa analala na mtumwa kila siku akisha anamkata uume wake..... Ukiwauliza ushahidi hawana! Wapo kuchafua historia ya watu tu, wanataka tuamini kuwa utawala wa kisultani ulikuwa wa kidhulma, huu wa saivi tuuite vipi basi? Zanzibar ipo nyuma kwenye kila kitu.