Wafanya biashara Lipeni kodi acheni ubabaishaji

Wafanya biashara Lipeni kodi acheni ubabaishaji

Zitto Kabwe

EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni. Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000.

Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika.
Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila kusubiri kurejeshewa kupitia kodi. Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa matumizi).
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?
Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?
Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba.........​





swala la kugoma kulipa kodi ni kutoitendea haki serikali,wafanya kazi tunalipa kodi ya kichwa-kodi ya mapato,tunalipa VAT,bado tunalipa kodi ktk vitu tunavyonunua.
wafanyabiashara acheni ubabaishaji,lipeni kodi kwa manufaa ya Taifa hili,huu si wakati wa kugomea hizo machine na mbona nchi nyingi tu wanatumia hizi machine? inakuwaje nyie hapa Tanzania mnaleta mgomo eti hamtaki kulipa kodi?
Hapana,wafanyabiashara lipeni kodi kwa maendeleo ya Taifa hili

mnapokwenda china kununua vitu,mnapewa risiti toka ktk vimeshine ambavyo hapa mnavigomea,lakini mkiwa china hamgomi kupokea risiti inayokuonyesha kodi kiasi gani umelipia toka ktk ile bidhaa uliyonunulia,mnaogopa kugoma mkija china kwani mnaelewa serikali ya china haiwezi kuwaonea huruma na itawang'oa shingo,lakini mnaporudi na mzigo Tanzania mnagomea machine hizo na tena pesa yenyewe inatoka kwa wanunuaji ndio wanaolipa kila aina ya kodi unayotakiwa kulipa.
Hapana lipeni kodi wafanyabiashara.

Wrong.
Wafanya biashara hawa 16000 ni wale big ones.
Kina bakhressa na kampuni zake.bia na kampuni zao. Soda zote.
Tanesco na luku zake.makampuni ya ndege.masupermarket.boti za zanzibar.
Kampuni za ujenzi
Dawasco na kama hizo
Gloceries na kama hizo
Waagiziaji magari
Wauzaji vipuri
Maduka ya electriniki
Maduka makubwa ya vivaa vya ujenzi.nk...nk

Wafanyabiashara hawa wote biashara na mauzo yao kwa siku ni zaidi ya shs million 5
Sasa wewe ukifanya hesabu ya haraka haraka utaona VAT inayotakiwa kulipwa na hawa 16000 registred vat basi sio chini ya Billion 5000.
Leo anakuja waziri kivuli ati machine hizi zinasaidia !!
Ukweli hizi machine ni deal kwa wale wa VAT wanazifuarahia.hesabu inayo rekodiwa ndio hio hio kisheria huwezi tena kumzidishia.
Ndugu Zito kaa fanya utafiti sawa sawa utafahamu kuwa EFD hazijasaidia kitu.
Figure kuongezeka ni kawaida kila mwaka mapato yanaongezeka kutokana factors nyingi sana.
EFD kwa hawa wa chini ya sales ya 14m ni sawa ikiwa mtawapa machine bure na pia kuwa wazi mtatokotoa vipi kodi kutoka hawa ambao sio VAT regelistred?
 
tena kodi kama vat hawalipi wao,wao ni mawakala tu wa kuikusanyia serikali,anaelipa ni mlaji wa mwisho.walipe wasitutanie kabisa hawa!

......hili suala watu wengi hawalitambui.....wafanyabiashara ni mawakala.......wanachogomea sio mashine....ila hizo mashine hazitawapa nafasi ya wao kufanya mazagazaga......na mapato yao yakiripotiwa kwa usahihi watatakiw akulipa kodi husika.......sasa hivi wafanya biashara wengi hawalipi kodi ipasavyo.......kwani ni vigumu kufuatilia mauzo yao.....
 
......hili suala watu wengi hawalitambui.....wafanyabiashara ni mawakala.......wanachogomea sio mashine....ila hizo mashine hazitawapa nafasi ya wao kufanya mazagazaga......na mapato yao yakiripotiwa kwa usahihi watatakiw akulipa kodi husika.......sasa hivi wafanya biashara wengi hawalipi kodi ipasavyo.......kwani ni vigumu kufuatilia mauzo yao.....

Hapo mkuu umenena,hilo ndio tatizo la wafanya biashara wakitanzania,ujanja ujanja mwingi sana,hizi machine zinatumika kila kona ya Dunia,iweje hapa bongo tu ndio tujifanye eti ni makini zaidi na kuzitia kasoro hizi machine?
hawa jamaa waisaidie tu serikali kukusanya kodi tunayolipa sisi walaji wa mwisho.
wengi wao wanasafiri kwenda china na wanaponunua vitu ktk maduka ya uchina wanakutana na risiti kutoka ktk hizi machine ikimaanisha kuwa wamekubali kulipa kodi wakiwa uchina,lakini wanapofika Tanzania hawataki kuzitumia machine zilezile ili kuisadia serikali kukusanya kodi, kwanini?
 
