crabat
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 4,323
- 2,207
Zitto Kabwe
EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni. Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000.
Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika.
Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila kusubiri kurejeshewa kupitia kodi. Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa matumizi).
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?
Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?
Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba.........
swala la kugoma kulipa kodi ni kutoitendea haki serikali,wafanya kazi tunalipa kodi ya kichwa-kodi ya mapato,tunalipa VAT,bado tunalipa kodi ktk vitu tunavyonunua.
wafanyabiashara acheni ubabaishaji,lipeni kodi kwa manufaa ya Taifa hili,huu si wakati wa kugomea hizo machine na mbona nchi nyingi tu wanatumia hizi machine? inakuwaje nyie hapa Tanzania mnaleta mgomo eti hamtaki kulipa kodi?
Hapana,wafanyabiashara lipeni kodi kwa maendeleo ya Taifa hili
mnapokwenda china kununua vitu,mnapewa risiti toka ktk vimeshine ambavyo hapa mnavigomea,lakini mkiwa china hamgomi kupokea risiti inayokuonyesha kodi kiasi gani umelipia toka ktk ile bidhaa uliyonunulia,mnaogopa kugoma mkija china kwani mnaelewa serikali ya china haiwezi kuwaonea huruma na itawang'oa shingo,lakini mnaporudi na mzigo Tanzania mnagomea machine hizo na tena pesa yenyewe inatoka kwa wanunuaji ndio wanaolipa kila aina ya kodi unayotakiwa kulipa.
Hapana lipeni kodi wafanyabiashara.
Wrong.
Wafanya biashara hawa 16000 ni wale big ones.
Kina bakhressa na kampuni zake.bia na kampuni zao. Soda zote.
Tanesco na luku zake.makampuni ya ndege.masupermarket.boti za zanzibar.
Kampuni za ujenzi
Dawasco na kama hizo
Gloceries na kama hizo
Waagiziaji magari
Wauzaji vipuri
Maduka ya electriniki
Maduka makubwa ya vivaa vya ujenzi.nk...nk
Wafanyabiashara hawa wote biashara na mauzo yao kwa siku ni zaidi ya shs million 5
Sasa wewe ukifanya hesabu ya haraka haraka utaona VAT inayotakiwa kulipwa na hawa 16000 registred vat basi sio chini ya Billion 5000.
Leo anakuja waziri kivuli ati machine hizi zinasaidia !!
Ukweli hizi machine ni deal kwa wale wa VAT wanazifuarahia.hesabu inayo rekodiwa ndio hio hio kisheria huwezi tena kumzidishia.
Ndugu Zito kaa fanya utafiti sawa sawa utafahamu kuwa EFD hazijasaidia kitu.
Figure kuongezeka ni kawaida kila mwaka mapato yanaongezeka kutokana factors nyingi sana.
EFD kwa hawa wa chini ya sales ya 14m ni sawa ikiwa mtawapa machine bure na pia kuwa wazi mtatokotoa vipi kodi kutoka hawa ambao sio VAT regelistred?