Mkuu tatizo kubwa hapa ni gharama za ununuzi wa hizo mashine.. Mie nina duka langu ambalo mtaji wake ni milioni mbili.. Humo ndani nina muuzaji ambae analipwa.. Kuna kodi ya pango ambayo inalipwa.. kuna malipo ya TRA ya mwaka (ambayo minimum makadirio ni shilingi 290,000.. umeme ambao ni shilingi 60,000 kwa mwezi.. bado kuna ushuru wa uchafu ambao unatakiwa ulipe.. Juu ya yote hayo unakuja kupewa mzigo wa kununua mashine kwa shilingi 600,000..! Piga hesabu hapo uone kama kuna uwezo wa kununua hiyo mashine..

Ingekuwa ni vema wakatoa kwa mkopo mdogo ambao mfanyabiashara anaweza ku-afford kulipa.. Wangefanya hivyo ingeweza sana kusaidia kwa TRA na kwa mfanyabiashara pia..

NB: Hapa ninawazungumzia wafanyabiashara wadogo sio wale wakubwa ambao naona wameingilia kati na kulifanya hili ni la kwao..

Hata wewe Mkuu hili suala nawe umelivamia si la kwako TRA wameainisha hapo Wafanyabiashara wenye Mapato ghafi ya Tshs 14 Milioni kwa Mwaka wewe wa Milioni 2 unahusika nyinyi ndiyo wapotoshaji hujui lolote unakomenti!
 
Hata wewe Mkuu hili suala nawe umelivamia si la kwako TRA wameainisha hapo Wafanyabiashara wenye Mapato ghafi ya Tshs 14 Milioni kwa Mwaka wewe wa Milioni 2 unahusika nyinyi ndiyo wapotoshaji hujui lolote unakomenti!

Umeona tatizo lilipo.maana unashangaa hadi mama ntilie na wamachinga nao eti waligoma.hii inaonyesha jinsi upotoshaji wa makusudi ulifanywa ili kuwabeba wakwepa kodi
 
Hata wewe Mkuu hili suala nawe umelivamia si la kwako TRA wameainisha hapo Wafanyabiashara wenye Mapato ghafi ya Tshs 14 Milioni kwa Mwaka wewe wa Milioni 2 unahusika nyinyi ndiyo wapotoshaji hujui lolote unakomenti!

Ungesoma comment yangu yote usingekuja na hilo uliloliandika au pengine basi una upungufu wa kuelewa.. Tatizo kubwa hapa kwa wafanyabiashara wadogo ni kulazimishwa kununua fiscal machine kwa gharama ya Tshs. 800,000 (ambayo sasa wamepunguza mpaka laki 600,000).. Kwetu sie hatuna matatizo na matumizi ya mashine hizo.. Ila gharama ya kununua hatuiwezi.. Kinachotokea hapa ni wafanyabiasha wakubwa ku-hijack hii vurumai na kuingiza matakwa yao..
Mwisho ungesoma kwenye comment yangu hapo kwenye NB..
Hope umenielewa.. Halafu kuwa na lugha ya dialogue ili elimu tuipate wote..
 
Kabla ya maneno na lawama je mnajua kuwa efd machine hutumia network kama simu?je unajua kuwa network ikikata huwezi fanya biashara mpaka irudi au update barua kutoka track ya kukuruhusu kufanya biashara au sivyo fungal duka mpaka net irudi
 
kama wafanyabiashara ni mawakala wa kuikusanyia kodi serikali ni kwa nini hizo mashine wasingezipewa bore?unless kama kuna malipo wanapata kutokana na kukusanya kodi hiyo
 
Serikali iwape BURE tu ili kuondoa sababu,...watavuna pesa mingi sana TRA,
ila naona ugumu kwa taxpayer kutoa hela bila shuruti unakuwepo kutokana na matymizi ovyo ya serikali,mtu haoni govt inamsaidia nini,so bora ajiibie tu afaidi...
Nchi km Denmark nasikia taxes up to 70%,(corporate tax nafkr).,they get a lot in return,health,maji ,umeme ,infrastructure nzuri nk,so haiumi kivileee....
Hehhehe hapa bongo jee..lazma watu waandamanee japo quid-pro quo ni kawaida kwenye kodi,
 
Chance ya wafanyabiashara ilobaki naona ni kuuza BAADHI YA VITU bila kutoa risiti...ili japo waibe hko ki'VAT kdogo (esp kwa wateja wasodai risiti)si itawezekana,??ama EFD can trace ur Stock,purchases and all that??
 
Back
Top Bottom